Movie ya Bodies At Rest

The Duke of Cambridge

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,493
3,712
Image may contain: 1 person, standing, text that says 'Blu u.rayDisc BODIES AT REST FSK 16 reigegeben RENNY YMARLIN (STIRB LANGSAM 2, CLIFFHANGER) EUROVIDEO'

..Walijua wamefanya kosa..wakajua kuwa wanatakiwa kulisawazisha kabla ya alfajiri..wakasawazisha kosa la kwanza..kwa kufanya kosa la pili..

..Waliihitaji risasi kutoka kwenye mwili wa maiti..risasi ilikuwa inatambulisha kuwa wao ndo wauaji..walitaka kuharibu ushahidi kwa gharama yoyote..iwe jua iwe mvua..

...risasi ipatikane...

...Ni maaskari waovu..walipewa medali za kipolisi mabegani..bastola zao zilipata leseni ya kuua kama ishara ya kuzuia maovu itapobidi..walijua walipaswa kulinda raia na mali zao..

..wao wakalinda mali zao wakasahau za raia...

..Ni pathologist nick chan..daktari alieaminiwa na nchi kwenye hospitali ya jiji..hata maiti zilijua nick yupo kazini..operesheni za kufumba macho ye aliomba tochi aangalie kwa karibu..

...Alibebeshwa heshima ya utumishi wa nchi hospitalini..akakubali..akaiishi heshima hiyo..mpaka ilipokuja siku ya leo..

..Siku mbaya,siku asiyopenda iwepo kwenye diary yake nyumbani..

..wahuni waliohitaji risasi kwenye mwili wa maiti..walimkuta nick kazini..wakamshurutisha awatolee risasi kinguvu..hawakujua..

..Kwenye mochwari yenye maiti zaidi ya mia..nick chan alihitaji utundu wa matumizi ya akili kuwaonesha kuwa ye hajaanza kazi jana..

..aliwapeleka mpaka kwenye maiti waliyoihitaji..akawatolea risasi wasiyoihitaji!...

..utajiuliza nick alitoa wapi risasi feki!..nick alijibu baadae swali lako..

..Yess maaskari wao ni wajuzi kwenye matumizi yao ya silaha..nick chan ni fundi wa kidaktari kwenye matumizi ya mwili wa binadam..vita ilichezwa kiufundi wa sindano na bastola..

..Walienda wakiamini wamepata risasi..wakarudi walipogundua risasi sio yenyewe..safari hii walikuja wakidhamiria kuua..

wakamkuta nick kajiandaa kulinda heshima ya maiti hospitali kwa akili za kidaktari..

..Wakimuacha hai kawaahidi kutowapa risasi..wakimuua watapaswa kuitafuta maiti mpaka waipate na waipasue wenyewe kutoa risasi..na muda sio rafiki kwao!..

..Haikutakiwa ifike asubuhi kwa wale wavamizi..na daktari aliihitaji asubuhi kwa gharama yoyote ile wavamizi wakamatwe..

..Ni mchezo wa paka na panya ndani ya mochwari mpaka kunakucha..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom