Moyo Mwema wa Juma Volter Mwapachu

Moyo Mwema wa Juma Volter Mwapachu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
MOYO MWEMA WA JUMA MWAPACHU

1743603034929.png

Tulikuwa tumeshamaliza kuzika taratibu tunarudi kwenye magari yetu tuondoke Pande turejee Tanga mjini.
Akanijia mmoja wa vijana walionipokea Tanga nilipohamia mwaka wa 1997.

Nitamtaja kwa jina moja tu la kificho "Mwinyi."
Mwinyi alikuwa kati ya rafiki zangu wakubwa.

Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa sekondari labda kidato cha kwanza.

Mwinyi akanisalimu na kunipa pole kisha akaniuliza kama nakumbuka "note" niliyompa ampelekee Juma Mwapachu Dar es Salaam miaka mingi iliyopita.

Mimi sikuweza kukumbuka.

"Nilipomaliza kidato cha nne nilitaka niendelee kidato cha tano nikaja kwako na kukueleza kuwa nyumbani hawana uwezo wa kunisomesha kidato cha tano na cha sita.

Basi wewe ukaniandikia "note" ukanipa ukaniambia niende Dar es Salaam nikamuone Juma Mwapachu.
Nilikwenda nikamuona na nikamweleza shida yangu.

Juma Mwapachu ndiye aliyenisomesha hadi nikamaliza kidato cha sita."
Nilipigwa na butwaa.

Vipi na iweje mimi nimesahau jambo kubwa na hisani kama hii?
Sote tukashukuru.

Alhamdulilah.
Mwinyi alipomaliza kidato cha sita alikwenda Uingereza kuendelea na masomo.

Mwinyi aliselea Uingereza kwa yapata miaka 20.
Kamaliza masomo na akatafuta maisha huko.

Mwaka jana nilikuwa na utafiti wa kulitafuta kaburi la Abushiri bin Salim.
Nikaenda Tanga.

Mwinyi akaja hoteli niliyofikia kunisalimu.

Ndiyo alikuwa muda karejea nyumbani baada ya muda mrefu kupita akiwa Uingereza lakini mimi na yeye tulikuwa hatujaonana.

Nilipomueleza safari yangu ya Pangani yeye akasema atanipeleka na gari yake.
Tulivutana sana katika hili kwani mimi nia yangu ilikuwa kukodi gari inipeleke yeye hakutaka kunisikia kabisa.

Si tu alinipeleka Pangani bali aliwapigia simu wahusika Pangani kuwataarifu kuwa tunakwenda kwa shughuli maalum.

Huko kote yeye ni maarufu kwani ni mtu wa biashara.
Safari yangu Pangani ilikuwa na mafanikio makubwa sana.

Baada ya muda mfupi nilirejea tena Tanga kuelekea Pangani kuendelea na utafiti wangu.

"Sheikh Mohamed nimetingwa na kazi lakini In Shaa Allah kesho nitakuletea gari yangu na kijana akupeleke Pangani."

Hakika nilikuwa nimeelemewa na wema na ukarimu huu.
"Sheikh Mohamed kuna mambo mengi naona wewe umesahau."

Tuko ndani ya gari yake yeye anaendesha mimi niko pembeni.

"Unajua wewe ndiye uliyenifundisha mimi computer nilikuwa nikitoka shule nakuja nyumbani kwako unanielekeza.

Computer ile ilinifia mimi mikononi mwangu."
Mimi sikumbuki haya anayonieleza Mwinyi ila naikumbuka ile computer.

Ilikuwa zawadi kutoka kwa rafiki yangu Dr. Harith Ghassany.
Alininunulia tukiwa Muscat mwaka wa 1997.

Miaka mingi imepita.

Labda kama si kule kupelekwa High School na Juma Mwapachu, Mwinyi maisha yake yasingebadilika wala asingeweza kufika Uingereza kuendelea na masomo.

Juma Mwapachu alikuwa na roho ya peke yake.
Jumbe Menye aliyekuwa MC pale msibani alisema kuwa Juma Volter Mwapachu alilea vijana wengi wadogo zake.

Hiki ndicho kisa cha rafiki yangu Mwinyi na kaka yetu Juma Mwapachu na roho yake nzuri.
Allah msamehe na mtie peponi.
Amin.
 
Ukitenda wema umepanda mbegu njema & vice versa is True 😊

Asante mzee Mohamed kwa thread nzurii nzurii Kama hizi.
 
MOYO MWEMA WA JUMA MWAPACHU

View attachment 3291241

Ningependa kufahamu zaidi kuhusu mama yao na akina mwaoachu,alikuwa,mwarabu au mzungu?
 
Nimesoma hapa nikafikiri Mwinyi ndiye marehemu, kumbe habari inamuhusu marehemu Juma
 
Hivi huu msiba mbona naon kama serikali imeususa...
Sijaona wala kusikia tamko lolote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom