Mpaka leo sijawahi kusikia uthibitisho wowote kuwa Serikali ndiyo inateka watu

Kwanini unatoa shutuma kwa Serikali kuwa ni watumishi wake wakati huna uthibitisho wowote kuwa ni watumishi wa Serikali
Utoto unakusumbua unajua kazi ya Jeshi la polisi?
Anaye takiwa kutoa taarifa za watu kutekwa ni mwenye mamlaka ya kuwahoji kama Polis hawataki kuwahoji watekaji ni dhahiri wanajua kinachoendelea.
 
Utoto unakusumbua unajua kazi ya Jeshi la polisi?
Anaye takiwa kutoa taarifa za watu kutekwa ni mwenye mamlaka ya kuwahoji kama Polis hawataki kuwahoji watekaji ni dhahiri wanajua kinachoendelea.
Zote hizo ni dhana tu ambazo ndo wengi wanakuwa wanasema sema tu
 
Mshauri member wa familia yako yeyote amkosoe Bwana mkubwa kwenye media halafu kaa wiki utapata majibu
 
endelea kusubiri uthibitisho huo na usisahau pia kwenda pale JNIA kusubiria meli iliyobeba noah yako
 
Mpaka sasa sijaona uthibitisho wowote kuwa wote waliotekwa na kuachiwa au wale waliopotea moja kwa moja au hata waliokutwa wameuwawa kuwa mambo hayo yanafanywa na vitengo fulani fulani vya Serikali.

Hata walioachiwa baada ya kutekwa sijawahi kuwasikia wakisema kuwa waliowateka na watumishi wa Serikali kweli sijawahi kuwasikia.

Serikali imekuwa ikikemea vitendo hivyo nakumbuka hata wakati wa Dr Ulimboka alipookolewa akiwa mahututi katika msitu wa Mabwepande Rais wa awamu ya nne Dr Kikwete alisema waziwazi kuwa Serikali haijamtuma mtu yoyote kumteka na kumtesa Dr Ulimboka na kama kuna mtu amefanya hilo basi ni kwa utashi wake na Serikali haijamtuma yoyote kufanya hayo na kamwe haitatuma mtu kufanya hayo.

Sasa maswali ya kujiuliza tu ni kwanini wote waliowahi kutekwa kwanini wakiachiwa hawataki kusema ukweli nani amemteka na huko walikuwa wanaulizwa nini hiyo ingekuwa sababu ya kujua nini kinachoendelewa na kujua hata chanzo cha hayo matukio.

Kwa wao kukaa kimya haitasaidia kujua nani anawateka na haitajulikana kamwe na kwa kauli ya Dr Kikwete awamu ya nne ni kuwa Serikali haitumi mtu yoyote kumteka mtu na kumtesa kwasababu yoyote ile.

Ni muhimu kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa vyombo husika kuhusu ushahidi wowote ule ili hawa watu wajulikane otherwise hawa watu hawatajulikana kamwe milele na milele na mtabaki kulalamika tu.

Mpaka siku utakayopata fahamu kuwa serikali huwa ni nini ama ni nani ndio utajapata picha halisi ya kinachoongelewa kwa yanayoendelea kutokea.
 
Mpaka siku utakayopata fahamu kuwa serikali huwa ni nini ama ni nani ndio utajapata picha halisi ya kinachoongelewa kwa yanayoendelea kutokea.
Serikali haihusiki na hayo mambo yenu unless una ushahidi.
 
Heri maskini mwenye furaha na amani kuliko tajiri asie na furaha na amani.Tumwambie ukweli umoja wa Taifa letu ndio nguzo yetu,na tutaweza mengi kwa kasi zaidi pamoja. Bado nashuhudia ushamba uchama ktk mikutano rasmi ya serikali! Ni dhambi kutumia njaa za watu ,eti sharti avae kijani ndio apate riziki ,huu ni ukoloni mwingine wa kishamba zaidi karne hii.Watu wanavaa nje ila mioni mwao wanajua wanachokiamini.Tanzania ni kubwa zaidi ya yeyote
 
Back
Top Bottom