Mpaka lini CCM itaendelea kujisukasuka katika bahati hii ya mtende?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,047
Posted Date::6/9/2008
Mpaka lini CCM itaendelea kujisukasuka katika bahati hii ya mtende?
Na Ally Saleh
Mwananchi

DALILI kuwa Chama Cha Mapinduzi kimechoka kuwepo madarakani ni nyingi. Na zile za kuwa muda wa kuondoshwa madarakani umefika ni nyingi zaidi, na hilo liko wazi kabisa kuonekana na kila jicho linalotaka kuona.

Kuchoka kwenyewe si lazima waseme ''Jamani eeh si tumechoka!'' Lakini ni kwa kauli na matendo yao ambayo huko nyuma hatukuwa tukiyaona lakini sasa yaliyofichwa vifuani yanadhihirishwa uwanjani.

Makosa makubwa na ambayo kisiasa hayawezi kusameheka yamekuwa yakitokezea katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na baadhi yake yametikisa nchi hii kama tetemeko la ardhi la kipimo kikubwa cha Richter cha kupimia matetemeko.

Ingewaje mtiririko wa makosa hayo kwao watawala hawataki yahusishwe na siasa. Kwa maana kushika madaraka ni siasa lakini kufanya makosa katika madaraka si siasa ni utawala.

Hayo ni kwa upande wa Tanzania Bara, lakini sio kama hakuna matukio ambayo ni ya kiwango kinachofanana na hicho kwa upande wa Zanzibar maana nako pia CCM inaonekana kuchoka kubaki madarakani, lakini bado inaendelea kuwepo, sijui niseme kwa kudra ya Mungu au vipi.

Maswala kama ya kushindwa kwa Mwafaka, kukamatwa wananchi kwa kudai haki za kiuchumi na kushirikishwa katika utawala, ni mambo yanayoikwaza Zanzibar kwa sasa.

Kama una Serikali ambayo inaweza kubaki na 'bifu' na mwekezaji bila ya kujali faida za uwekezaji, huku Rais akijua suala la wenyewe, Waziri Kiongozi akilielewa vyema, Spika wa Baraza la Wawakilishi akilifahamu vizuri sana na bado suluhu haitafutwi, unapata hamu ya kujiuliza hivi kweli Serikali kama hiyo inataka kubaki madarakani?

Au kama Ikulu inaandikiwa kutatua tatizo lenye maslahi makubwa ya uchumi na ustawi wa nchi, kama la mwekezaji, na hata kujibu tu kuandika kuwa barua yake imefika na inafanyiwa kazi na kumtaka astahamili, ingawa kiwanda chake kimekwama kwa miaka mitatu na nusu, unapata shida kuamini kuwa una Serikali iliyo makini na ambayo inataka kuendelea kubaki madarakani.

Na itokezeapo kuna kampuni ambayo inaweza kutoa ajira zaidi ya 1,000 kwa wananchi, ambapo ajira hizo zitaunga mkono familia 1,000 lakini zaidi ya wananchi 5,000 kwa wastani, na serikali haifanyi juhudi za kuhakikisha kwamba ajira hizo zinapatikana, unajiuliza ni kweli Serikali iliyopo madarakani inataka kweli kubaki madarakani?

Naamini sana kuwa kama haya yote yangekuwa yakitokezea sehemu nyingine duniani kwa kweli isingekuwa ni mawaziri tu waliojiuzulu, lakini pengine hata Serikali yenyewe ingetakiwa kuwajibika na sehemu nyingine hata Rais asingekuwapo tena madarakani, maana hata yeye angekuwa ni mzigo kwa chama chake.

Maana chama hakimuweki mtu kwenye nafasi ya urais kwa kuwa leo yupo yeye, lakini Chama kinamuweka mgombea ili kesho na keshokutwa ashinde tena au akijengee chama mazingira yakushinda tena na iwapo atashindwa kuuzika au nafasi ya chama kubaki madarakani inafinyika, basi Rais nae hutolewa muhanga.

Kwa hali ilivyo hivi sasa Chama Cha Mapinduzi kama ingekuwa katika nchi nyingine, kingekuwa kimo katika tafakuri kubwa na yenye kina kulilia uhai wake madarakani na mgombea wake kubaki katika nafasi ya Urais, maana makosa ambayo yangekipeleka chama hicho kwenye kaburi la kisiasa yamekuwa mengi mno.

Lakini CCM inaishi katika mazingira ya bahati kubwa sana kisiasa au tuseme katika jamii ambayo imepumbazwa sana kisiasa kiasi ambacho inaogopa kuhoji na pia inaogopa kudai. Hiyo ni sadfa kubwa sana kwa siasa za Tanzania ambayo inazuia CCM isiondoshwe madarakani.

Maana haiingii akilini kupandishwa kote kwa bei, kuibiwa kote kwa rasilimali za nchi, kubaguliwa kote kwa wananchi, kutengwa kushirikishwa kwa wananchi, kuzuia fursa za kuweka mazingira bora ya siasa na bado wananchi wa nchi hii wakakaa kimya kabisa kama hakuna linalotokea.

Kwamba yote yanayotokea nchi hii na bado watu hawaamini kuwa yanahusiana na siasa kwamba ni kwa ajili ya udhaifu katika kusimamia siasa kwa upande wa chama kinachotawala, ni bahati kubwa kwa CCM.

Kwamba bado nchi nzima ina lepe la usingizi kuwa nchi hii ingepaswa kuwa imara zaidi kiuchumi na tulipo sasa chini kabisa katika orodha ya nchi masikini, ni sababu ya siasa na kushindwa kwa CCM na wananchi hawaamini hivyo, ni bahati kwa CCM.

CCM ina bahati ya mtende kuwa rushwa inayoila nchi hii imetokana na kukosekana sera imara za kusimamia hilo na pia ugawanaji wa rasilimali za nchi, na bado watu wasiamini kuwa kukosa mwelekeo wa hayo ni kutokana na CCM yenyewe kukosa mwelekeo na udhibiti, kunanishangaza mno.

Kwamba unapoishauri kampuni ambayo ilikuwa na mipango ya kutoa ajira 1,000 lakini zimekwama kuwa njia mbadala ni kulisukuma ombi lao kupitia upinzani, lakini kampuni hiyo ikafanya woga kuwa suala hilo litakuwa la kisiasa na kampuni ina hiari kuliwacha kama lilivyo. CCM inakuwa na bahati sana.

Au Serikali kukosa dola 3,000,000 kwa miaka mitatu, ajira 450 kupeperuka, mapendekezo ya Kamati ya Baraza kupuuzwa na kuwepo kwa uwezekano wa Serikali kushtakiwa na kuja kulipa mamilioni ya dola, na bado Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakanyamaza kimya na umma usiwe na njia ya kuhoji, ni uhaini mkubwa kwa nchi.

Unapoona mambo yamefikia hapo unajiuliza iwapo sisi Watanzania na Wazanzibari tunaishi katika karne gani ambayo kama wananchi hatuwezi kufanya maamuzi juu ya khatma yetu kwa mazoea tu ya kuwa CCM ndio chama bora zaidi. Hatuwezi kujiuliza basi haifiki pahala tukaweka vigezo kujiuliza ubora ni upi? Hivi tunaitendean haki nchi hii kwa kuendelea na mazoea? Au mpaka lini CCM itaendelea kujisukasuka katika bahati hii ya mtende?

Na ndio maana CCM imeanza kuingia woga kuwa wakati umefika sasa kwa nchi hii kuwa na wagombea binafsi. Maana inawezekana wagombea wa vyama vyengine wasikubalike na wananchi kwa sababu hizo hizo nilizozisema.

Lakini kwa fikra zangu vyovyote iwavyo CCM isikae ikaamini kuwa mambo yatakuwa hivi hivi kila siku. Umma haujafa, ila umelala tu na kidogo kidogo unaamka. Wananchi wanaoweza kujiuliza masuali magumu kila siku wanaongezeka na tabaan ambao wanaweza kufanya maamuzi magumu wanaongezeka.

Pengine haiko mbali siku ambayo wananchi watafanya uamuzi si kwa sababu wameizoea CCM na kuukataa ule msemo wa Kiswahili kuwa '' Zimwi likujualo halikuli likakwisha,'' kwa sababu zimwi hili la CCM lishaimaliza nchi hii, na kwa kiasi kikubwa hakipo tena cha kukila, na hilo ndio litaamsha wananchi.

Simu: +255 777 4300 22

Tovuti: www.eternaltourszanzibar.net

Blog: jumbamaro.blogspot.com
 
Nadhani wa kuulizwa swali sio CCM bali ni wapinzani. Je kwanini wanashindwa ku-make their case to wananchi pamoja na kuwa na loopholes zote za kufanya hivyo?
 
aliyeandika hii makala anaweza kuwa na point, lakini sidhani kama alifikiria zaidi !
 
Kuna yeyote Tanzania anayefikiria zaidi kuliko makada wa CCM!? Tangu lini? Siku zote makada wa CCM ndiyo wamekuwa wanafikiria kuliko mtu mwingine yeyote yule Tanzania, na huko kufikiria kwao ndiyo chanzo cha nchi kwenda mrama, lakini wao hawalioni hili bado wako busy wanafikiria tu!!!!
 
Nadhani wa kuulizwa swali sio CCM bali ni wapinzani. Je kwanini wanashindwa ku-make their case to wananchi pamoja na kuwa na loopholes zote za kufanya hivyo?

..wapinzani inabidi waanze target zao polepole sio lazima kugombea nchi nzima,wangeanza na kuchukua Dar maana ndio best bet yao ilipo walikuwa na nafsi nzuri sana 95 wakati wa kina Mrema ila usanii wa CCM ndio umeua upinzani lakini sio excuse...they need to fight back!
 
Kwa jinsi nchi inavyoendeshwa sasa hivi sidhani kama kuna haja ya kusubiri, maana mafisadi wanaweza kukomba kila kitu mwaka mmoja tu wa 2005/2006 wamekomba $288 milioni ambzo ni sawa na shilingi bilioni 288. Wakiendelea kuwepo madarakani, Wapinzani kama wakiingia watakuta kweupeee na Watanzania tutaanza tena kuwahoji mlikuwa wapi miaka yote mpaka mafisadi wakakomba kila kitu? Je, hakumsikia maombi yetu kwenu ya kuunganisha nguvu na kuunda chama kimoja chenye nguvu!?
 
Back
Top Bottom