Moto wateketeza nyumba ya mchungaji Tabora

Moto wateketeza nyumba ya mchungaji Tabora

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Moto umezuka na kuteketeza nyumba yenye vyumba tisa ambayo anaishi mmoja kati ya wachungaji wa iliyotokea usiku wa jana Jumatano, Agosti 20, 2025, hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini mali mbalimbali zilizokuwamo zimeteketea.

Mchungaji Amosi Chidemi ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo amesema saa moja usiku wakati akiwa sebuleni na familia yake wakaona moshi unajaa ndani na baada ya kwenda kuangalia unapotokea moshi wakaona moto tayari umeshatanda katika baadhi ya vyumba.

Soma pia: Marekani: Polisi inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kusababisha moto mkali uliochoma nyumba zaidi ya 10,000 na kuua watu 10

Screenshot 2025-08-21 000910.png

Amesema yeye pamoja na familia yake wametoka salama lakini hajui nini ambacho kimeokolewa mpaka kwani majirani walianza uokoaji wakati tayari moto umeshakuwa mkubwa.

“Wakati tumekaa sebuleni, tumemaliza kula chakula tukawa tunaongea, tukashangaa moshi unaingia sebuleni.

Nikatoka ili niangalie moshi unatoka wapi ndio nikakuta ile pazia ya kwenye korido ndio imeshatanda moto ukiwa ni mkali kabisa, mke wangu akanivuta kwamba tutoke nje kupitia mlango mwingine, ndio tukanusurika wote," amesema.
 
Uchunguzi ufanyike huenda wasiopenda huduma yake wametaka Kumuua kwa kuchoma nyumba yake
 
Pole sana mtumishi,hongera pia kwa kuchagua mke mwema,maana ingekuwa hawa UKIFA UTANIACHIA NINI saa hizi tungekuwa tunaongea mengine...
 
Back
Top Bottom