Mount Meru Hospital mgomo wa madaktari umeanza rasmi

massai

JF-Expert Member
May 2, 2011
653
137
Hospitali ya mkoa wa Arusha nao safari hii wameungana na madaktari wenzao wa muhimbili katika mgoma usiokua na mwisho mpaka madai yao ya msingi yatakapo timizwa.

Ikumbukwe kua hule mgomo wa mara ya kwanza Arusha hawakushiriki kabisa.

ANGALIZO KWA JK NA WASHAURI WAKE:

Kama ijulikanavyo mageuzi yataanzia kaskazini, basi sasa ni wakati muafaka kwa JK kuchukua maamuzi haraka iwezekanavyo tofauti na hivyo pale magogoni atakua anapasikilizia akiwa msoga kama the huege. Machalii wa Arusha sio watu wa kufanya nao masihara hata kidogo, hakuna atakayekubali kuvumilia ulegelege wa serikali dhaifu na dhalimu kukaa na kuangalia maisha ya watanzania walalahoi wakifa pasipo sababu za msingi, kisa ni kulindana na ushakaji usiokuwa na tija kwa mustakabali wa taifa na maisha ya raia wasiokua na hatia.

Wao wakiugua hata mafua wanapanda ndege kwenda India, kwanini wasituboreshee na sisi angalau kuliko kutudharau na kutukejeli? Haikubaliki na haitokubalika madaktari wapewe stahili yao kama wanavyotaka, tofauti na hilo lazima kieleweke.

CHANZO CHA HABARI ni kutoka kwa doctor mmojawapo Mount Meru Hospital.
 
Ikumbukwe kua hule mgomo wa mara ya kwanza Arusha hawakushiriki kabisa
Mkuu siyo kweli; ma-dr wa Mt Meru waligoma ila walikuwa wanafika kazini na kusaini na baadhi ya huduma walikuwa wanazitoa...

Mfano mgonjwa mmoja walikuwa wanaweza kumhudumia kwa saa nzima au zaidi yaani watajizungusha wee wakati issue ni ya robo saa tu...
 
Wanasiasa kweli ni watu wa ajabu sana. Hivi Serikali haijui kwamba sisi (watanzania) ndio waajiri wao?
Yaan hawa watu wawili ni bora kuliko maisha ya watanzania? Au kuna picha kubwa zaidi ambayo mimi ninashindwa kuiona? Iwe na iwavyo lakin kwa mshikamano huu wa Madokta, hata wakiunganisha vitisho vya vyombo vyote vya DOLA hawatafanikiwa.

Kinachotakiwa si kutumia ubabe, bali busara, unyenyekevu, uwajibikaji na maelewano. Kama sivyo basi wategemee waajiri wao (wananchi) kuchukua hatua kwani hawa ndio wagonjwa watarajiwa na hawafurahishwi na hali ilivyo hata kidogo.

I support the Doctors
 
Mkuu siyo kweli; ma-dr wa Mt Meru waligoma ila walikuwa wanafika kazini na kusaini na baadhi ya huduma walikuwa wanazitoa...

Mfano mgonjwa mmoja walikuwa wanaweza kumhudumia kwa saa nzima au zaidi yaani watajizungusha wee wakati issue ni ya robo saa tu...

Sasa mkuu kama huduma zilikua zinatolewa utaita ni mgomo?mgomo una maanisha tools down kama walivyofanya sasa!
 
Tunisia, Misri na Libya zilianza vivi hivi. Madaktari leo mara kesho utasikia manesi kisha wafanyakazi wengine, lakini yoote tisa kama wale wajamaa wa vyuo vikuu wakiwaunga mkono basi ujue Tanzania itageuka jina na kuwa Tunisia. Tusiombe yafike huko. Mungu ibarki TANZANIA. MUNGU UILINDE TANZANIA.
 
Hivi ni kweli kwamba Dr Mponda ni shemeji yake na wakubwa hao na ndiyo maana wanamlinda mpaka kuhatirisha maisha ya watanzania kiasi hiki???:playball:
 
Binafsi nashindwa kuamini kama hawa madaktari wote niwendawazimu na wasio na utu. Kwautulivu mkubwa bila ushabiki wala ushawishitoka upande wowote, nimeliangalia hili swala kwa uhalisia wake ambao hata mimikama muhudhuriaji mahospitalini nimelinganisha mambo.

Kwanza chanzo cha mgogoro nahisi si ule mgomo wa Interns,ingawa wengi wanaamini hivyo. Najua ni kutowajibika kiufasaha kwa viongozi wetuwenye dhama juu ya mambo ya Afya. Ule mgomo wa Interns ni kiashiria kimojawapotu, maana swala lile lilishughulikiwa kisiasa na propaganda nyingi, binafsinilipata hasira na vijana wetu tunaowategemea wawe madaktari bingwa baadaye,ila baada ya kuibuka kwa ukweli juu ya jambo lile na kwamba walikuwa na madaiya msingi ambayo watu wachache tu waliamua wasijishughulishe. Pia nilipatwakichefuchefu baada ya kusikia maovu ya viongozi wenye dhamana wakitumiamadaraka yao kufanya ufisadi kwa kinga ya madaraka yao. Hili pia lilidhibitishwana Mh. Waziri Mkuu alipowasimamisha baadhi ya viongozi kwa kuwatuhumu baadhi yahayo tuliyoyasikia.

Ninakila sababu ya kudhibitisha kuwa Madaktari wanafanyakazi zao katika mazingira hatarishi sana. Napenda nitoe mfano mmoja, ambapoMezi Januari tulimpeleka mgonjwa wetu wa Kansa pale Hospitali ya Ocean Road,Dar es salaam. Mgonjwa alikuwa kwenye hali mbaya na alishapata vidonda vikubwavisivyotazamika bila ujasiri wa kutosha. Tulipofika pale tulipokelewa vizuri,tukapea kitanda. Ila kabla Daktari hajaanza kuzunguka kwa ukaguzi,tulitaarifiwa mapema na wauguzi wasaidizi kuwa ni muhimu tuwe na vifaa/dawa ilikuwezesha ukaguzi na matibabu. Kwasababu tulihitaji maelekezo ni vifaa ganihasa nilimuomba atuorodheshee, kweli nilishangaa hata gloves na dawa ya kusafishiakidonda ilibidi kununuliwa na mgonjwa pia. Basi kulikuwa hakuna cha kufanyaikabidi kwenda Posta Mpya kwenye Mapharmacy ili kutafuta vifaa/dawa hizo.Napenda kuwajulisha pia, kuna wagonjwa walishindwa kukaguliwa vizuri, iliwa nikugusa majeraha au hata kusafishwa kwa frequency inayotakiwa kutokana na kukosavifaa hivyo. Pia imeshakuwa ni kanuni sasa, kwa wamama wajawazito kutembea navifaa vyote hadi gloves pindi wanapokaribia kujifungua. Maana wanaweza patwauchungu wakiwa njiani/kwenye shughuli nyingine mbali na nyumani hivyokuwahishwa hospitali kwa kujifungua. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamab, hivi hizigloves na vifaa vingine anavyotembea navyo huyu mama vinakuwa salama (sterile)kama inavyohitajika. Maana anaweka tu kwenye kikapu na kuendelea na shughulizake zingine. Yapo mambo mengi na wengi wetu tunayajua ila si wakati wake sasa.Napenda kuwaambia wale wanaoshabikia propaganda za mgomo huu, waende wakajioneewenyewe mahospitalini.

Napenda kuishauri serikali, kwahili wasijiridhishe napropaganda tunazozisikia kwenye vyombo vya habari na hata humu jukwaani. Sisindiyo waathirika wakubwa na ukweli zaidi tunaujua sisi. Mara kadhaatumeshuhudia maafa ya wapendwa wetu kwa ukosefu wa vifaa vidogo tu ambavyo leohii tunasikia madaktari wakiomba kupatiwa. Hivyo tunaomba Busara itumike katikakulishughulikia swala hili, na si kutafuta nani mshindi. WOTE TUWEKE SIASAPEMBENI NA TUANGALIE UHALISIA. Swala la kuondolewa kwa Mawaziri wa Afya siSerikali kuonyesha udhaifu, bali ni kurudisha IMANI kwa Madaktari na sisiwananchi pia. Mara ya kwanza mgomo huu, tulitarajia taarifa yenye ufumbuzi wamatatizo ya msingi toka serikalini, lakini tulipomsikia Waziri husika Bungenikutuletea Ngonjera ya kuwa Dr. Ulimboka si Daktari, badala ya kutuambia kiinina utatuzi kwakweli hata sisi wengine Imani ilitutoka na kuona sasa swalalimehskuwa vuta nikuvute. Tunatarajia safari hii serikali itawajibika ipasavyona Tunawaomba madaktari mrudishe moyo ili muweze kutuhudumia. Wananchitusikubali kuingia kwenye mtego wa ama kuwachukia madaktari au KuichukiaSerikali. Natumaini bado serikali inawatu wa kuweza kulishughulikia jambo hilivizuri ipasavyo bila kukimbilia suluhu za jazba. Hatutapenda kuona nchiinaingia kwenye machafuko eti kwasababu ya vuta nikuvute katika sakata hili.Nasisitiza tusitafute MCHAWI bali tuzingatie uhalisia na uwezo wetu. MunguIbariki Tanzania
 
Jamani vipi amri ya mahakama haija wafikia bado?

Mahakama ipi hiyo mkuu, the Heag au ni hizi zinazomilikiwa na magamba. Kama ni the Heag hapo sawa lakini kama siyo basi mgomo ni mbele kwa mbele mpaka magamba yanyonyoke.
 
nadhani kwa huku arusha tutegemee utatuzi hivi karibuni,wanajua impact ya mgomo kwa uchaguzi
 
Jamani vipi amri ya mahakama haija wafikia bado?

Mahakama ipi hiyo mkuu, the Heag au ni hizi zinazomilikiwa na magamba. Kama ni the Heag hapo sawa lakini kama siyo basi mgomo ni mbele kwa mbele mpaka magamba yanyonyoke.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom