Motivational quotes

Screenshot_20211215-061641.jpg
 
Biology inasema baada ya tendo la ndoa mbegu za kiume zinazoingia kwa mwanamke ni zaidi ya million 300, zote huanza kuogelea kwenda kwenye ovuli(yai), kati ya mbegu hizo zote mbegu 500 tu ndo zinazofanikiwa kulikuta yai, mbegu zingine huchoka na kufa njiani, na katika mbegu hizo 500 ni mbegu 1 tu hufanikiwa kuingia kwenye yai na kutengeneza kiumbe, mbegu hiyo ni wewe unaesoma huu ujumbe.

Biology inasema uliwashinda wenzako zaidi ya million 300 ndio maana leo upo hai, usingewashinda usingezaliwa

Je umewahi kufikiria juu ya hili, ulikimbia bila miguu, mikono wala macho ukashinda, ulikimbia bila ujuzi, elimu wala vyeti ukashinda, ulikimbia bila msaada wa yeyote ukashinda

Ni kitu gani leo cha kukufanya uwaze kushindwa na kukata tamaa??, leo una macho, mikono, miguu, elimu, ujuzi na maarifa, zaidi unaongozwa na maneno ya mwenyezi mungu.

Ulipowashinda wenzako zaidi ya millioni 300 ina maana wewe ni mshindi, ushindi wako una sababu kubwa, kwa nini ushindwe na wengine leo kwanini ushindwe na maisha leo?? Kwanini uwe mtumwa wa mtu mwingine, you are the champion

Weka malengo, pambana, muombe mungu ulizaliwa ukiwa mshindi usikubali kushindwa wewe ni shujaa


Tone la maarifaView attachment 2017020

Hii nayo ni motivational quotes
 
Back
Top Bottom