Moyo wa mtu ni kichaka

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,079
14,381
Ambwene mwasongwe kwenye wimbo wake wa nguvu ya kujua kuna sehemu anasema “Moyo wa mtu ni kichaka, umehifadhi mambo mengi”

Neno maisha ni fupi ila lina namna zaidi ya moja ya kulielezea, Watu wanapitia mambo mazito sana,
  • Kikazi
  • Mahusiano
  • Na familia kiujumla
Mengine ni aibu kubwa,huwezi kutamka au hata kuyaombea ushauri kwa watu wengine ,hivyo wanaona bora wakiishi nayo na wengine wamekufa na maumivu yao.

Unapoona mtu amejinyonga au kunywa sumu ajiuwe kwa hari ya kawaida unaweza kumlaumu au hata kuaani vikali(sina maana kua nnakubaliana nao) hapana. Siwezi kuzuia ila elewa kua kuna wakati unafikia
  • Unahisi hakuna sehemu salama kwako kupiga hatua
  • Huwezi kusimama kwasababu hauna pakushika
  • Huoni kama kuna asubuhi mbele yako
  • Hauhisi kama kuna siku mpya itakuja,
  • Mwisho unaona Afadhali kama usiwepo sababu uwepo wako ndio umekupa hayo!
Uonapo watu wengi kwenye pilikapilika za kila siku wanatembea wanapishana,huyu kaingia hapa kashika hiki kaenda pale. Kila mmoja kwa wakati wake kwa kitu chake hi ni kawaida, na hi ndio maana ya kuishi ila laiti ukiweza kumuuliza mmoja kwa mwingine akuambie yalipo ndani yake, akupe mkasa wa maisha yake

Kuna ambao utatamani kuwasikiliza. Na pengine wengine usiombe hata waendelee na mikasa yao. Watu wanaishi na makovu makubwa ndani yao,wengine wanavisasi na hasira kuu

Unapoona mama furani (l,r) ameolewa ikiwa ametoka tu kumzika mumewe kikawaida tutaona kwa namna yetu ila hatujui mengi nyuma yake! Hata kwa wanaume vivyo hivyo

Hii haina uhusiano na jinsia ya mwanadamu. Mwanaume anachukuliwa kama ni mtu mgumu kwa namna ya kani ila haina maana kua maumivu ya ndani yanatofautina. Mwanaume anaumia sana pale
  • Anaposhindwa kutimiza majukumu yake (kwa namna yoyote ile)
  • Au malengo yake yanapokwama
  • Au ngome yake kuingiliwa
Sawa na mwanamke pia japo pana utofauti kidogo kwenye maelezo yake. Unao marafiki wengi, unakumywa nao na kufurahi ila kamwe huwezi kuwaambia mambo furani, sio sababu watawaambia wengine ila ni kwasababu hauoni uafadhali ikiwa watajua

Ni kwasababu hakuna unafuu,haiupi moyo wako nafasi ya kupumua. Hivyo ni heri ukiishi nayo!..

Maisha ni hadithi. Maisha ni filamu unayoiigiza na kuitazama mwenyewe na kuwapa watu nafasi kidogo watu wengine waitazame. Shiriki huduma za jamii ishi na shilikiana na watu vyema. Ishi maisha yako, timiza wajibu na malengo yako. Mengine yaache kama yalivyo.
 
Mwanaume anaumia sana pale anaposhindwa kutimiza majukumu yake kwa namna yoyote ile

Mwanaume anaumia sana pale anaposhindwa kutimiza majukumu yake kwa namna yoyote ile

Ndio,
Hi iwafikie akina dada,mama wote
Unapomuomba kitu,jambo mume wako au boyfriend wako
Na kwabahati mbaya akashindwa kulifanya kwa kakati huo
Kikawaida utaumia Na pengine kukasilika sana
Ila elewa kua mwanaume anaumia zaidi!
Na pengine tabasamu lako ni dawa tosha!
 
Unao malafiki wengi ,unakumywa nao na kufurahi
Ila kamwe huwezi kuwaambia mambo furani ,sio sababu watawaambia wengine
Ila ni kwasababu hauoni uafadhali ikiwa watajua
Ni kwasababu hakuna unafuu,haiupi moyo wako nafasi ya kupumua
Hivyo ni heri ukiishi"" "" )

Haya maneno yamenigusa, huyu ni Mimi kabisa.... Rafiki anaweza akahisi sikumsaidia shida yake kwasbb nimetaka, kumbe Kuna Hali napitia na siwezi kumuelezea. Napambana nalo mwenyewe na hawez kuja kujua

Ubarikiwe, mtoa mada. Maneno yako yamenibariki.
 
Unao malafiki wengi ,unakumywa nao na kufurahi
Ila kamwe huwezi kuwaambia mambo furani ,sio sababu watawaambia wengine
Ila ni kwasababu hauoni uafadhali ikiwa watajua
Ni kwasababu hakuna unafuu,haiupi moyo wako nafasi ya kupumua
Hivyo ni heri ukiishi"" "" )

Haya maneno yamenigusa, huyu ni Mimi kabisa.... Rafiki anaweza akahisi sikumsaidia shida yake kwasbb nimetaka, kumbe Kuna Hali napitia na siwezi kumuelezea. Napambana nalo mwenyewe na hawez kuja kujua

Ubarikiwe, mtoa mada. Maneno yako yamenibariki.

Ahsante queen
Pole pia
Pambana kujenga heshima yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom