Moyo kuwa mkubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo kuwa mkubwa

Discussion in 'JF Doctor' started by Preta, Aug 21, 2010.

 1. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  Wapendwa natumaini mu wazima wa afya, nina nyanya yangu mwenye umri wa miaka 80 na ushee hivi, amekuwa akiugua hapa na pale, mnajua mambo wa uzee tena, sasa hapa juzi kati hospital (kcmc) wamemwambia moyo unakuwa mkubwa.....wakuu hii ishu inaakaaje...nini sababu ya hili tatizo? naombeni msaada wenu wa mawazo
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Preta, Kama nitakuwa nimewaelewa watoa huduma, watakuwa wamesema moyo ''umekuwa mkubwa'' kwa lugha ya kitaalam wanasema Heart enlargement hasa wanapotumia vipimo vya kuonyesha moyo.

  Hii ina maana kuwa moyo ''haujavimba'' bali umeongezeka size.
  Sababu ni nyingi, lakini kwa ufupi ni kuwa inawezekana mahitaji ya mwili[kwa damu] yameongezeka na hivyo kulazimisha moyo kufanya kazi ya ziada, au performance ya moyo haitoshelezi mahitaji ya mwili kwa sababu kadhaa, hali hii inaitwa compensatory mechanism.

  Kwahiyo kuongezeka size sio tatizo la awali bali ni dalili za kuwepo kwa tatizo mahali fulani. Sababu za tatizo zikitafutiwa ufumbuzi moyo utarudi katika hali yake ya kawaida, na kwa hiyo matibabu hayalengi moyo bali sababu zinazopelekea moyo kufanya hicho kinachoitwa ''compensatory mechanism''.

  Pamoja na maelezo haya, wataalam waliokaribu na mgonjwa wanaweza kutoa sababu halisi kutokana na picha au vipimo.

  Ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kuvimba kwa moyo[ mimi ningesema kuongezeka ukubwa] ni hatua za moyo wenyewe inazochukua kukabiliana na tatizo fulani linaloathiri utendajikazi wa moyo.

  Kwa vile bibi yupo KCMC nina hakika kuwa wataalamu watamshughulikia vizuri na usiwe na hofu, tumuombe mola matibabu yampe bibi unafuu na arejee hali yake.

  [kwa wasomaji: Unapomuona mbeba lumbesa ana kifua kimegwanyika, au bega limejaa hatusemi amevimba kifua au bega,tunasema amejaa au ameongezeka/ ametuna kifua au bega Enlarged chest/ shoulder muscles.
  Lakini ukijikwaa kidole, au ukawa na kidonda mguu ukavimba, au akawa umeumia kwa kitu mkono ukavimba, au ukawa umeumwa na nyuki uso ukavimba, hapa tunatumia neno kuvimba Inflammation hatusemi enlargement]
  Ahsante
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  asante sana mkuu kwa kunielewesha hili, maana watu wengine tukishasikia mambo yanayohusu moyo huwa akili zinahama
   
 4. r

  runemo Member

  #4
  Jun 8, 2016
  Joined: Apr 1, 2016
  Messages: 86
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 25
  Kw
  Upande wangu mimi mwanangu mchanga wa miezi 4, kapigwa xray amekutwa na moyo mkubwa,nilikuwa nataka kujua hili tatizo kama linatibika na ukuwaji wake utakuwaje hapo baadaye
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Jun 9, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunarudi katika hoja ya msingi kuwa kuongezeka kwa ukubwa ni dalili za tatizo lakini x-ray pek yake haielezi tatizo ni nini.

  Kuna umuhimu wa kuendelea na vipimo Zaidi kama ECG(EKG) kujua namna moyo unavyofanya kazi kwa kuangalia spikes and dips za moyo valve n.k.

  Hivyo kujua kama tatizo linatiba au la haitoshi kuchukua x-ray kama kipimo pekee.

  Hapa pia naomba nifafanue kidogo. X-ray ni miali inayopenyeza na kutoa picha.
  Ni technology ambayo imetumika kwa miaka mingi lakini inaelekea kuwa archaic

  Ukivunjika mfupa picha ya x-ray itaonyesha mfupa ulipovunjikia.
  Lakini x-ray haiwezi kutumika katika baadhi ya viungo kama figo kwasababu haionyeshi kwa undani 'functions' na jinsi ziinavyoathiri utendaji.

  Ni kwa msingi huo, figo zikiathirika ni muhimu kufanya blood test ambayo itaeleza kwa undani nini hasa kinasumbua kwa kusoma uwiano wa vipimo na kawaida ya vipimo hivyo

  Kipimo kama MRI au ECG vinaeleza kwa undani tatizo kuliko x-ray inayotoa picha pekee.

  Hapa ningeomba nitoe mfano rahisi wa 'mtaani', kuwa picha za mnato (still picture) inakuonesha tu picha ya kitu, haielezi kwa undani. Tufanye ndiyo x-ray

  Video inaonyesha kutoka kila kona, kama ni moto unaunguza wapi na unelekea wapi(vipimo kama ECG, MRI)

  Ahsante
   
 6. chakii

  chakii JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2016
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 16,471
  Likes Received: 14,164
  Trophy Points: 280
  Pole, hiyo ni moja ya complications za Hypertension/Shinikizo la Juu la damu/High blood pressure.


  Matibabu ni pamoja na kutibu presha na kama ana upungufu wa damu pia ni vyema akatibiwa.
   
 7. KAWETELE

  KAWETELE JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2016
  Joined: Dec 11, 2015
  Messages: 283
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 80
  na mm niongezee yangu;
  MOYO mkubwa kitaalamu inaitwa (cardiomegally), na inafuatana hapo KCMC wametumia kipimo gani kufikia hitimisho hilo. kwa mfano xray huonesha tu kuwa moyo umetanuka kifuani, lakini echocardiography huonesha pia vyumba vya moyo kama vimeatanuka au la. na kwa huku kwetu Tanzania SABABU KUBWA za mioyo kuwa mikubwa ni kutanuka kwa hivyo vyumba vya chini vya moyo viitwavyo ventricles'DILATED CARDIOMYOPATHY"(nina data sahihi)

  moyo mkubwa siyo ugonjwa ni dalili za magonjwa mengine..
   
 8. dre4691

  dre4691 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2016
  Joined: Feb 22, 2016
  Messages: 487
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 80
  Umeiva
   
Loading...