Naomba nialike kwako nije kulaHabari ya muda huu popote pale ulipo wana jamvi.
Kama ulipo haijadondoka tarehe 25/12/2023 basi endelea kuvuta subira itafika tuu punde si punde.
Ni sikukuu leo ya kuadhimisha kukumbuka kuzaliwa kwa Kiongozi wa waumini wa dini ya Kikristo.
Heri ya Sikukuu na Maandalizi ya Mwaka Mpya 2024.
Mpendwa, kama hadi muda huu hujajua sikukuu inaendaje usipate msongo wa mawazo. Shukuru kwa uzima na afya uliyonayo, siku itapita na maisha yataendelea.
Imezoeleka sikukuu ni siku ya kula chakula kizuri, uvae nguo mpya, ukatembee mahala ambapo mtafurahia mandhari na chakula na vinywaji kishe mrejee nyumbani kulala au wengine kulala hukohuko, ama ualike wageni waje kula na kunywa au ualikwe mahala...
Ndugu, kama hukufanikiwa kusafiri, hukufanikiwa kuwa na gari jipya, hukufanikiwa kuwapa familia yako nguo mpya au mlo maalum (pilau nyama) wa sikukuu basi....
Kaa na familia yako mjadiliane kwa amani na upendo namna gani mnavuka mwaka mpya.
Inapendeza ukiwa na mahitaji yote hayo ila si lazima, ukipata sawa ila ukikosa basi usikumbatue huzuni.
Furahini katika Bwana tena Nasema Furahini....
Kila mwenye furaha ashiriki furaha yake na asiye nayo.
Sina mpangilio mzuri wa nini nataka kusema ila ikiwa huu ujumbe umekulenga. Amka, kaoge, kamshukuru Mungu, andaa kile ulichonacho jikoni basi furahi na nafsi, ndugu jamaa au marafiki walio karibu nawe hata kwa simu tuu.
Wale wanaopitia changamoto za ugonjwa, misiba, kesi mahakamani, polisi, nawaombea mpate ahueni.
Ntatupia picha baadae ya kile nilichobarikiwa nacho.
Kasinde Matata [emoji846].
Mkuu kama ni ule utani wa kwenye mpira ni mambo ya kawaida. Lakini kinyume na hapo basi,pole sana na Mungu akutie nguvu, maumivu tumeumbiwa wanadamu tuyabebe hadi kifo kitakapo tufika.Nilikuwa nanyi humu tukifurahi maisha lakini huu mwaka ulikuwa mgumu sana kwangu. Sikuwahi kupitia magumu kama haya toka nizaliwe. Namshukuru Mungu kwa yote
Asante mkuu. Utani wa mpira ni maumivu ya sekunde 2 tu yanaishaMkuu kama ni ule utani wa kwenye mpira ni mambo ya kawaida. Lakini kinyume na hapo basi,pole sana na Mungu akutie nguvu, maumivu tumeumbiwa wanadamu tuyabebe hadi kifo kitakapo tufika.
Nilikuwa nanyi humu tukifurahi maisha lakini huu mwaka ulikuwa mgumu sana kwangu. Sikuwahi kupitia magumu kama haya toka nizaliwe. Namshukuru Mungu kwa yote
Mkuu kama ni ule utani wa kwenye mpira ni mambo ya kawaida. Lakini kinyume na hapo basi,pole sana na Mungu akutie nguvu, maumivu tumeumbiwa wanadamu tuyabebe hadi kifo kitakapo tufika.
Mpendwa, kama hadi muda huu hujajua sikukuu inaendaje usipate msongo wa mawazo. Shukuru kwa uzima na afya uliyonayo, siku itapita na maisha yataendelea.
Namshukuru Mungu sana, 2023 umekua ni mwaka mzuri kwangu, kuna vitu vingi vizuri vimetimiaπ , hongereni kwa wote ambao wishes zenu zimetimia na kama hazijatimia wakati wa Mungu ni wakati sahihi let's keep on praying atajibu kwani sikio lake si zito hata asisikie.
I wish you all a Merry Christmas and happy new year π
Hapa ndio pa muhimu...
Kasinde ubwabwa twaula wapi leo?
Amina ahsante Kasie hivi bado lile jina Kasie mahaba linaendelea kutumika mtumishi?Asante kwa salamu, na kwako pia.
Ashukuriwe aliye juu kwa kufanikisha mengi kwa upande wako. Ikawe heri na neema tele kwa 2024.
Hongera pia kwa kujawa na moyo wa shukrani.