Moyo wangu haupendi tena mwanaume nifanyeje?

Wadau naomba mnishauri,nifanye nini?baada ya kuwa kwenye uhusiano na mpenzi
kwa miaka mitano na baadae kuamua kumwacha kwa jili ya ulevi wake wa kupitiliza
nahisi au najikuta simwamini na wala simpendi mtu yoyote tena,ikumbukwe kuwa
nina umri wa miaka 30,na pia sio kwamba siku zote sikujua kama choice yangu ni
mbaya bali niliamini angebadirika na kuwa mpenzi bora,lakini kadri siku zilivyokuwa
zinakwenda ndivyo na ulevi alivyokuwa anazidisha kurudi kwake peku,kuumia kwa ulevi.
Mbali na ulevi,hakuwa mtu wa mapenzi nikimaanisha kunijali,mfano,yeye alikuwa anafanyia
kazi mkoa mwingine mimi mwingine,mwaka unaweza katika asije kwangu kunitembelea
na akija ujue kaja Dar kwa shida za kiofisi,pia vitu kama zawadi ni ndoto toka kwake kinyume
na mimi,sasa kwa kawaida unaweza ukasema jamaa hakuwaanakupenda lakini si kweli
mbali na mapungufu hayo nilijihakikishia ananipenda kwa mambo fulani niliyokuwa napele
leza kama je ana mpenzi mwingine,au ananiongeleaje kwa watu?au je mahusiano yake
kwa mpenzi wa zamani yalikuwaje,nikagundua kwamba jamaa Tatizo ni Ulevi tu wa kutia umaikini
Sasa ni mwaka niliamua kumwacha,na kweli nikafanikiwa kumtoa moyoni,tatizo akitokea mpenzi
mwingine moyo haukubali,nitafanyaje?au nijilazimishe?au nina tatizo la saikologia?lpz help
2012 ulikuwa na miaka 30 ina maana kwa sasa una miaka 38?
 
Mapenzi ni hisia, na huja automatically kama vile kupepesa macho. Usijilazimishe wala kusikiliza hisia hizo, we endelea na maisha tu, kula vizuri, fanya mazoezi kila unapoweza achana kabisa na kusikiliza hizo hisia.

Utakapokutana na mtu ambaye hisia zako zinamkubali, basi utajikuta tu tayari umezama kwenye mahaba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom