Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Je, huu sio mtego wa panya au wa samaki?
Nifuate hadi mwisho,
Solomon M. Kambarangwe
01/04/2016
Huu ni mtazamo wangu maana kwangu sitaki danganyatoto kwa kutumia fikra duni za wananchi waliojazwa ujinga kwa kunyimwa elimu na huo ujinga ndio mtaji wa ccm kuendelea kuifanya nchi yetu shamba la bibi, huo ndio ukweli jitafakarini maana kila kitu mnashangilia tu akili ya kutafakari inapewa likizo ya milele.
1. Watu wengi wameishasahaulishwa ubakaji wa demokrasia Zanzibar kwa Magufuri kusema kuwa atapunguza mishahara mikubwa.
2. Pigo la kunyimwa fedha za maendeleo limechukuliwa kama habari ya gari kugonga ng'ombe wawili.
3. Wana CCM wanachukulia CUF kujiondoa kwenye uchaguzi Zanzibar sawa na ule usemi wa "Hasira za Mkizi, Tija kwa mvuvi".
Kama ndivyo huo ni ukosefu wa akili hai na ni kile tunakiita "kujiteka na kujiua" (self assassination) kwasababu CUF sio Wakongoman au Waganda waliochaguliwa kuiongoza Zanzibar.
Ni Wazanzibar waliowachagua Wazanzibar wanachama wa Cuf kuingoza nchi yao kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.
Kwa akili zile zile za Hapa Kazi tu na:
kupiga picha vitanda Muhimbili vikishushwa na kuwekwa wardini na kurushwa kwenye Tv kuwa ni maajabu serikali kununua vitanda vya wagongwa.
Matukio ya Rais kukagua vifaa tiba MRI na CT Scan pale MoI mbele ya kamera za wanahabari.
Yakifanyika MoI ila hospitali 99% nchini hazina hivyo vifaa, madawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia wananchi katika hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa.
Swali vifaa hivyo vipo hospitali ya Taifa ya Muhimbili? Jibu mnalo.
Yalikuwa ni matukio lakini uhalisia mateso ya wagonjwa kukosa huduma ya vipimo vya MRI na CT Scan MoI bado liko pale pale kama hali iko hivyo Muhimbili jiulize huko Rukwa, Kigoma na mikoa mingine ya pembezoni hali ikoje?
Kumbukeni kuna familia nyingi kutokana na umasikini hata kufik hospitali za wilaya hawawezi kutokana na umasikini ulio urithi wa awamu nne za serikali za ccm kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 bado kuna wananchi zaidi ya 65% wanaishi maisha hohehahe ilhali nchi yetu tajili sana kwa maliasiri.
Magufuli ni mtoto wa ccm na tabia za ccm, alikuwa kweny serikali zilizopita, kuongea kujitofautisha na ccm ni uongo maana ni mwana ccm yule yule aliyekuwepo toka awamu ya kwanza hadi ya nne bila kukosoa chama chake.
Sasa kwa kutumia vitu rahisi kutafuta makubwa mithiri ya mtego wa samaki au wa panya kwangu nataka niweke wazi maoni yangu.
Huyu kada wa ccm alikuwa mbunge na waziri, wabunge wa upinzani walipoyasema maovu ya CCM na kupuuzwa Maspika wa ccm na wabunge wa ccm bungeni kwa lugha ya kejeli kuwa wanatafuta umaarufu alishiriki kupiga meza na wabunge wa ccm kubeza hoja za kutetea wananchi masikini wanaokufa kwa kukosa madawa na vifaa tiba hospitali, hata gloves, sindano ila:
#Kuna watumishi hewa lukuki nchini,
#kuna malipo hewa lukuki.
#Kuna mishahara mikubwa ya kufuru lukuki.
#Kuna ufisadi wa kutisha lukuki na maovu mengine mengi sana yanafanyika ila huyu mwenzetu aliisubili aseme akiwa ikulu, Je asingekuwa ikulu? je aliona ni sahihi wakati ule? Je, alikuwa hajui?
Wapinzani tukisema tunaambiwa kuwa ni uchochezi ila akisema Magufuri au kada wa ccm ndio sawa, ule ule ujinga wa limbwata ya rushwa na udumavu wa akili kutokana na umasikini wa fikra pevu na akili za wana ccm kushikiwa kule Lumumba.
Nauliza, hivi watanzania waliopoteza maisha Magufuri na serikali ya ccm wakiunga mkono ccm kukandiza ukweli wa vyama vya Ukawa kuhusu ubadhilifu na utapanyaji wa mali za umma, hii leo alipokuwa Rais kwa nguvu ya NEC na ccm ya leo maisha ya wananchi hao waliokufa sio bora ila ya hawa wa leo? wanaotaka wamuone nabii Magufuri, mzazi mwenye huruma?? Eti na ccm yake ni mpya....kwa walio na mtazamo huo wanapotoka na wanakosea sana sawa na mtoto aangaliaye kivuli ktk dimbwi lefu la maji na kuruka dimbwini kucheza na kivuli chake na kuishia kufa maji.
Hivi, ukienda kwa jirani kuazima gari upereke haraka mgonjwa hospitalini akakunyima kisha akawa mwepesi kuwapa majirani gari kufuata maiti ya mgonjwa wako huyo sio mchawi? Kama nakosea nikosoe maana huo ni mtazamo wangu.
Hivi Magufuli na ccm waliosababisha majanga ya kunyimwa fedha za maendeleo kutoka ktk asasi za Kimataifa kwa taifa letu na kisha kupiga kabali wananchi masikini wasio na kipato watoe michango, je ni kunar uovu kuliko huo? Hapa ndipo mjue ccm ni ile ile.
Sasa nauliza, kwanini mambo makubwa yenye tija kwa wananchi kuondoa matumizi ya hovyo hayashughulikiwi??
Mambo makubwa ya kinyonyaji .......yaani yenye matumizi hewa ila gharama kwa wananchi masikini ila Magufuli hataki kuyazungumzia hata kidogo.
1. Wakuu wa Wilaya ni useless....hawana kazi bali kutoa matamko tu.
2. Mikoa, wilaya, majimbo (constituencies) na kata nyingi pasipo ulazima ni mzigo kwa wananchi kulipa watumishi wengi wasiotakiwa kama busara ya kubana matumizi ingetumika.
3. Mwenge unaofanya majukumu ya ccm kwa gharama kubwa sana kwa wananchi.
4. Mikataba ya kinyonyaji. Hii ni mingi sana. Ila haigusii wala hauna dalili hiyo na hapa ndipo Watz tunapoteza sana.
5. Katiba mbovu ni jipu Na.1 kwa Watanzania haigusii hata kidogo.
6. Ufisadi uliofanyika enzi za awamu ya pili, tatu na nne uliofanywa na vigogo wa CCM hagusii.
Haya yote ndiyo yanatanabaisha kuwa ccm ni ile ile na ndilo jipu lililooza, huwezi kupata msafi ndani ya ccm maana wote wanaunga mkono uovu, rushwa, ukandamizaji wa haki, kupotosha ukweli na kufitini masirahi ya wanyonge kwa faida ya mafisadi walio ktk chama chao kwa kauli ya chama kwanza mtu baadae.
Nauliza,
1..hivi wezi wa makumi ya melfu ya makontena bandarini wako wapi?
2...hivi wale waliohukumiwa miaka kadhaa kutumikia jela na baada ya miezi kutolewa na kupewa kifungo cha nje kufanya usafi wako wapi? Wanafanya usafi hadi leo ?
3. Hivi bei ya sukari imeshuka?
4. Hivi mfumuko wa bei ukoje? Unajisikiaje ukienda dukani na 50,000/-
5.. Unajua ukienda na milioni 100 Tshs kubadili kwa Pound za Uingereza unapata Pound takribani 30 elfu tu? Yaani unaenda kwa kubeba na trolley ila unapewa vijinoti vichache vinapwaya kwenye mfuko wa shati.
6. Hivi wazee, watoto na mama wajawazito wanapimwa, wanatibiwa bure na kupata madawa bure huko mahospitalini?
7...hivi kuna dalili zozote za tatizo la ajira kushughulikiwa?
8. Elimu sasa ni bure na bora?
9. Nauli imeshuka hata bei ya mafuta iliposhuka?? Unajua inakughalimu kiasi gani?
10.. Boda boda, mamantilie na wajasiliamali wengine wadogo wamepewa unafuu katika shughuli zao?
11. Hivi hapo mtaani kwako mara ya mwisho kuona sarafu ya shilingi moja, tano, kumi na 20 ni lini? Unajisikiaje? Unajua hiyo inatafsiri gani ktk maisha yako ya kila siku?
12. Je lini umeona shilingi 50, 100, na 200?? Hizi nazo zimeanza kuyoyoma....nazo zitaondoka na Magufuri.
Kwasababu Mkapa aliondoka na shilingi 1 na 5..Kikwete akaondoka na shilingi 10, 20....sasa tutaona awamu hii kama shilingi 50,100 na 200 hazitakuwa historia.
Siwezi kutaja yote ila nataka kukuuliza wewe unayeimba kombolela za hapa kazi tu za ccm haya yanatokea Congo au Tanzania? Jibu unalo.
Sasa unapoishia kucheka na kushangilia watumishi hewa, mara mishahara mikubwa unajiuliza hawa ccm wamekuwepo serikalini toka mwaka jana? Au mwaka juzi?
Je, wewe kipindi chote hicho hukuitetea ccm kuwa ni chama bora TZ? Hii leo unasemaje sasa? Kuwa ni chama bora kilicholea hayo wanayoyasema kutafuta sifa kana kwamba ni wageni ccm. Wewe sio jipu unapowashangilia?
Halafu nikuulize, hivi mchawi akiloga mwanao baadae akakwambia dawa anayo kisha akampa dawa mtoto au ndugu yako ila hakupona akaishia kuwa mlemavu na zezeta ila hafi kabisa.
Je, utafurahi kuwa huyo mchawi amekutendea wema5 kuwa mgonjwa wako hajafa?
Hivi huyo zezeta au mlemavu aliyelogwa ametendewa haki?
Unajisikiaje umuonapo nduguyo au mwanao aliyelogwa na mchawi mjuaye? Huyo mchawi unampenda? Unamsifu na kumshangilia kuwa kakupa dawa mgonjwa wako hakufa?
Hapa nchini mchawi wa maendeleo ni CCM. Na aliyelogwa ni mwananchi na wahanga waliologewa maendeleo ni sisi makabwela tunaotazama uchumi wa nchi na kuusikia eti unakua na kukusanya matrilioni ya shilingi ila mifukoni mwetu hakuna kitu hata mulo kuupata ni tabu. huko mahospitalini na mashuleni ni majanga matupu.
Kuweka akili mfukoni na kushangilia ccm eti inashugulikia watumishi hewa? mishagara mikubwa? unashangaza sana.
Hujiulizi MRI na CT scan ziko wapi? Maharamia wa makontena wako wapi?
Mahakama ya mafisadi iko wap?
Kwanini wanagusia mambo mepesi ila mfumo unaosababisha hayo maovu kurekebishwi?
Naona ni jitihada za kuweka watu katika kizimba cha fikra, na kuwahamisha kutoka ktk kutafakari mambo muhimu ya Zanzibar na Tz kuwekewa vikwazo kupewa fedha za maendeleo tudanganywe na mambo madogo kisha tukicheka tulipie vicheko kwa viboko vya michango na kodi kubwa wao wakijineemesha ktk ofisi za serikali, hapo ndipo mjue ujinga ni mzigo na tija kwa mwelevu jambazi.
Magufuli=CCM na ccm ni ile ile!