Mpanda: Mwalimu amuoa mwanafunzi wake


K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,208
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,208 280
wanafunzi-jpg.625292

BAADHI ya walimu wanaofundisha katika Shule za Sekondari za Katumba na Nkeswa zilizopo katika kambi ya wakimbizi ya Katumba wilayani Mpanda katika mkoa wa Katavi, wanatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike.

Aidha imeelezwa kuwa mmoja wao “amemuoa” mwanafunzi wake kwa kumtolea mahari kwa wazazi wake. Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Kakunda alielezwa hayo na Diwani wa Kata ya Katumba iliyopo katika Halmashauri ya Nsimbo, Seneta Baraka wakati alipokutana na madiwani na watumishi wa halmashauri ya Nsimbo katika majumuisho ya ziara yake ya siku moja aliyoifanya mkoani Katavi.

Akimsimulia mikasa ya walimu hao, Diwani Baraka alisema: “Nilishatoa taarifa ya mwalimu aliyemweka kinyumba mwanafunzi wake wa kike pia walimu wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike katika vikao vya baraza la madiwani, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yao badala yake baadhi ya madiwani wenzangu wamevujisha siri za vikao na kwenda kuwataarifu walimu hao kuwa mimi ndio ninayewashtaki,” alieleza.

Chanzo: Habari Leo
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
30,706
Likes
87,330
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
30,706 87,330 280
Apate ushauri kwa mzee Makamba snr
 
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Messages
4,357
Likes
1,314
Points
280
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2010
4,357 1,314 280
Mbaya sana Walimu wangu,hangaikeni na Mama zao.
 

Forum statistics

Threads 1,250,531
Members 481,403
Posts 29,736,682