Mpaka sasa Bunge litaendelea kuzuiwa kujadili mauaji haya?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Kwa hatu hii tuliofikia nitashangaa sana kama kuna mbunge atatoa hoja ya kujadili mauji haya na kiti kikakataa na nitashangaa zaidi iwapo wabunge wataridhika hoja ya aina hiyo kukataliwa.

Haiwezekani watu wasishituke kwa hali hii ya mauji haya ya mfululizo na itabidi tuanze kujiuliza kulikoni.
 
Tatizo ni kuwa ingawa Bunge ni mhimili huru according to Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini kwa bahati mbaya sana Bunge letu limeamua 'kujibinafsisha' kwa ule mhimili mwingine ambao huwa unatamba kuwa eti wenyewe umejichimbia zaidi chini!

Kutokana na hali hiyo kila kinachojadiliwa Bungeni, lazima kipate blessings kwa kupitia 'remote control' iliyopo pale Magogoni!
 
Kwa hatu hii tuliofikia nitashangaa sana kama kuna mbunge atatoa hoja ya kujadili mauji haya na kiti kikakataa na nitashangaa zaidi iwapo wabunge wataridhika hoja ya aina hiyo kukataliwa.

Haiwezekani watu wasishituke kwa hali hii ya mauji haya ya mfululizo na itabidi tuanze kujiuliza kulikoni.
Pia na sisi raia tujiulize sana maswali " ni nani wa kulaumiwa katika msala huu?"
Jambo lolote lenye kutatiza ambalo majibu yake huwa yamejificha, ni lazima kujiuliza maswali hayo ili kupata mustakabali wa jambo na namna ya kupata mhusika wa kumuwajibisha kwa jambo kama hilo lililofichika, maana limechukua muda mrefu sasa.
Na kamwe, haiwezekani hapa duniani jambo kama si la kichawi, likawa ni la wazi, maana yake limefanywa na biadamu "physicaly", likaachwa likapita hivihivi.
 
Hali imeshakuwa tete Mwigulu amepwaya katika ile wizara. Inabidi ajiuzuru au aondoke.
Mwigulu hausiki na Yale mauaji,Hata waziri wa mambo ya ndani angekuwa Rais au Mkuu wa Majeshi bado mauaji yangetokea tu kama issue ilishapangwa maana ni mauaji ya kuvizia na invincible killers or snipers.

Narudia wito wangu tena intelligencia itafute root cause ya haya mauaji ndiyo dawa pekee ya kudhibiti mauaji hayo ya kishenzi!!
 
Mbona hii Nchi tuna Vijana shupavu sana, kuna yule aliyemtolea Nape bastola na yule aliyemtolea Malima ile Mashine kubwa......Nina uhakika hawa wanataka kuwa stationed huko kibiti........hali ni tete wakuu.
 
Kinacho nishangaza ni kwamba, wanao uwawa ni wana-ccm alafu wana-ccm walioko bunguni hawataki jambo hili lijadiliwe na bunge zima! Something is wrong some where!!

Ni kama aina fulani ya ugaidi.
 
hawa jamaa wanatafuta jina "MAGAIDI" ili iwe rahisi kwa vijana kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya nchi kujiunga nao.
tusitegemee mauaji haya kukoma yataendelea tu hadi pale serikali itakapokubali kuwa ni magaidi,na tukumbuke ukishakubali kuwa ni magaidi basi utalii,wawekezaji watakimbia nchi na uchumi kuzidi kushuka
 
Mbona hii Nchi tuna Vijana shupavu sana, kuna yule aliyemtolea Nape bastola na yule aliyemtolea Malima ile Mashine kubwa......Nina uhakika hawa wanataka kuwa stationed huko kibiti........hali ni tete wakuu.
Hawana msaada kwa sasa
issue ya kusini inahitaji approach tofauti na hiyo inayo tumiwa na Polisi
 
Kama lilishindwa kujadili walivyoniteka, samahani nimekosea tulivyotekwa mm na akina Roma, Moni na Osama hivi naye alitekwa?
 
Kwa hatu hii tuliofikia nitashangaa sana kama kuna mbunge atatoa hoja ya kujadili mauji haya na kiti kikakataa na nitashangaa zaidi iwapo wabunge wataridhika hoja ya aina hiyo kukataliwa.

Haiwezekani watu wasishituke kwa hali hii ya mauji haya ya mfululizo na itabidi tuanze kujiuliza kulikoni.
Kwakweli, hili ni janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom