Moyo unauma, nahitaji ushauri wenu wana JF wenzangu

Moyo unauma, nahitaji ushauri wenu wana JF wenzangu

bidam90

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
273
Reaction score
203
MREJESHO
Samahan sana wana jf kwa kuwa kimya bila kuwajuza kilichojiri nilibanwa kidogo na mambo ya chuo,simnajua tena mwaka wa mwisho(4th yr)!
Napenda niwashukuru wote kwa msaada wenu wa mawazo/ushauri pia na pole zenu mmeweza kunisaidia sana kujua nin cha kuamua ktk jambo zito hili lililonipata!

Bibiye alikuja Dodoma kwa kulazimisha kwani nilimkatalia nikamwambia haitabadili kitu chochcote hata akija!!Alifika dodoma mida ya sa 12 jion akapanga chumba(lodge) na kunipigia simu niende nikakataa nikwambia siwezi kwenda kulala chumba kimoja na yeye kwa huruma nikamwambia kama ana shida na mie anifwate chuo!Alikuja chuo huku akiwa analia sana,aliona aibu hata kunitazama sikumuongelesha chochote tukatafuta sehemu tukakaa huku nikiwa nimenyamaza kimya bila kumwambia chochote akawapigia simu rafiki zake waongee na mie nikakataa!
Aliomba sana msamaha na kukiri kweli alimpa hifadhi yule jamaa kwake kwa siku mbili japo anajuta kwani ni ujinga na huruma zake ndo zimemponza.Anavyodai hakufanya nae chochote japo jamaa alimng'ang'ania sana na kutaka walale wote kitanda kimoja wafanye........!Alimkatalia sana japo jamaa alikuwa anamlazimisha sana na kweli mda wote huo wa siku mbili alolala jamaa kwake nikimpigia simu alikuwa hana aman nikimuuliza alikuwa tu akinijib wamegombana na jiran yake!!
Bibiye ilibidi amwambie jamaa kuwa mpenzi wake naenda kumtembelea na hakutaka kuniambia kwani aliona aibu na kujisikia vibaya kunificha kwa mda wa siku mbili kuwa jamaa alilala kwake pia hakuniambia kuwa alikuwa ni mpenzi wake wa zaman ila anavyodai alipanga kuniambia siku ile ambayo nilitaka kwenda!!Jamaa baada ya kuambiwa mie naenda akamwambia mpenzi wangu kuwa atamuharibia/atavunja uhusiano wangu na bibiye, ndipo jamaa alipoamua kunipigia simu na kunieleza mambo mengi mabaya sana kuhusu mtu wangu tangu siku alofika Morogoro!

Sikutaka kuamini hayo yote alonambia nikamuombea hostel za rafiki zangu wa kike alale ila nikamwambie kesho asubuhi arudi zako morogoro nahitaji kufikiria, alizidi sana kulia na kuniambia kweli angekuwa amefanya chochote na yule jamaa asingethubutu hata kuja dodoma kuniona!!Alivyoona nakuwa mgumu kukubali akaniambia asubuhi na mapema ataondoka mie nikamwambia sawa haina shida unijulishe tu mda utakaotoka!!Asubuhi ilipofika nikajua atakuwa ashaondoka kumbe alikuwepo bado akazidi sana kuomba msamaha na kuapa hatarudia tena kunificha jambo lolote sikumjibu lolote nikamwambia twende nikusindikize ukapande gari urudi ulipotoka alizidi kulia na kunilaumu kwanin simuamin na hana namna nyengine ya kuniaminisha!!!!

Nilipofika mjini STAND moyo wangu ukaniuma sana kwanin nisimsamehe wakati kaomba sana msamaha na kujutia kosa alofanya nikaamua kwenda kumtafutia chumba(lodge) alale ili kesho yake arudi Mororogo!Tulipofika chumbani aliomba aende msalani nikachukua simu yake nikaanza kusoma msg's zake alokuwa akichat na rafiki zake ni kweli alikuwa akikiri ananipenda sana alimpa tu jamaa hifadhi kwa huruma na hamna chochote walofanya jamaa alikuwa anamtaka warudiane ila ye alikuwa anakataa na kumwambia tayari anae mtu jamaa alikasirishwa ndo akaamua aharibu uhusiano wetu!!
Aliporudi nikamwambia nimekusamehe alinikumbatia na kuzidi kulia sana alinilaumu pia kwanini sikumuamin mda wote huo ananimbia!!Alikiri anaogopa sana kunipoteza na hatarudia tena kosa lolote!!Nimemsamehe kwakwel bibiye kwasasa kazidisha saan mapenzi kwangu nimepiga mkwara sitaki kumuona mtu yoyote pale kwake kama ni discussion zifanyikie chuon na akinidanganya tena sina tena msamaha!!







ILIPOISHIA

Hivi navoongea wana JFyupo njiani anakuja Dodoma kuniona nimemkataza kuja ila analazimisha! Nimemwambia hata akija hawezi badilisha kitu chochote!!!Ni binti nilompenda sana nae alinipenda pia kiasi cha kuwa kwe mahusiano miaka mi4 sasa bila kusalitiana!nilikuwa msaada mkubwa sana kwake tangu alipokuwa akiishi kwenye maisha ya shida, mateso kutoka kwa mama yake wa kambo!nilikuwa mchango mkubwa sana kwake katika suala la elimu tangu amalize kidato cha sita mpaka sasa yupo chuo.Nilifanya jitihada sana kumtafutia chuo alipomaliza kidato cha sita akapata chuo Mbeya alifanikiwa kumaliza diploma nikaendelea kumpigania aendelee kusoma degree nilimuombea mkopo na kufanikiwa kupata (90%) chuo alipata Morogoro!

YALOJIRI
Alipofika chuo alipanga chumba nje ya chuo ili apunguze gharama za maisha bahati mbaya mizigo yake aliiacha Mbeya alipokuwa akisoma diploma kwa rafiki yake wa kiume ambae sikujua kuwa alikuwa ni mpenzi wake wa zamani japo waliachana kipindi wapo kidato cha tano!Jamaa alipanga nae kumtumia mizigo yake kutoka mbeya kumpelekea morogoro anaposoma!na wakati wote huo alikuwa akiniambia kuhusu hio mizigo kumuachia huyo rafiki yake!Kumbe jamaa nae alipangiwa chuo hicho hicho anosoma mpenzi wangu japo yeye alikuwa anachukua masters!

Hivo ikabidi mizigo asafiri nayo hadi Morogoro kumpelekea! jamaa alipofika na mizigo aliipeleka chumban kwa mpenzi wangu sikujua kuwa jamaa kalala siku mbili chumba kimoja na mpenzi wangu bila hata ya kuniambia kuwa jamaa kafikia kwake!Juzi niliamua kumpigia mpenzi wangu kumwambia kuwa ntaenda kumtembelea japo alikubali ila alileta sababu kibao kuwa na kazi za chuo nyingi aloachiwa!

Wakati huo huo nadhani alimwambia jamaa kuwa nategemea kwenda ikabidi jamaa anipigie simu anielezee kila kitu nadhani sababu alishazoea kuwa nae pale ndani wivu ulimuingia ikabidi aniambie! Sikutaka kuamini maneno ya jamaa ikabidi nichunguze kwa kumpigia simu mpenzi wangu kumuuliza yupo wapi akanambia yupo nyumbani peke yake kumbe alikuwa na jamaa, kwani pia nilimpigia jamaa na kumwambia amuongeleshee mpenzi wangu ili nisikie sauti yake ni kweli kuwa jamaa alikuwa akishinda na kula pale kwa mpenzi wangu mda wote tangu afike morogoro bila ya mpenzi wangu kuniambia!

Alipoona nimegundua ikabidi anipigie simu na kuomba sana msamaha na kunieleza kuwa jamaa hakuwa na pakulala ikabidi ampe hifadhi kwa siku mbili yeye alikuwa akilala godoro la chini jamaa akilala kitandan tofauti na alivyoniambia jamaa kuwa walikuwa wakilala kitanda kimoja!Niliumia sana kwanini anifiche kwa mda wote huo asiniambie kuwa ni mpenzi wake wa zamani na kwanini amruhusu jamaa alale chumbani kwake wakati ana rafiki zake kibao wa kiume wanaishi ndani ya hostel za chuo angeenda kumuombea pakulala!,na anavyodai hawakufanya chochote kwani jamaa alikuwa anamlazimisha sana warudiane ila alikataa sana pia alikuwa kwenye siku zake! Amelia sana nakuniomba msamaha kwa kutokuniambia ukweli ilibidi nimuulize kwanini aliamua kunificha akanambia aliona vibaya kuniambia kwani yule ni rafiki yake pia ni ujinga wake umemponza!

Mpaka sasa nipo kwe wakati mgumu katumia mpaka rafiki zake kumuombea msamaha anataka mpaka kuja Dodoma kuniona ili anielezee kila kitu lakini moyo wangu unasita sana! Nilimuamini sana wala sikutaka kumbana nani wa kuwa nae rafiki lakini leo hii kweli analaa chumba kimoja na mpenzi wake wa zamani siamini kuwa hamna kitu walofanya!

Ushauri wenu wana JF wenzangu nifanyeje?
 
Huyo mwanamke hajatulia ndio maana ulivyomwambia unataka kwenda alianza kuleta vijisababu.

Inamaana asingekuwa huyo jamaa kukupa ukweli mpaka sasa usingejua lolote. Usiumize kichwa kwa mwanamke mpumbavu angalia maisha mengne mwache aendelee na huyo jamaa.

Anakufanya ww mtoto. Kama aliweza kumwonea huruma kumpa hifadhi nini kitazuia kumpa papuchi?
 
Walk away dude! Usije fungua uzi kama huu tena huko bdae utakapokuwa ndoani na mna watoto. Kama angegongwa huko nje its another case. Ila kumlaza kwenye kitanda ambacho probably na wewe ukienda utalala. Hizo ni dharau, kutokujitambua na wala kukupenda kwa this...
 
Huyo mwanamke hajatulia ndio maana ulivyomwambia unataka kwenda alianza kuleta vijisababu.

Inamaana asingekuwa huyo jamaa kukupa ukweli mpaka sasa usingejua lolote. Usiumize kichwa kwa mwanamke mpumbavu angalia maisha mengne mwache aendelee na huyo jamaa.

Anakufanya ww mtoto. Kama aliweza kumwonea huruma kumpa hifadhi nini kitazuia kumpa papuchi?

Si unaona mkuu, badala auchapishe mwendo mchepuko njia kuu yaja anatoa sababu. Mi nakuambia wanaume tuna heshimu wake zetu coz wakije michepuko inatoka. The girl would obviously rather be with mchepuko than jamaa
 
huyo demu hana misimamo kaka tena achana nae kabisa baadae atakuja kukufanya kitu kibaya mno
 
Kwahiyo huyo jamaa mwenye kuchukua masters analilia penzi kiasi hicho?! halafu mkuu kuna huu msemo "MCHUMBA HASOMESHWI" jaribu kuuzingatia sana otherwise UTAKUJA KUJIUA.
Hizo hela unazompa kuanzia sasa sitisha mara moja na kama unazo nyingi sana basi fanya umjengee Mama yako japo kijifrem awe anapokea hela ya pango kila mwezi.
 
Ww mwenyewe unamtetea sasa tutakupa ushauli gan,? Amelala chin jamaa kitandani, amemulazimisha hawakufanya unahakili kweli, halafu ww mwenyewe tena unajihoji kwani asimuombee kwa marafiki zake wa kiume ili hali anao weng? Chukua hatua kaka, kama una msamehe poa ila ujuwe mzigo ulipakuliwa 100%endapo walilala chmba 1.
 
Napata picha ya MZUMBE MZUMBE !
 
pole kaka hyo mwanamke si mwaminifu hta ukimuoa atakuwa na tabia hzo kwa kua hajaona thamani yko ndo maana mwenyezi mungu kakuonesha mapema
 
Kwahiyo huyo jamaa mwenye kuchukua masters analilia penzi kiasi hicho?! halafu mkuu kuna huu msemo "MCHUMBA HASOMESHWI" jaribu kuuzingatia sana otherwise UTAKUJA KUJIUA.
Hizo hela unazompa kuanzia sasa sitisha mara moja na kama unazo nyingi sana basi fanya umjengee Mama yako japo kijifrem awe anapokea hela ya pango kila mwezi.
Mkuu asante kwa ushauri wako lakin suala la ada alikuwa akilipiwa na mzazi wake,me nilikuwa nikimsaidia pesa ndogo ndogo tu za matumizi
 
Ww mwenyewe unamtetea sasa tutakupa ushauli gan,? Amelala chin jamaa kitandani, amemulazimisha hawakufanya unahakili kweli, halafu ww mwenyewe tena unajihoji kwani asimuombee kwa marafiki zake wa kiume ili hali anao weng? Chukua hatua kaka, kama una msamehe poa ila ujuwe mzigo ulipakuliwa 100%endapo walilala chmba 1.
Hapana mkuu simtetei il najaribu tu kuwaeleza alivyokuwa anajitetea,hio sabab hainingii kabisa akili mwangu,lazima wamekumbushia tu
 
Back
Top Bottom