Mourinho akataa kumrithi Scolari

Mourinho akataa kumrithi Scolari

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,439
Reaction score
29,632
Brazil inasemekana kujaribu kumshawishi Maurinho, kocha wa Chelsea, ili akabidhiwe jukumu la kukifundisha kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil, lakini Maurinho amekataa na kudai asingependa kuiacha Chelsea kwa sasa.

Baada ya kipigo cha karne cha Brazil kwa kuchapwa 7-1 na German na 3-0 na Netherlands ndani ya nchi yao wenyewe, wa-Brazil walifikiria mwisho wa matatizo yao ni Maurinho, hasa katika Mashindano yajayo ya Copa America 2015 na Kombe la dunia mwaka 2018 huko Urusi.

Kikosi cha Brazil kinakabiliwa na mechi nne za kimataifa za kirafiki mwaka huu; dhidi ya Colombia Sept. 5 huko Miami; kisha dhidi ya Ecuador on Sept. 8 pale New York; halafu dhidi ya Argentina Oct. 11 mjini Beijing na hatimaye dhidi ya Turkey Nov. 12 jijini Istanbul.

Source: Daily Star, UK
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom