Movement Against Story za Udini

Movement Against Story za Udini

KimaroKimario

Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
11
Reaction score
1
WanaJF kuna issue moja inanikwanza sana ya hawa viongozi wetu (kutoka vyama vyote na serikali) kutaka kupata umaarufu kwenye hii issue ya udini.

Mitaani tumekuwa tukiishi vizuri kama dugu moja bila mipasuko hii ya kidini sema kwa sasa naona shida inaletwa na hawa viongozi ombao kila wakifungua madomo yao ni kufuel issue ya udini kama janga la taifa. Halijawai kuwa janga na litakuwa janga nyie wapumbafu wachache mkiendelea na kelele zenu kila kukicha kwa kuleta worry na fear ndani ya mioyo yetu.

Mwisho wa siku hii mipasuko ikimaterialise ni sisi wananchi wa chini ndiyo tutaumia. Kwa hali hiyo ni wakati umefika tuwe na msimamo kuhusu hizi story za udini. Ushauri wangu ni sisi wananchi tuziboycott (tusizientertain) hizi story za udini bila kujali imesemwa na nani.

Watu wa media tunawaomba nyie pia kuingia kwenye vita hii na kutowapa watu media coverage wenye kuonekana wazi wazi wanatoa matamko ya kucreate fear au maudhui ya kufuel hii theory ya mpasuko wa kidini nchini.

Nchi haina mpasuko na yeyote anayesema hivyo anania mbaya ya kuona huo mpasuko wa kidini kwenye taifa letu.

Nawakilisha
 
mimi nadhani kuna ufa na si mpasuko, ila wanasiasa wameamua kuupanua huo
ufa kwa manufaa yao binafsi kwa kuhakikisha kila wanapofungua mdomo wanaliongelea, mauwaji na vitendo vya ulipuaji wa
makanisa ni vitendo vya jinai na siyo udini.
 
mimi nadhani kuna ufa na si mpasuko, ila wanasiasa wameamua kuupanua huo
ufa kwa manufaa yao binafsi kwa kuhakikisha kila wanapofungua mdomo wanaliongelea, mauwaji na vitendo vya ulipuaji wa
makanisa ni vitendo vya jinai na siyo udini.

Na hapo ndipo lilipo tatizo la msingi. Kukwepa ukweli kuwa kuna tatizo. Hizo hate literatures zinazotolewa kwenye majumba ya ibada ni mbegu mbaya ambayo matunda yake tutaanza kuyavuna hivi karibuni. Kuamua kunyamazia hali hii ni kuwapa nguvu wale wanaoeneza chuki hizi.

Suluhu pekee katika hili ni kwa serikali kutekeleza wajibu wake. Kila tendo linaloashiria uchochezi wa kidini lichukuliwe hatua zilizo dhahiri kwa jamii. Hii itasaidia sana kudhibiti vitrndo hivi. Tusioneane aibu.

Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba serikali imejionesha kuwa haina ubavu wa kuvichukulia hatua vikundi ama taasisi zinazoeneza propaganda chafu za udini. Hofu ya dola imeyeyuka mithili ya icecreame. Sasa kila mwenye ujasiri anajiona kuwa yuko juu ya sheria.

Tunakoelekea tutataka raisi asiye profess imani yiyote ile. Kuwa na imani ya dini fulani iwe ni automatic disqualification ya kuwa rais! Ni mtazamo tu.
 
Kwa sasa issue ilivyo ni sawa na ile kauli ya 'Abiria chunga mzigo wako' maana kondakta (serikali) hawezi kukusanya nauli na kulinda mizigo.
 
Tunakoelekea tutataka raisi asiye profess imani yiyote ile. Kuwa na imani ya dini fulani iwe ni automatic disqualification ya kuwa rais! Ni mtazamo tu.
Umechelewa, Kwenye rasimu ya katiba mpya hilo halimo!
 
sasa hapa unamaanisha nini ndugu yangu???

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,
Mtumwa hufika sehemu akaanza kumnunia bwana wake na hata kumrushia mawe,
Haukuwahi kusikia kifua chaweza geunga mkongo?
Suala la udini litaendelea sana kwa sasa 7bu tu yule mtumwa kaamua kumkandia bwana wake we unadhani bwana atachuna tu hivihivi? Lazima atapetape ila no way out keshamwaga mboga mtumwa ameamua nae kumwaga ugali.
What goes around comes around.
"You can cool somepeople for sometime but you cannot fool all for all time" (A CERTAIN GREAT PHILOSOPHER I DONT REMEMBER). You get me? Hv a gudtym.
 
Back
Top Bottom