Mpaka mbolea ya bandia !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka mbolea ya bandia !!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kwame Nkrumah, Feb 18, 2012.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mbolea bandia yaharibu mazao Mbozi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 17 February 2012 21:03 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Brandy Nelson,Mbozi
  UONGOZI wa Serikali wilayani Mbozi, umesema mbolea bandia iliyosambazwa wa wakulima katika wilaya hiyo, imesababisha uharibifu mkubwa wa mazao mashambani na hivyo hasara kwa wakulima.

  Hata hivyo Mkuu wa hiyo, Gabriel Kimolo alisema polisi na vyombo vingine vya dola, vinafanya uchunguzi wa kujua mtandao wa watu waliohusika katika kusambaza mbolea hiyo, ili sheria ichukue mkondo.

  Kimolo ambaye alikuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini wake, alisema mbolea hiyo imesababisha athari kubwa katika ustawishaji wa mazao mashambani.
  Tunakilaani sana kitendo hiki maana kimerudisha nyuma maendeleo ya wananchi wanaotegemea shughuli za kilimo katika maisha yao, tutawachukuliwa hatua wote watakaokamatwa kwa kujihusisha na uuzaji wa mbolea hii,” alisisitiza Mkuu wa wilaya.

  Aliwataka wakulima kuwa makini wanaponunua mbolea, ili kuepuka uwezekano wa kutumbukia tena katika blaa kama hilo.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Ambakisye Minga, alisema yeye pia ni miongoni mwa wakulima waliouziwa mbolea hiyo bandia na kwamba amepata hasara kubwa.

  Kwa mujibu wa Minga, yeye aliuziwa mifuko 18 na alipoitumia, haikusaidia kukuza mazao na badala yake, imeyaharibu.“Mbolea hii imetuletea hasara kubwa na hatujui tufanye nini,” alisema.Habari zilisema wakulima katika wilaya hiyo wameuziwa zaidi ya tani 45 za mbolea bandia ya urea .
  Maofisa wa Tume ya Ushindani, Kampuni ya Yara Tanzania Limited, Nexlaw Advocates na Polisi ndiyo walioibaini mbolea hiyo ikiuzwa katika maduka ya pembejeo katika Vijiji vya Mlowo na Ihanda, baada ya kufanya msako.


  Source hii hapa: Mbolea bandia yaharibu mazao Mbozi

  MY TAKE: Kilimo kwanza kitawezakana vipi hapa? Malalamiko yote KIkwete hasikiii? Mtoto wa Mkulima upo? Kama kweli Pinda ni mtoto wa mkulima hapa ndiyo unatakiwa kuonyesha makali yako.

  Grrrrhh aaargh.... Bora Lowassa arudi.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  lowasa?
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  yaan nchi ya kudump uozo..
  fcc,tra,tbs,chief govt chemist,tfda wote wanachumua tumbo hawafikirii madhara yake yanawadhuru na wao
   
Loading...