Moto waunguza bweni chuo cha Kilimo (MTWARA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto waunguza bweni chuo cha Kilimo (MTWARA)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mcubic, Oct 3, 2012.

 1. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 9,658
  Likes Received: 3,474
  Trophy Points: 280
  Kumetokea ajali ya moto katika chuo cha kilimo Mtwara(MATI-Mtwara). Moto huo umetokea majira ya saa tatu asubuhi leo hii, Umeunguza bweni la wasichana linalochukua takribani watu 70. Chanzo cha moto huo inasemekana kuwa ni hitilafu ya umeme katika mo ya chumba kilichopo kwenye bweni hilo. Vyanzo vimezidi kueleza hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa wanafunzi hao zaidi ya kuunguliwa na vitu vyao pamoja na magodoro yao ya kulalia. Polisi walifika chuoni hapo na kuchukua maelezo kwa mkuu wa chuo hicho ndugu Waziri mwinyi. Kikosi cha kuzima moto kilishindwa kupeleka gari chuoni hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ubovu wa gari lao, hivyo kulazimika kutumika gari la kuzima moto la bandari. Chuo cha kilimo Mtwara kipo kama kilomita kumi na nne kutoka mtwara Mjini, kinatoa kozi za kilimo kwa Ngazi ya cheti na Astashahada.
   
Loading...