Mpango huu wa Elimu ya mkoloni, tutakuja kuwa na upungufu watu wa sanaa na biashara

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Wizara ya Elimu ilitoa tamko kuwa wanafunzi wote wasome sayansi, mpaka hapo walimu wa masomo ya Sanaa na biashara hawana soko tunasomesha wasomi baadae tunawatelekeza sisi wenyewe, kwa miaka ya baadae kutakuja tokea ukosefu wa walimu masomo ya Sanaa na biashara kama ilivyosasa hamna walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi.

Je serikali inaweza jenga viwanda vya kuwaajiri wanafunzi walioshinikizwa wasome sayansi? Sayansi inayofundishwa ni ya viwanda au ndio hii ordinary science? Kwa nini serikali isirudishe TECHNICAL SCHOOLS? Ndio ziwe zinafundisha industrial science (elimu ya viwanda). Hawa walimu wa biashara na sanaa walio mtaani, walioajiriwa na walio vyuoni tunawapeleka wapi? Serikali inaanda wasomi halafu inakuja kuwatelekeza

Bado serikali inasomesha wakandarasi halafu bado tenda watapewa wengine, sawa sisi wakandarasi wazawa hatuna uzoefu juu kazi Fulani na miradi mipya nchini. Serikali inatutengenezea mazingira gani ili sisi tujifunze? Nilitarajia kwenye mikataba iwe inaorodhesha kuwa wakandarasi wa nje wawe wanashirikiana na wakandarasi wazawa iwe, iwe ni sheria kwenye mikataba ili sisi wakandarasi wa ndani tuweze pata maarifa juu ya teknolojia na ufanyaji kazi wa miradi iliyo migeni hapa nchini kama fly over Dar n.k

Wizara ya elimu inabidi ibadili mifumo ya elimu hapa nchini ili sera ya viwanda iweze tekelezwa kwa uhakika, swala la kunyima mikopo kwa wanafunzi wa vyuo waliotoka diploma ni ujinga wa hali ya juu. Kwa nchi yetu ni lazima tutoe kipaumbele kwenye mikopo kwa masomo ya sayansi ili tutoe motisha na kwa kutilia maanani fani za sayansi ni gharama sana kwa familia duni za kitanzania haziwezi mudu gharama hizo.

Wizara ya elimu pia yapaswa kuandaa mtahara mmoja wa nchi nzima, sio ukienda shule za wahindi wanakuwa na mitahala yao, mbona sisi tukienda tunasoma mitahala yao? kama yetu ina mapungufu basi tushirikiane kutunga mitahala mipya inayoendana na kizazi na mahitaji ya karne ya 21.
 
Back
Top Bottom