Motisha na nguvu

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
7,580
Reaction score
13,048
Safari ya maili elfu huanza na hatua moja. Usiogope ukubwa wa ndoto yako; ogopa tu kutochukua hatua ya kwanza. Anza leo, hata kama ni kwa udogo.

Usilinganishe sura yako ya kwanza na sura ya ishirini ya mtu mwingine. Kila mtu anasafari yake. Endelea kuandika hadidhi yako kwa uvumilivu. Wakati wako unakuja. Kizuizi kikubwa kati yako na mafanikio yako sio watu wengine, sio mazingira, ni sauti ndogo ndani ya kichwa chako inayosema `Siwezi'.

Nyamazisha sauti hiyo kwa vitendo. Jana ni historia, kesho ni fumbo. Leo ni zawadi. Ndio maana inaitwa `Present' (Zawadi). Itumie vizuri zawadi yako ya leo, kwa maana ndiyo pekee uliyonayo... Mjusi na tafakari.
 
Mi nauza magimbi nataka kuwa tajir wa dunia umr wangu miaka 48 !!
Bado hujachelewa. Cha muhimu yafanye magimbi kuwa fursa, na siyo magimbi yakufanye fursa kwa wengine. Nikiwa na maana ya kwamba, jiwekee nidhamu ya pesa. Siyo umeuza magimbi kidogo tu unakimbilia starehe na malaya, huko ni kutajirisha wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…