Moyo unaniuma sijui nifanyeje?

Moyo unaniuma sijui nifanyeje?

UTAUMIA UTALIA LAKINI MWISHO WA SIKU UTASAHAU NA UTAMPATA ANAAEKUFAA POLE SANA KIJANA SOMA KWA BIDII MAANA MKE MWEMA ATAPATIKANA KWA UKUBWA WA POCHI YAKO...ILA USIPOKUWA NA POCHI ILIYOTUNA UTAISHIA KUOA MKE ILIMRADI NA WEWE UONEKANE UMEOA.
 
Dogo acha utani bint ni bikra afu were uliishajiingiza mapenzini? na nani? mbona umeanza mapenzi ukiwa ndogo? utasababisha ka dushe kako kawe kibsmia tulia usome ukimaliza chuo fanya mapenzi uwezavyo kwa sasa utaendelea kuumia na vile pesa hauna utaendelea kudanganya eti bado nina bikra
duuuuu,unaishi dunia gani?
 
Miaka 19 bado unakuwa mzito kwenye maamuzi ya mapenzi? Nyie ndo mnaoishia kujinyonga
 
Dini siku hizi zimekuwa sehemu ya kuficha maovu. Eti ana hofu ya Mungu halafu ana wapenzi 4. How comes?
Mnadhalilisha sana Mungu wa wote. Kwenda kweny nyumba za ibada haimanishi kuwa una hofu ya Mungu.
Mkuu tulia, kuwa busy na masomo hayo yote yatakwisha na utayasahau.
Umenikumbusha kale ka msemo ka wazinzi '' Shetani alinipitia'' sasa ww umekaleta vice versa. Eti ana hofu ya Mungu lkn ana wapenzi 4 duh!
 
Wakubwa zangu shikamoni,

Niliamua kutulia na msichana mmoja tu nikaamua nitulie nae huyo, kiukweli nampenda sana mpaka nimeamua kuwa mwaminifu kwake. Jana alinielekeza kuwa nimekuwa muwazi sana kwake na yeye ameamua kuniambia ukweli kuwa amekuwa na mahusiano na vijana wengine 3 jumla tupo wa 4. Lakini yeye bado ni bikra na hajawahi kulala na mtu yeyote.

Yeye ni mtu wa dini sana na amekuwa akihudhuria semina wiki hili na akaamua kunieleza ukweli wote na pia anasema anataka kuachana na sisi wote na atulie. Mimi nimetafakari sana Jana hiyo nikaenda kanisani muhubiri akasema ili ufanikiwe ni lazima ujitoe mahali unapodhani ni comfort zone yako nikaguswa nikajua kuwa natakiwa kuachana na mapenzi nae na nisiwe na mwanamke yoyote. Umri wangu ni miaka 19, nimefaulu na mwezi huu naanza kwenda college na yeye bado yupo shule.

Baada ya kutoka church akili yangu ilitulia na kuniambia kuwa ninataka kuwa na amani nae ninatakiwa niachane nae na nikaridhia baada ya mimi na yeye kuonana nikakumbuka mambo mengi sana tuliyopanga pamoja na ninampenda kwa kuwa anajiheshimu na ana hofu ya Mungu. Moyo unaniuma toka hapo ninafikiria mipango yangu na malengo niliyokuwa nae ninaumia sana natamani hata nisingejiingiza kwenye mapenzi.

Ninatamani nifuate sauti ya Mungu ila ninatambua maamuzi ya Mungu ni magumu na ndio haya yanayonikumba sasa. Leo ninataka nionane nae sitapenda aondoke tukiwa hatujaelewana hili jambo litatuathiri sana na hatutaweza kuendelea na masomo na kiukweli tunapendana sana.

Nikifikiria sina cha kumwambia ninatamani niseme neno moja tu na roho yangu ipone haya maumivu ninatamani kumlaumu ninaishia kumsamehe kwa kuwa nampenda sana na pia ninatamani kuachana nae ila hofu yangu ni kuwa nitaumia sana siku za mbeleni.

Na sina mpango wa kuwa mzinzi ninatamani Mungu anibariki anipe mwanamke ambaye atakuwa wangu mimi peke yangu na asinisumbue. Inafika muda najilaumu sana kwanini nilianza mapenzi maana naumia sana. Wapendwa naombeni ushauri wenu nimwambie nini ili tuweze kuelewana na moyo wangu utulie. Na pia nifanye maamuzi yapi kuhusu sauti inayonena ndani yangu.
Sasa bro nakushauri kwamba huyo demu ni muongo na tena keshaliwa na kukunwa sana isipokuwa wewe umeingia kichwa kichwa na sasa anatingisha kiberiti,eti anataka aachane na nyie wote ili arudi kuwa binti wa kanisani,hii haingii akilini,mwambie hata wewe umepata mwingine na hutaki upate dhambi kwa sababu yeye ameamua kumrudia Mungu,hapo patakuwa patamuuuuuu hadi utakuja kunipa shukurani na utaamini mademu nuksi kwa kutikisa kiberiti,yaani uwe mkavu na umwambie kiume kuwa umempata mnaoendana kitabia na kimapenzi.Halafu kumbuka usicheze na elimu.
 
piga moyo konde na usonge mbele pia udumu katika maombi, michezo na ujichanganye na watu wengine. nothing is permanent not even our troubles, yatakwisha pia hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho Mkuu
You said it all....
Kingine zingatia masomo yako,build your dreams. Hujachelewa,start now..mapenzi hapo,tumeyakuta na tutayaacha.
 
  • Thanks
Reactions: THT
nilikua naisoma habari ....nilipofika hapo Mimi sijui Nina miaka 19 ....baaaas
 
Wakuu naomba mtofautishi kati ya mungu na MUNGU,hayo ni maneno ma wili tofauti
 
Mashaka yangu pekee ni huu ya umri wenu ambao naona bado ni mdogo. Nahisi ni umri ambao hisia zina nguvu zaidi kuliko akili, kwa hiyo uthabiti wa kudumu katika mahusiano ni hafifu sana.

Ungekuwa walau 25 ningekushauri kuweka msisitizo mpaka umpate kwa kuwa umesema unampenda na anajheshimu. Nakuhakikishia kuwa hiyo binti anatumia mbinuya kusema anaachana nanyi wote ili kuona ni yupi kati yenu yupo serious na yeye. Kumbuka hats katika utungisho (fertilization) ni sperm moja tu kati ya mamilioni ndiyo inayofanikiwa kuingia kwenye yai. Hiyo ni ile iliyoweza kukimbia, kuvumilia na kupambana hadi mwisho.

Be that sperm. Never give up.Ni wale tu wansopambana na kuvumilia hadi mwisho ndio wanashinda.
 
Mashaka yangu pekee ni huu ya umri wenu ambao naona bado ni mdogo. Nahisi ni umri ambao hisia zina nguvu zaidi kuliko akili, kwa hiyo uthabiti wa kudumu katika mahusiano ni hafifu sana.

Ungekuwa walau 25 ningekushauri kuweka msisitizo mpaka umpate kwa kuwa umesema unampenda na anajheshimu. Nakuhakikishia kuwa hiyo binti anatumia mbinuya kusema anaachana nanyi wote ili kuona ni yupi kati yenu yupo serious na yeye. Kumbuka hats katika utungisho (fertilization) ni sperm moja tu kati ya mamilioni ndiyo inayofanikiwa kuingia kwenye yai. Hiyo ni ile iliyoweza kukimbia, kuvumilia na kupambana hadi mwisho.

Be that sperm. Never give up.Ni wale tu wansopambana na kuvumilia hadi mwisho ndio wanashinda.
Tumeongea tumeelewana nimemwambia simwachii hat a iweje
 
Mkuu unatambia kwa sheria za serikali na dini miaka 19 sio mtoto. Umenikumbusha wakati nina umri unaolingana na huu nilikuwa nikiwafuata walionizidi umri na kuwaeleza matatizo yanayohitaji ushauri walinipuuza ila iliniumiza sana wakati huo mpaka nilipokuwa na umri mkubwa zaidi nikatambua kwamba ni changamoto za maisha tuu. Ukifungwa mlango mmoja Mungu atakufungulia mlango mwingine, tena pengine bora zaidi.
Sawa mkuu
 
simama katika kweli ya Mungu utapata majibu.
 
Unaijua GPA ya 3.5? Ukishaijua amua uendelee kuumwa moyo au ukomae na GPA ya huko college kwako..
 
Hahahahahaa UKWATA, CASFETA, MAPENDO DAIMA ya shule huku mtaani ni magumu. Kuna maisha halisi huku, mshike Mungu kisawasawa Sio kishule shule. Utakuja kuona kuwa hakuna investment ya hovyo Kama ya kwenye ngono!!! Hailipi kabisa aiseee, Wazuri wapo wengi sana, kwa umri wako kuwa na Mpango Mkakati na binti Wa mwenzio ni uchochezi!
 
Back
Top Bottom