kwani wao hawamo kwenye serkali ya muungano? Katika watu waliokwenda newyork ni pamoja na mjumbe mmoja kutoka zanzibar au jussa hakulijua hilo?written by amini // 19/01/2012 // habari // no comments
na mauwa mohammed, zanzibar
wajumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar wamehoji hatua ya serikali ya jamhuri ya muungano ya tanzania kupeleka maombi umoja wa mataifa (un) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari.
Kauli hiyo imewasilishwa na mwakilishi wa mji mkongwe (cuf), ismail jussa ladhu na kutaka kutoa hoja ili baraza hilo lijadili katika kikao kinachoendelea mjini zanzibar.
Alisema hatua hiyo ya serikali ya muungano ni nzito inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vema kwani waathirika wakuu huenda wakawa ni wazanzibari.
Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa leo katika ofisi za umoja huo new york, marekani.
Spika wa baraza la wawakilishi, pandu ameir kificho, alitumia busara kubwa na kuwataka wajumbe wasubiri na kuiagiza serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa tanzania.
Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa muungano kupeleka maombi hayo kwa umoja wa mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.
Aliitaka serikali ya mapinduzi ya zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya umoja wa mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo.
Naye mwakilishi wa kuteuliwa, ali mzee ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, profesa anna tibaijuka, anayedaiwa kusimamia na kuwasilisha hoja hiyo un, hakuweza kupatikana kutoa maelezo ya jambo hilo.
Jitihada za tanzania daima kuonana na tibaijuka ofisini kwake zilikwama baada ya kupewa maelezo kuwa waziri huyo alikuwa nje ya ofisi kwa shughuli za kikazi na kwamba asingeweza kurudi. Aidha, simu yake ya mkononi iliita mara nyingi bila kupokewa.
Chanzo tanzania daima
Je swala ili halikupita kwenye baraza la mawaziri?!
Hatutuna sababu ya kukubaliana katika hilo, kwani hata tukiamua sasa muungano ukavunjika, Zanzibar haiwezi kutambulia kama nchi mpaka sisi tukubali, kwa umbali ambao Zanzibar ipo, Sheria za Kimataifa za mipaka ya bahari haiitambui zanznibari kama nchi.
Hivyo achaneni na ndoto za mchana, hilo lingewezekana ingeanza Taiwan kutambuliwa kama nchi.
Sema ujinga wa viongozi wetu ndiyo unawapa kichwa na kuwajazeni ujinga, ila endeleeni kulalamika bila ya kuona, mwisho haitukuwa mzuri kwenu.
Kwani wakati wanapeleka hilo ombi la kuongeza eneo la bahari kulikuwa hakuna mawasiliano na SMZ? Mbona jambo hili linaleta utata. Mi nilifikiri SMZ ingefurahia jambo hilo?
Katika kikao cha leo Waziri wa ardhi na makaazi ametamka ya kwamba Kuhusu hili Baraza la mapinduzi halikupewa taarifa yeyote.
kwenye timu iloenda UN alikuwepo shah wa mafia na zakiah meghiji wa zanzbar,wamewakilishwa vizuri,ombi limeobwa na JMT na si upande mmoja kama huyu paka alichosema
Lazima kieleweke hapo.
Kwani kuna namna hapo na hila za kutaka kupora eneo huru la Zanzibar la rasilimali za bahari.
Hongera Jusa kwa kuona mbali.
Katika kikao cha leo Waziri wa ardhi na makaazi ametamka ya kwamba Kuhusu hili Baraza la mapinduzi halikupewa taarifa yeyote.
Lazima kieleweke hapo.
Kwani kuna namna hapo na hila za kutaka kupora eneo huru la Zanzibar la rasilimali za bahari.
Hongera Jusa kwa kuona mbali.
Hongera sana Ismail Jussa.
Kwani huo ni uvunjifu wa Katiba zote mbili ya Muungano na ile ya Znz. Ni lazima kieleweke hapo na kumjuza Prof Tibaijuka kuwa Znz ni nchi anapaswa kuiheshimu kwa dhati kabisa.
Hongera sana mwakilishi wangu.
Watanganyika bado mnaendelea kuwacheyea WaZANZIBARI? Subiri muone kali yao, sio wale mambumbumbu tena. Yangu macho.
Hongera sana Ismail Jussa.
Kwani huo ni uvunjifu wa Katiba zote mbili ya Muungano na ile ya Znz. Ni lazima kieleweke hapo na kumjuza Prof Tibaijuka kuwa Znz ni nchi anapaswa kuiheshimu kwa dhati kabisa.
Hongera sana mwakilishi wangu.