Moto waunguza majengo NIT

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
Moto mkubwa ulioanza alfajiri umeteketeza kabisa majengo mawili la Accounts na Store hapa chuo cha usafirishaji NIT Dar-es-salaam. Mpaka sasa chanzo hakijajulikana ingawa kuna kaharufu harufu kidogo ka hujuma kwa ajili ya kuficha madhambi yalikuwapo hapo chuoni kabla ya kuingia mkuu mpya aliyekuja wiki hii. Zimamoto kama kawaida walifika wakajitahidi mpaka maji yakawaishia haukuzimika, wakaenda kuchukua mengine mpaka jengo yakateketea kabisaaa.
 
Poleni sana marehemu, Mungu aziweke roho zenu mahala pema peponi. Amina
NB. Kama ulikuwa mtenda dhambi basi sahau juu ya kuingizwa peponi.
 
Chamba cha nyaraka za uhasibu cha chuo cha usafirishaji kiunguzwa moto usiku wa kuamukia leo kufuatia tuhuma za ufisadi zinazo waakabili ( eliezermsonge mkurugenzi wa fedha, mkuu wa chuo elifadhili mgonha na hussen senzige) ambapo wote wameshahojiwa na pccb kwa hatua za mwisho za kupelekwa mahakamani!


Tukio la kuunguza ofisi limekuja mda mfupi wakati serikali imepeleka mabadiliko ya uongozi ambapo imepeleka mkuu mpya wa chuo.!!!

Bw eliezer msonge aliwelwa na mh philimon luhanjo na katika cv yake luhanjo ana appear kama referee.


Mwaka 2008 wakati tuhuma hizo zinatawala hapo kuna mfanyakazi anayeitwa mariam alinyofoa nyaraka za wizi na kuzipeleka ikulu, na zilipo fika huko, luhanjo akaziona na kuzirudisha kwa ndugu yake msonge na kuagiza amufukuze maramoja na mariamu akafukuzwa hadi sasa!!.
 
Poleni sana marehemu, Mungu aziweke roho zenu mahala pema peponi. Amina
NB. Kama ulikuwa mtenda dhambi basi sahau juu ya kuingizwa peponi.
Mwita, hawajafa watu bali ni mali za umma na documents ndizo zimeteketea.
 
Poleni sana marehemu, Mungu aziweke roho zenu mahala pema peponi. Amina
NB. Kama ulikuwa mtenda dhambi basi sahau juu ya kuingizwa peponi.

kah mkuu kwani kuna taarifa za kifo?? At unatanguliza kabisa just incase....hahaha
 
Mwita una uhakika huyo ndyoko ni mrembo? Unaijua jinsia yake lakini?
 
Tangu mwaka 2008, kumekuwepo na tuhuma za ufisadi chuo cha Usafirishaji (NIT) ambapo miradi yake mingi ilikiuka sheria za manunuzi na kupelekea maliza umma kuibiwa .

Tuhuma zilihusu Jeshi la Magereza ambapo mlengwa mkuu alikuwa PCP Augustino Nanyoro ambaye alihusishwa na wizi wa zaidi ya Tshs 600,000,000/= kupitia Kampuni ya GONDO ENTERPRISE ya ndugu yake iliyopo BUGURUNI.

Baadhi ya wafanyakazi kitengo cha uhasibu waliamua kupeleka nyaraka za uhalifu huo Ikulu DSM, Lakini siri hizo ziliwarudia mafisadi kama ifutavyo.
Mtuhumiwa namba moja ni ELIEZER MSONGE (MKURUNGENZI WA UTAWALA NA FEDHA) NI MTU WA KARIBU Na PHILIMON LUHANJO-IKULU DSM.Baada ya Luhanjo kupokea tuhuma zinazomkabili jamaa akaamua kumurejeshea taarifa hizo za siri huku akisisitiza aliyetoa siri hizo afukuzwe kazi mara moja!!!!

Mpango huo ulifanyika haraka na yule msamalia mwema akafukuzwa kama mbwa kwa amri ya Philimon Luhanjo ili kulinda wizi hadi leo.Eliezer Msonge alimuweka hawala yake aitwaye Bi . DEBORA kwenye kitengo cha manunuzi wakati anajua hana sifa ,lakini kwa kuwa ni hawala yake na wote wanapora mali ya umma pamoja.

Juhudi za wapambanaji zimefanyika kwa kasi kubwa mpaka tarehe 3/11/2011 ambapo serikali iliamua kufanya mabadiliko ghafla ya kuweka Mkuu wa Chuo Mpya Ndg MHALAGWA . Baada ya hapo ,Mtandao wa Philimon Luhanjo uliamua kufanya Njama za kulipua ofisi ya Uhaibu tarehe 4/11/2011 ili kupoteza Ushahidi.
Tukio hili linafanyika wakati kaimu mkuu wa chuo (ELIFADHILI MGONJA)ametorokea Zambia !!!

Hadi naandika post hii kuna kikao kizito kinaendelea Chuoni hapo .
Nimeambatanisha Nyaraka za ushahidi wa Ufisadi huo hapa chini






 

Attachments

  • NIT -2.pdf
    2 MB · Views: 181
Kaazi kweli kweli,,, mtandao wa ufisadi... Mama angekoleza zaidi kama angeweka na vocha au hundi walizolipwa hao watu!!!
 
Ukombozi wa pili hauepukiki kabisaaa...Tanganyika wachumia tumbo wanazaliana kwa haraka kama bakteria ndani ya mwili wa mwanadamu
 
Moto mkubwa ulioanza alfajiri umeteketeza kabisa majengo mawili la Accounts na Store hapa chuo cha usafirishaji NIT Dar-es-salaam. Mpaka sasa chanzo hakijajulikana ingawa kunDuh hii nomaa kaharufu harufu kidogo ka hujuma kwa ajili ya kuficha madhambi yalikuwapo hapo chuoni kabla ya kuingia mkuu mpya aliyekuja wiki hii. Zimamoto kama kawaida walifika wakajitahidi mpaka maji yakawaishia haukuzimika, wakaenda kuchukua mengine mpaka jengo yakateketea kabisaaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom