Binafsi nashindwa kuamini kama hawa madaktari wote niwendawazimu na wasio na utu. Kwautulivu mkubwa bila ushabiki wala ushawishitoka upande wowote, nimeliangalia hili swala kwa uhalisia wake ambao hata mimikama muhudhuriaji mahospitalini nimelinganisha mambo.
Kwanza chanzo cha mgogoro nahisi si ule mgomo wa Interns,ingawa wengi wanaamini hivyo. Najua ni kutowajibika kiufasaha kwa viongozi wetuwenye dhama juu ya mambo ya Afya. Ule mgomo wa Interns ni kiashiria kimojawapotu, maana swala lile lilishughulikiwa kisiasa na propaganda nyingi, binafsinilipata hasira na vijana wetu tunaowategemea wawe madaktari bingwa baadaye,ila baada ya kuibuka kwa ukweli juu ya jambo lile na kwamba walikuwa na madaiya msingi ambayo watu wachache tu waliamua wasijishughulishe. Pia nilipatwakichefuchefu baada ya kusikia maovu ya viongozi wenye dhamana wakitumiamadaraka yao kufanya ufisadi kwa kinga ya madaraka yao. Hili pia lilidhibitishwana Mh. Waziri Mkuu alipowasimamisha baadhi ya viongozi kwa kuwatuhumu baadhi yahayo tuliyoyasikia.
Ninakila sababu ya kudhibitisha kuwa Madaktari wanafanyakazi zao katika mazingira hatarishi sana. Napenda nitoe mfano mmoja, ambapoMezi Januari tulimpeleka mgonjwa wetu wa Kansa pale Hospitali ya Ocean Road,Dar es salaam. Mgonjwa alikuwa kwenye hali mbaya na alishapata vidonda vikubwavisivyotazamika bila ujasiri wa kutosha. Tulipofika pale tulipokelewa vizuri,tukapea kitanda. Ila kabla Daktari hajaanza kuzunguka kwa ukaguzi,tulitaarifiwa mapema na wauguzi wasaidizi kuwa ni muhimu tuwe na vifaa/dawa ilikuwezesha ukaguzi na matibabu. Kwasababu tulihitaji maelekezo ni vifaa ganihasa nilimuomba atuorodheshee, kweli nilishangaa hata gloves na dawa ya kusafishiakidonda ilibidi kununuliwa na mgonjwa pia. Basi kulikuwa hakuna cha kufanyaikabidi kwenda Posta Mpya kwenye Mapharmacy ili kutafuta vifaa/dawa hizo.Napenda kuwajulisha pia, kuna wagonjwa walishindwa kukaguliwa vizuri, iliwa nikugusa majeraha au hata kusafishwa kwa frequency inayotakiwa kutokana na kukosavifaa hivyo. Pia imeshakuwa ni kanuni sasa, kwa wamama wajawazito kutembea navifaa vyote hadi gloves pindi wanapokaribia kujifungua. Maana wanaweza patwauchungu wakiwa njiani/kwenye shughuli nyingine mbali na nyumani hivyokuwahishwa hospitali kwa kujifungua. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamab, hivi hizigloves na vifaa vingine anavyotembea navyo huyu mama vinakuwa salama (sterile)kama inavyohitajika. Maana anaweka tu kwenye kikapu na kuendelea na shughulizake zingine. Yapo mambo mengi na wengi wetu tunayajua ila si wakati wake sasa.Napenda kuwaambia wale wanaoshabikia propaganda za mgomo huu, waende wakajioneewenyewe mahospitalini.
Napenda kuishauri serikali, kwahili wasijiridhishe napropaganda tunazozisikia kwenye vyombo vya habari na hata humu jukwaani. Sisindiyo waathirika wakubwa na ukweli zaidi tunaujua sisi. Mara kadhaatumeshuhudia maafa ya wapendwa wetu kwa ukosefu wa vifaa vidogo tu ambavyo leohii tunasikia madaktari wakiomba kupatiwa. Hivyo tunaomba Busara itumike katikakulishughulikia swala hili, na si kutafuta nani mshindi. WOTE TUWEKE SIASAPEMBENI NA TUANGALIE UHALISIA. Swala la kuondolewa kwa Mawaziri wa Afya siSerikali kuonyesha udhaifu, bali ni kurudisha IMANI kwa Madaktari na sisiwananchi pia. Mara ya kwanza mgomo huu, tulitarajia taarifa yenye ufumbuzi wamatatizo ya msingi toka serikalini, lakini tulipomsikia Waziri husika Bungenikutuletea Ngonjera ya kuwa Dr. Ulimboka si Daktari, badala ya kutuambia kiinina utatuzi kwakweli hata sisi wengine Imani ilitutoka na kuona sasa swalalimehskuwa vuta nikuvute. Tunatarajia safari hii serikali itawajibika ipasavyona Tunawaomba madaktari mrudishe moyo ili muweze kutuhudumia. Wananchitusikubali kuingia kwenye mtego wa ama kuwachukia madaktari au KuichukiaSerikali. Natumaini bado serikali inawatu wa kuweza kulishughulikia jambo hilivizuri ipasavyo bila kukimbilia suluhu za jazba. Hatutapenda kuona nchiinaingia kwenye machafuko eti kwasababu ya vuta nikuvute katika sakata hili.Nasisitiza tusitafute MCHAWI bali tuzingatie uhalisia na uwezo wetu. MunguIbariki Tanzania