Movie Review 2019: Bird Box!

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,432
7,055
Kwa watazamaji filamu wenzangu, naona hii itakuwa ndiyo title ya kila thread ya movie review nitakayoianzisha kwa mwaka 2019.

Hatuna utaratibu wa kuchambua movies hapa nchini kama ilivyo huko duniani. Kama upo, basi tunaufanya kwa kiasi kidogo sana. Kwahiyo, naona we need to get in the habit of doing so. For entertainment and learning purposes. Huenda wadau wa filamu zetu wakajifunza baadhi ya mambo kupitia JF.

Tunaweza kuzijadili kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza kwa wale watakaomudu.
---

Okay.. Kuna movie mpya inaitwa Bird Box. Ni thriller. Inavuma sana kwenye corridors za wanaofuatilia movies. Kwa sasa inatrend kwenye toplist ya Netflix tangu irushwe December 2018. Asili yake ni kitabu kinaitwa Bird Box hivyo hivyo kilichotoka mwaka 2014.

Nimeitazama.

Nawakaribisha kupitia uzi huu tuichambue ili kushirikishana mitazamo yetu baada ya kuangalia na kutoa go ahead/stop order kwa wasiotazama.

Synopsis yake:

" Bird Box is a 2018 American post-apocalyptic horror thriller film, directed by Susanne Bier from a screenplay written by Eric Heisserer, and based on the 2014 novel of the same name by Josh Malerman. The film follows a woman, played by Sandra Bullock, as she tries to protect herself and two children from malevolent supernatural entities that make people who look at them go insane and commit suicide. Bird Box had its world premiere at the AFI Fest on November 12, 2018, and began a limited release on December 14, before streaming worldwide on Netflix on December 21, 2018.

Official trailer yake
 
Ichambue sasa tujue inaelezea nini
Sawa mkuu.

Kwa ufupi:
Kuna viumbe visivyoonekana vimevamia mji. Viumbe hivyo ukifumbua macho imekula kwako, lazima ujidhuru. Salama yako ufumbe macho au kama ukiwa ndani ya nyumba uzibe madirisha na milango mwanga usiingie ndani.

Katika hali ya taharuki, kuna kundi la watu wachache wamegundua siri hiyo hivyo wakajikuta wameingia kwenye nyumba moja. Na ndio kundi pekee lililobaki (survivors).

Kwenye kundi hilo kuna wadada 2 ni wajawazito na wakajifungulia humo humo ndani. Mmoja wao alifanya uzembe akafungua mlango na viumbe vikamvaa. Akajiua. Hivyo mtoto wake ikabidi abaki na yule dada mwingine ambaye ndiye Star wa hii movie.

Kila mtu anaonekana kukata tamaa kwa sababu hawajui wataishi hivyo hadi lini. Vyakula vinaisha na hakuna tumaini. Kwahiyo wenye kutiana wanatiana, wenye kulewa wanalewa. Kila mtu anaeeeeenjoy cha mwisho mwisho, kasoro huyo dada ambaye watoto wanampa sababu ya kupambana.

Sasa hizo harakati za kupambana kuwanusuru watoto ndio uhondo wa movie ulipo. Mambo ni mengi.
 
Kwa waliotazama naomba mje hapa tuichambue. Maana nimepitia reviews huko nje wapo watu wameiponda sana japo mimi nimeiona imetulia.

Lengo la hii movie ni kutisha na kusisimua. Kwa kiasi fulani inatia mchecheto.

Wanaoikosoa wanasema imeiga idea ya ile movie ya A Quit Place na Blind nini sijui. Hata hivyo wamempongeza Malorie kwa kuicheza vizuri na kuvaa uhusika. Yaani ameibeba movie!

Wengine wanasema ukisoma kitabu chake unafurahia zaidi..
 
Ila kuna mijamaa haizibi macho inawaangalia hao viumbe lakini hawajidhuru wanawatafuta watu na wakulazimisha kuangalia wenyewe wanadai ni viumbe wazuri kuwatizama.
 
Ila kuna mijamaa haizibi macho inawaangalia hao viumbe lakini hawajidhuru wanawatafuta watu na wakulazimisha kuangalia wenyewe wanadai ni viumbe wazuri kuwatizama.
Wale ndio nilishindwa kuelewa... Ni kama madish fulani hivi.. Yaani hao viumbe walikuwa na mawakala wao ambao ni mwezi mchanga!
 
Wale ndio nilishindwa kuelewa... Ni kama madish fulani hivi.. Yaani hao viumbe walikuwa na mawakala wao ambao ni mwezi mchanga!
Wale sio wazima hata mie sijawaelewa,yule mdada bonge mwenye mimba huruma yake ndio imeponza na wenzie wote.
 
Wale sio wazima hata mie sijawaelewa,yule mdada bonge mwenye mimba huruma yake ndio imeponza na wenzie wote.
Yule dish! Eti alipatwa na huruma kisa hata yeye ilishamtokea kuwa mlangoni akiomba msaada wa kufunguliwa.. So she knew how it felt!
 
Yule dish! Eti alipatwa na huruma kisa hata yeye ilishamtokea kuwa mlangoni akiomba msaada wa kufunguliwa.. So she knew how it felt!
ni nzuri kiasi niliicheki mwanzoni mwaka huu. ila wajawazito walikuwa hawadhuriki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom