“Mpaka kifo kitutenge” wanawake sasa wakataa kiapo hicho……….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

“Mpaka kifo kitutenge” wanawake sasa wakataa kiapo hicho……….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 8, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hivi sasa wanandoa wa Marekani hawako tayari tena kujiapiza kwamba, wataishi na mume hadi kifo kije kiwatengenishe. Badala yake, wengi hutaka kujiapiza kwa kusema, “tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, kama tu penzi litaendelea kuwepo.” Kwa sababu maandiko ya dini ya Kikristo kwa mfano, hayawezi kubadilishwa katika jambo kama hilo, wanandoa wengi wameamua kutofunga ndoa zao kanisani na badala yake hufungia mahali pengine. Hii ni ili kukwepa kutamka kwamba, wataishi hadi kifo kiwatenge, wakati wanaona kabisa watu wengi wamechanganyikiwa na hawajui tena maana ya kupenda.Kila bibi harusi anaogopa kujiapiza kwa kauli hizo zenye kumfunga. Inaelezwa kwamba, woga huo unatokana na kile kinachoonekana majumbani, kwamba, ndoa nyingi hazina kuaminiana na zinatisha kwa visa na mikasa. Inaelezwa na watu wanaopenda kuyachukulia mambo kimkabala na mila na desturi kwamba, utaratibu huu mpya wa kukwepa kusema, “hadi kifo kitutenge,” wakati wakufunga ndoa na badala yake kusema kitu kama, “naahidi kuwa mwaminifu kwako, kama tu penzi bado lipo,” huenda utadhoofisha ndoa nyingi.

  Raisi wa Muungano wa Makanisa Katoliki na haki za binadamu, William Donahue, amesema, kubadili kiapo hicho na kusema, “kama tu penzi litaendelea kuwepo,” ni sawa na kuweka masharti kupenda, jambo ambalo litafanya kupenda kupoteze maana yake ya asili. Amesema kupenda hakuwezi kuwekewa masharti. Kiongozi wa utafiti huu Mary Jo Gallegos amesema, kwa hivi sasa ambapo watu wa mila na imani mbalimbali wanakutana na kuoana, mambo ya kuambiana hadi kifo kitutenge, hayawezi kuwa na nguvu. Mama huyo ameendelea kusema, hakumbuki kwa mara ya mwisho ni lini alimsikia mwanamke mwenye kufunga ndoa, akiahidi kwamba, atampenda mumewe hadi kifo kije kiwatenge. Anazidi kusema, hakuna jambo kama hilo kwa sababu, wengi wamegundua kwamba, huko ni kujitwisha mzigo ambao mtu hawezi kuubeba.

  Amezidi kusema kwamba, watu wengi sasa wanaiona hali halisi na wanajua ukweli mkubwa zaidi katika ndoa. Amesema wale walio kwenye ndoa ya pili au ya tatu, wanajua ukweli mkubwa zaidi kuliko wale walio kwenye ndoa ya kwanza au ambao hawajaingia kwenye ndoa kabisa. Jambo la maana anasema, ni kwa wanandoa wote kuamini kwamba, wataishi kwa amani hadi kufa, lakini wakijua lolote linaweza kutokea. Huko Marekani, nusu ya ndoa huishia kwenye talaka. Hata hivyo kiwango hicho kimeshuka, baada ya wengi kuamua kuwekana kinyumba au kuwa vimada badala ya kufunga ndoa. Hivi sasa wapenzi huishi pamoja kwa miaka mitatu au zaidi kabla hawajaamua kama wafunge ndoa au hapana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake, haamini kwamba, anampenda.

  Sharon Naylor, ambaye ni mtunzi wa kitabu cha Your Special Wedding Vows (Kiapo Maalum kwa Ndoa Yako) anasema amewahi kusikia bibi harusi akiapa siku ya ndoa yake kwa kusema, “hadi pale muda wetu wa kuwa pamoja utakapoisha.” Anasema kiapo kama hiki ni sahihi kwani kuapa kwa kitu ambacho huna uhakika wa kukiweza au ambacho unajua siyo kweli, ni kujitendea haki. Mabadiliko haya katika kuapa siku ya ndoa yanaashiria kwamba, taasisi inayoitwa ndoa inaendelea kupambana na mabadiliko ambayo hatimaye yataiporomosha na watu wataanza kuishi kama wanyama wengine. Inaelezwa pia kwamba, huenda ni kutokana na ubabe wa wanaume ambao umewabadili wanawake na sasa wameanza kuitazama ndoa kama kifungo……….


  Thread hii ni dedication kwa MadameX ambaye anatafuta mume wa kumuoa baada ya kuchoshwa na masharobaro
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  anyway, wameamua kuwa wakweli kwa wanachoamini, ila bado naamini katika 'hadi kifo kitutenganishe'
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kongosho bila shaka wewe utakuwa ni miongoni mwa wale waliozaliwa miaka ya 1960........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nina mixed feelings hapa! Ni dream yangu iwe mpaka kifo kitutenganishe, lkn najua kuna baadhi ya vitu sitaweza kuvivumilia. Hivyo nami ningeapa "mpaka pale tutakaposhindwa kuishi pamoja"
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza Kaunga leo kawa mhafidhina kama mimi............Siamini kama umeniunga mkono....................LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280
  Naona hapa kwetu waanze kusema hadi ''umasikini ubishe hodi''
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Rweye hilo nalo neno.............
  Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba, kwetu sisi ulitima ukibisha hodi basi na mapenzi nayo yamekwisha.........!?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  i also still believe in 'For As Long As We Both Shall Live'. if I'm marrying my bf then I'm committing my life to him bcoz I love him and i dont want to be without him.
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Na wanaume?
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huu ukilaza huu, hata sijaelewa........... Hebu tufasirie sisi tusiojua hiyo lugha, maana naamini unakijua kiswahili vizuri na ndio maana umelewa mada hii na ndio maana umechangia......................
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  "tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, lakini ukileta jeuri na kibri nakutafutia nyumba ndogo ujinga ukutoke."
   
 12. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Naungana nao. Lazima tubadilike ili tusitende dhambi kwa vifungo vya Kanisa. Love is uncertain, lol.
   
 13. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kwa wanawake wa kibongo waape "tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, kama tu hutakuwa na nyumba ndogo."
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kwa muda nilisahau objective yangu kwenye nyuzi zako! U got me this time! LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ha ha ha, na kweli mie wa enzi za zamadamu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  vipi Kongosho umeolewa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  nimeoa . . . . .

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  acha kumzeesha mwenzio,1998 kongosho alikuwa darasa moja la kwanza na lulu mtendeni praimari.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  blaine,wewe ni She? mmmhhhh hizi avatar hizi!
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  ushawahi kupiga msuba?
   
Loading...