Moto wateketeza kituo cha yatima Monduli

Moto wateketeza kituo cha yatima Monduli

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Moto wateketeza kituo cha yatima Monduli. Watu kadhaa wakiwemo watoto wamenusurika kifo baada ya moto kuwaka na kuteketeza zaidi ya gunia sitini za Mahindi ya chakula mashine tatu za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na vifaa vingine katika kutuo cha kulelea watoto yatima na wazee wasiyojiweza cha amana Chidren home kilichopo kata ya Esirarei wilaya ya Monduli.

Mlezi wa kituo hicho cha kulelea watoto cha Amana Chridren home Steven Kimbi anasema tukio hilo limetokea majira ya saa tano usiku wamejitahidi kuuzima lakini ilichukua muda mrefu kwakuwa walikuwa wanatumia maji ya kuchota kwa ndoo hivyo chakula kilichowemo kwenye ghala chote kimeteketea mashine za kuzaga za kituo zimeteketea na hakuna mtu alipata madhara kwenye tukio hilo.

Wahudumu wanaishi ndani ya kituo hicho wakaeleza mazingira ya moto huo ulivvyotokea na kwamba umesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni themanini. Baadhi ya viongozi wa mtaa uliyotokea tukio ilo wameomba wasamariwema kujitolea kuwasaidia wazee na watoto wanaolelewa kituo kituoni hapo.


ITV
 
Mlezi wa kituo hicho cha kulelea watoto cha Amana Chridren home Steven Kimbi anasema tukio hilo limetokea majira ya saa tano usiku wamejitahidi kuuzima lakini ilichukua muda mrefu kwakuwa walikuwa wanatumia maji ya kuchota kwa ndoo hivyo chakula kilichowemo kwenye ghala chote kimeteketea mashine za kuzaga za kituo zimeteketea na hakuna mtu alipata madhara kwenye tukio hilo.


Poleni sana wahanga, je kile kikosi kilichotetewa kwenye tukio la ajali Sangasanga Morogoro baada ya Fuso na gari aina ya Man kugongana uso kwa uso majuzi usiku hakipo huko?
 
Na hali ya uchumi ilivyobana gunia sitin si mchezo polen sana sana
 
Back
Top Bottom