Moyo Na Mfumo Wa Mishipa Ya Damu Mwilini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo Na Mfumo Wa Mishipa Ya Damu Mwilini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Moyo ni ogani (organ) muhimu sana katika maisha ya uhai wa mwanadamu. Unapozungumzia moyo katika mwili wa mwanadamu ni sawa na kuzungumzia injini katika chombo cha moto. Hali hii inatokana na ufanyaji wa kazi wa damu, ambao msukumo wake mkubwa unaendeshwa na Moyo.

  Moyo upo katika sehemu ya kifua na sehemu kubwa ya moyo upo upande wa kushoto. Moyo umeumbika ukiwa na tabaka nne ambazo zimepangana kutoka katikati hadi tabaka ya nja kabida. Kitaalamu tabaka hizo huitwa:-
  Indocardium
  Mycocardium
  Pericardium.

  Tabaka hizi ni aina ya nyama laini iliyozungukwa na misuli (muscles) mingi. Hata hivyo kutoka tabaka moja hadi jingine kuna aina ya mafuta flani (fluid) ambayo yana utelezi, kazi kubwa ya mafuta hayo ni kuzizuia tabaka zisigusane. Mafuta hayo huwekwa na Allah S.W kwa ufundi wake katika uumbaji wake, ndipo aliposema katika Quraan :
  Ametukuka Mwenyezi Mungu, mbora katika uumbaji 23:14 Mafuta hayo huanza kuonekana katika moyo tangu mwanadamu huwepo katika tumbo la mamayake. Utafiti unaonesha kuwa mtoto anapotimiza umri wa miezi minne, ambayo ni sawa na siku 120 au sawa na masaa 2081.

  Sababu za msingi wa mafuta hayo kuonekana katika wakati huo ni kuwa huu ndio muda ambao mimba inaanza kuonekana. Uhai wa mtoto katika kipindi hicho, ndipo hata daktari huanza kupima mapigo ya mtoto.
  Mwenyezi Mungu ameumba, ndani ya moyo kuna chemba nne. Chemba hizi zimepangana vizuri kwa upande wa kushoto wa moyo vipo viwili na upande wa kulia vipo viwili. Kitaalamu huitwa Right ventricle, right atrium (kwa upande wa kulia) na kushoto kuna Left ventricle na left atrium.

  Kazi kubwa ya chemba hizo ni kupokea na kutoa damu mwilini. Damu inayopokelewa na moyo ni ile, iliyokwisha tumika ambayo huitwa deoxygenated blood. Damu hii kwa kawaida huwa na hewa ya Carbon dioxide, hewa ambayo ni chafu hivyo damu nayo huchafuka kwa kuwa imeshafanya kazi mwilini.
  Mshipa unaingiza damu iliyotumika kutoka mwilini kwenda moyoni huitwa, Superior and inferior vanecaver. Huu ndio mshipa ambao hubeba damu yote yenye carbon dioxide kutoka utosini hadi nyayoni. Damu hii huanza safari yake, katika mishipa midogo midogo ambayo huitwa capillaries.

  Damu hiyo husafirishwa na kuingia katika mishipa mingine ya damu inayoitwa Veins, ambayo husafirisha hadi katika pcha mbili za Vane caner. Mara baada kuingia katika bomba hilo kubwa, huwa inadondokea katika kimoja miongoni mwa chemba za moyo. Damu hiyo hupokewa na kusafirishwa kutoka katika chumba hicho kwa mfumo wa mawimbi. Hali hiyo inatokana na tabia vya chemba hizo kutanuka na kusinyaa wakati wa kupokea na kusafirisha damu.

  Kutoka katika chemba kinachoitwa Ventricle kwenda katika chemba cha Antrium, katika eneo hilo linalounganisha chemba zote mbili kuna mwanya mdogo hubakia ambao huruhusu damu kutoka upande mmoja na kuelekea upande wa pili bila kurudi nyuma.

  Hali hii inatoakana na kuwa kama damu itarudi nyuma na ikakutana na damu inayotoka mwilini itafanya chemba cha moyo kupokea damu nyingi ambapo kitazidiwa ujazo na kupasuka.
  Mwanya huo, unaoruhusa damu kutoka chemba moja kwenda chemba cha pili umefungwa aina fulani za misuli (muscles) inayofanya kazi bila ya kutegemea ufanyaji kazi wa akili.

  Muscles hiyo inaitwa Involuntary muscles hufanya kazi kama mtu husika amelala. Zipo baadhi ya sehemu nyengine za mwili wa mwanadamu zilizofungwa misuli hii sehemu hizo pia hufanyakazi hata kama ukiwa umelala. Mfano wa sehemu hizo ni mfumo wa hewa katiak mapafu, jinsia macho n.k

  Damu inapotoka katika chemba cha kwanza na kuingia katika chemba cha pili kwa mfumo wa mawimbi, hapo huchukuliwa tena damu hiyo hupelekwa katika mapafu ya mwili kupitia katika mshipa unaoitwa Pulmonary Artery. Lnego kubwa la kuletwa damu katika mapafu ni kufanyiwa mchujo, hapo damu hutolewa ile carbon dioxide na kuingizwa hwa safi ya oxygen. Mara baada tendo hilo la kupakiwa oxygeb kwa kupitia Red blood celss, damu hubadilika kwa kutoka hewa chafu (deoxygenated blood) na kuwa hewa safi (oxygenated blood)

  Damu inapokuwa safi, huchukuliwa tena na mshipa mwengine wa damu unaoitwa Pumlonary Artery. Damu husafirishwa kutoka katika mapafu na kuletwa tena upande wapili wa moyo, ambapo hpitishwa kwa utaritibu wa mara ya kwanza.
  Baada ya tendo hilo, damu hutoka katika moyo na kuisambaza mwili mzima kupitia mshipa mkubwa wa damu unaoitwa Oater ay Artery mkuu. Mshipa huu wa damu ndio uliotajwa na Mnweyezi Mungu ndani ya Quraan.
  " Na kama angeliongeza neno lolote lisilokuwa hii Quraan. Bila shaka tungelimkata mshipa wake mkubwa wa damu na tukaitoa roho yake. 69:44-46

  Mara damu inapoingia katika mshipa huu hugawanywa katika mshipa mdogo wa arteries na baadae huingizwa katika mishipa midogo

  midogo ya capillaries ambapo damu husambwaza mwili mzima.  [​IMG]
   
 2. m

  mahmoud abbas Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka umetisha nlikuwa sijui iyo kitu
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Usimtukane Mahmoud abbas Moderator atakufungia usiweze kuingia humu Jamii forums kuna watu humu ndani ya Jamii forums wanaleta chuki dhidi ya Uislam mimi huwa nawaita Walokole maana yake Waumini Wa Dini ya Kikristo Walokole ni Watu wenye Msimamo

  Mkali na chuki dhidi ya Dini ya Kiislam wewe muache alete Pumba zake Moderator anamfuatilia mkuu usimtukane mtu humu ndani muambie tu

  ukweli asipojirekebisha bonyeza Kitufe chekundu hapo juu yake yaani hiki ( [​IMG] ) Kumshitaki kwa moderator kisha Mkuu modeartor ata Deal naye asante sana Allah yu pamoja nasi inshallah.
   
 4. m

  mahmoud abbas Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poa kaka na asante kwa kunielekeza jinsi ya kumshitaki kwa moderator
   
Loading...