Moyo unaniuma sana

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
6,805
8,792
Habari za kazi na shughuli za hapa na pale

Juzi nilikua mahali napata lunch, wakati naendelea kupata msosi akapita omba omba flani kipofu yuko na mtoto, alivopita hakunijali akaenda kwa wengine mimi pia sikumtila maanani sana japo hua na tabia ya kuwapa pesa nikiwa nayo

Wakati anatoka akapita kwangu akaninyooshea mkono yule mtoto, daah!! Nikamwambia sina pesa lakini pesa ilikua kwa muhudumu nikaona uvivu kuomba chenji nimpe yule mtoto,

Yule mtoto aliondoka kwa huzuni sana, moyo uliniuma sana mpaka sasa bado nikikumbuka nilivomwambia sina pesa naumia moyo

Nimejaribu hata nikampe mwingine lakini bado tu, yule yule nataka ndio nimpe...

Haya maisha hakuna ajuaye kesho..
 
Kama hicho kitendo kinakuuma kweli basi ni fundisho, usisema tena huna wakati unazo!
 
Mimi kwa kweli Mungu atanisamehe, nilikua nawasaidia sana ila kuna jambo la kushangaza limenitokea mara 2 katika mazingira ya kutatanisha hadi leo sina imani nao,japo naamini sio wote wenye nia mbaya, kuna mmoja alikua mjamzito amechoka, akaniomba hela nilikua natoka chuo mfukoni nilikua na elfu 36,000 nikampa buku,kufika stand kuangalia mfukoni sina hata mia, pamoja na kuwa sijawahi kudondosha hela ila sikumtilia shaka nikajiaminisha huenda nimedondosha sehemu japo hapakua na mazingira yeyote ya kudondosha hela iliyo kwenye wallet huku wallet ibaki. Mara ya pili nilikua bara nimekunywa soda, nikalipa elfu 10,000 muhudumu kanirudishia 9,400 akaiweka mezani akaja mmama na watoto wanaomba msaada nikachukua ile 400 nikawapa elfu 9 nikaweka mfukoni, kufika home sina hiyo hela mfukoni, ilikua 2012, toka wakati huo hadi leo sijawahi kumsaidia yeyote yule anayeomba msaada barabarani.
 
daahh, wema hauozi ila,
 
Back
Top Bottom