Moyo wako ungefanya nn unazani?

Khaleed Shaban

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
399
58
Habari zenu wana jf? Ni hivi kuna rafikiangu ana mpenzi wake na jana tu kaja kuniomba ushauri ambao nimekosa majibu ivyo naombeni mnishauri ili nipate la kumwambia ilikua hivi yeye alikua na mpenz wake wakati anasoma chuo but baadae mpenz wake akasafiri nje ya nchi kusoma zaid,baada ya kufika uko mawasiliano na mchizi yakapungua na atimae kuisha kabisa,mchizi akapata mtoto wa kinyatulu akamdatisha na hatimae kutangaza ndoa ambayo inatakiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ila majuzi demu wake wa aliesafiri kwenda nje ya nchi kusoma amerudi na mchizi anadai bado anampenda na huyu wa sasa bado anampenda ukizingatia katangaza kumuoa akiniomba ushauri kisha akaniuliza kua kama ungekua ww moyo wako ungefanya nn unazani wakati mm bado nawaitaji wote? Nawasilisha mada kwenu wana jf
 
Nazani ningezani....
Mchini bora azani tu...
Moyo unashaurika toka lini
 
Dah!!!kazi ya MOYO ni kusukuma damu tu,mengine haya nikutiana BP bure,,,,,,,,,,, Aache MOYO wake ufanye kazi yake mapenzi aiachie wallet tu!!
 
hana lolote huyo, hapo anayependwa ni huyo aliyerudi kutoka masomoni ila anaona aibu tu kumuacha huyu ambaye ashamtangazia ndoa.
 
jamaa ni dini gani?...
ujuyo alie rudi kutoka ugaibuni bado ni wapenz.?
 
Anapendaje wawili? Kuna mmoja anadanganywa hapo. Huyo wa ndoa awe tayari kwa lolote bomu litamlipukia siku si nyingi.
 
Habari zenu wana
jf? Ni hivi kuna rafikiangu ana mpenzi wake na jana tu kaja kuniomba
ushauri ambao nimekosa majibu ivyo naombeni mnishauri ili nipate la
kumwambia ilikua hivi yeye alikua na mpenz wake wakati anasoma chuo but
baadae mpenz wake akasafiri nje ya nchi kusoma zaid,baada ya kufika uko
mawasiliano na mchizi yakapungua na atimae kuisha kabisa,mchizi akapata
mtoto wa kinyatulu akamdatisha na hatimae kutangaza ndoa ambayo
inatakiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ila majuzi demu wake wa
aliesafiri kwenda nje ya nchi kusoma amerudi na mchizi anadai bado
anampenda na huyu wa sasa bado anampenda ukizingatia katangaza kumuoa
akiniomba ushauri kisha akaniuliza kua kama ungekua ww moyo wako
ungefanya nn unazani wakati mm bado nawaitaji wote? Nawasilisha mada
kwenu wana jf

wote awaache
 
Huyo siyo wa kushauri,huyo mwanaume mie namuona mjinga tu anashindwa nini kuwa na uamuzi ulionyooka mpaka achanganye wachumba mie nampuuza kabisa.
 
hana msimamo huyo kwan alimuuliza huyo mpenzi wake wa zaman kipi kilikatisha mawasiliano??
 
Back
Top Bottom