Moyo nahisi unatoka, nishaurini nipumue

Moyo nahisi unatoka, nishaurini nipumue

Oxpower

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,182
Reaction score
3,118
Habari wanajamvi,

Ndugu yenu nimeachwa na mwanamke niliependa, mwanamke wa ndoto zangu, mwanake nilietamani kuwa nae toka niko shule, nimetumia muda, nguvu, pesa na jitihada nyingi kuwa nae lakini leo hili kaniacha, dah moyo unauma.

Story mpaka tunafika hapo iko hivi;

Kwa kifupi, mimi na mpenzi angu tunaishi mikoa tofauti hivo kupelekea kuwa tunakutana kwa msimu.

Mwezi wa 10 nilikutana na mpenzi angu lakini nikagundua kitu ambacho kilinishtua, bado alikua anawasiliana na x wake, niliumia sana ila aliniahidi kutorudia tena.

Mimi nikarudi mkoani kwangu, nikawaza sana kuhusu ile hali hadi nikakumbuka kadada flani hivi ambako niliwahi kukapenda nako kalinipenda sana ila hatukubahatika kudate.

Nikakatafuta bahati mbaya nae akawa anabwana tayaru,nikakomaa nae akanielewa na tukaanza uhusuano kwenye simu maana nae yuko mbali.

Mwezi wa 11 mwanzoni nikaenda tena kumtembelea mpenzi wangu, nilipofika akanikutamisha na x wake na kuongea mbele yangu kuwa hawez kuendelea nae maana yuko na mimi,na huyo x wake ananifaham vizuri tu maana nae alianza kudate nae baada ya mimi kumuacha huyo binti na kabla sijamuacha walikua marafiki,kwahiyo tulivyorudiana akawa hana chake akaniaminisha na mimi nikaamini ilo.

Tatizo likaja pale tulioenda kupata nlichokifuata, si ndo nikaacha simu yangu inazaga, akasoma sms za mchepuko wangu zote, nikakiri kosa na nikamuahidi nitamuacha.

Ni kweli nlivorudi haikua ngumu kuuambia mchepuko tuachane maana nao upo kwenye mahusiano, nao ukafurahi maana nao ulikua na hofu juu ya bwana ake akijua, ila sasa tukawa tunachat tu kawaida na kuna vitu aliniomba nimnunulie nitume kwenye gari maana yeye yupo mkoani.

Sasa majuzi nmekutana nae tena huyu mpenzi angu,ile tu tumetoka majambozi si ndo simu ikaingia sms,akataka kuisoma yeye kwanza,maskini ya Mungu mimi nlajikuta tu namkatalia alafu sikua hata na reason.

Baada ya kuona mwenzangu yupo siriazi ikabidi nimpe tu kabla hata mimi sijaisoma, akakataaa na akadai hatojishugulisha tena na simu yangu.

Akaniambia mimi sio muaminifu na hana sababu yakuendelea na mimi kuachana na hayo pia amewahi kunipiga fumanizi miaka ya nyuma.

Sipo tayari kuona nampteza, naomben ushauri wenu waungwana maana simu hapokei sms hajibu na bahati mbaya juz nlipaalta hasira nikatukana, ila nampenda sana sipo tayari kuachana nae.

Nisaidien jamani nimekwama.
 
Wote ni majambazi sio tu wezi. Mmepewa karama hiyo na shetani, Mungu atakupa wa kufanana nawe na ndo huyo, jitahidi mfunge ndoa nyie waasherati mtapendana sana, alafu kila mtu awe anasoma sms sa mwenzie na mfanye majumuisho ili mpate bingwa wa kuchepuka....jinga wewe watu wako bize unaleta story za kihingaaa
 
Ha ha ha ha
 
Simu jamani simu kwa nn usingemuoa hiyo umpendae
 
Wote ni majambazi sio tu wezi. Mmepewa karama hiyo na shetani, Mungu atakupa wa kufanana nawe na ndo huyo, jitahidi mfunge ndoa nyie waasherati mtapendana sana, alafu kila mtu awe anasoma sms sa mwenzie na mfanye majumuisho ili mpate bingwa wa kuchepuka....jinga wewe watu wako bize unaleta story za kihingaaa

hahaahhaaaaaaaaaaa
 
Nipe namba yake nikuombee msamaha ila utalipia huduma za ushauri nasaha (consultancy fee) nayo itakuwa 2.4% na utailipa kupitia bank ya stanbic...ahahahahaaha...fanya haraka niko bize wateja ni wengi ujuwe.
 
Hahahahaha, kula matunda ya kazi yako.Mrudie Mungu tubu tafuta wako huyo hakua wako.
 
Pole mkuu,najua unachokifeel..imefanana kidogo na story yangu lakini jikaze ujaribu kuongea nae

Incase akizingua jitahidi umove on..Ni vigumu lakini kwenye nia utaweza na utakuwa mwenye furaha tena
 
Wewe ulikuwa huna sababu ya kumkatalia kusoma sms ila
yeye alikuwa na sababu ya kuisoma hiyo sms
 
Mimi Binafsi Nasubiria Niliyepangiwa Nae Tu Hawa Gf Wa Zaman Ni Majanga Aisee
 
Njo Nikupeleke kwa mganga

Dah last thing nitafanya in my life..

Maana yangu ni kitu ambacho I am ready to go to the grave kuliko kwa mganga wa kienyeji..

Never ever ndugu..

Jiulize kitu kwani kabla haujamkuta huyo ulikuwa unaishije?

Know thyself - Jitambue hivyo yatosha!
 
keshaondoka ndo unaona umuhimu wake sio?, ila kabla unllikuwa unaona poa tu kuwachanganya!!!! wacha uisome namba tu mpendwa maana hakuna jinsi
 
Nipe namba yake nikuombee msamaha ila utalipia huduma za ushauri nasaha (consultancy fee) nayo itakuwa 2.4% na utailipa kupitia bank ya stanbic...ahahahahaaha...fanya haraka niko bize wateja ni wengi ujuwe.

hahahaha kwanini isiwe 3.4% me nachukua hiyo moja ndugu. maana jamaa moyo utaacha mwili huyu
 
Hili fumbo la nyinyi wanaume kudai mnawapenda sana wapenzi mlio nao na kwa wkt huo huo mnachepuka ndo hua silielewi at all, kwa nini umchukulie mtu for granted huku ukidai unampenda sana?bora uachwe tu.
 
Back
Top Bottom