MP Dr Hamis Kigwangallah, UPDATES PLEASE!

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
31
Leo Jumamosi tarehe 16/06/2012 ndiyo siku Mh. Kigwangallah (MB) anafanya maandamano na mkutano ndani ya Jimbo lake la Nzega, na kwa maelezo yake akiungwa mkono na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono katika hoja yake ya msingi iliyomsukuma kufanya maandamano na mkutano.

Hata hivyo nimeona kimya kingi, tangu asubuhi nimekuwamo humu jamvini bila updates zozote juu ya shughuli hii.
Kwa yeyeote yule aliyepo eneo la tukio, Isungangwanda, Nzega Ndogo au maeneo hayo, tuhabarisheni ili tuweze kupima matokeo ya tukio ili.

Itakuwa vyema kama tunaweza kupata na picha za mkusanyiko huo. Maandamano ni watu na Mkutano pia ni watu

UPDATES:
  • Mh. Kigwangallah amefanikiwa kufanya mkutano kama dhamira yake ilivyomsukuma
  • Hakukuwa na mshirika hata mmoja kati ya wale aliojinasibu kuwa wangemuunga mkono (wabunge)
  • Askari walikuwa wengi, maudhurio ya raia/wapiga kura ni hafifu lakini alipata wasikilizaji
  • Kama kawa fuso zilisomba watu
  • waandishi wa habari walikuwa, tutarajia mengi toka kwao
  • Naambiwa kanguruma vilivyo, najua ni member hapa jamvini na atakuja kutujuvya.
 
mimi niko Natal, nikienda town badae nitakuambia nini kimeendelea.
 
Hute, jitahidi tafadhali, mimi nimeharibikiwa katikati ya Mambali na Bukene nilikuwa nawahi kufanya coverage ya hii event
 
anatafuta umaarufu huyu hana lolote . kwa nini asianadam,ane kimya kimya
 
Alisema wananchi kwanza chama baadaye, akitenda kinyume na hapo tutamuona naye ni VuVuZela kama Nape
 
Leo Jumamosi tarehe 16/06/2012 ndiyo siku Mh. Kigwangallah (MB) anafanya maandamano na mkutano ndani ya Jimbo lake la Nzega, na kwa maelezo yake akiungwa mkono na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono katika hoja yake ya msingi iliyomsukuma kufanya maandamano na mkutano.

Hata hivyo nimeona kimya kingi, tangu asubuhi nimekuwamo humu jamvini bila updates zozote juu ya shughuli hii.
Kwa yeyeote yule aliyepo eneo la tukio, Isungangwanda, Nzega Ndogo au maeneo hayo, tuhabarisheni ili tuweze kupima matokeo ya tukio ili.

Itakuwa vyema kama tunaweza kupata na picha za mkusanyiko huo. Maandamano ni watu na Mkutano pia ni watu

BELOW PLEASE FIND THE UPDATE

556895_10151017990745479_291915688_n.jpg
 
Hatimaye napata taarifa kuwa muda mchache ulipita Mh. Kigwangallah ameonekana maeneo ya NATA (Kijiji) akiamasisha watu kuanza maandamano
 
Hatimaye napata taarifa kuwa muda mchache ulipita Mh. Kigwangallah ameonekana maeneo ya NATA (Kijiji) akiamasisha watu kuanza maandamano

intelejensia ya polisi inasemaje kuhusu hayo maandamano
 
Back
Top Bottom