Mother house punguza vibomu

Mother house punguza vibomu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Hapa kwenye nyumba Huku kwetu Kwamtogole tupo wapangaji nane. Watano vyumba vya ndani na watatu vyumba vya uani. Nyumba ina maji na umeme na iko karibu na barara kubwa. Mama mwenye nyumba anaishi katika moja ya vyumba vya ndani.

Huyu mama anaomba kuanzia mchuzi mpaka vitafunio vya chai. Akijua unapika kuku ataleta bakuli. Huwa hapendi wale wapangaji wa kula mboga za majani. Ukiwa wa bamia na matembele kamwe hutaona bakuli lake.

Vituko vimehamia kwenye manukato na pochi. Anakuja kukutembelea chumbani akiona perfume nzuri hiyo imetoka. Siku hizi ameanza kuazima pochi akienda shughulini. Kama ni pochi ya jina kubwa isahau tena.

Mama tumekuchoka wapangaji wako.
 
Hahaha besti unanikumbusha mbali sana kwenye nyumba za kupanga Chuga na zilivyodizainiwa U au L. Umbea uliokithiri, kupigana juju, mashindano ya kijingajinga yani ukioga mchana unaulizwa unakwenda wapi?

Ukiwa na kauwezo mwenye nyumba anakupapatikia na kukushobokea

Ila ukiwa na nyumba yako una amani. Sisi waswahili tukichanganyikana ni hatariii
 
Best hizi nyumba zetu mipango inatazamana. Watoto wa mjini wanaita ‘Face me I face you’ hayo ya umbea tena tumezoea ukiwa na danga bora ulipeleke guest. Hapa home utahesabiwa hata usiowakumbuka.
 
Ila wanawake ndiyo mpo hivyo katika kuazimana vitu
 
Hapa kwenye nyumba Huku kwetu Kwamtogole tupo wapangaji nane. Watano vyumba vya ndani na watatu vyumba vya uani. Nyumba ina maji na umeme na iko karibu na barara kubwa. Mama mwenye nyumba anaishi katika moja ya vyumba vya ndani.

Huyu mama anaomba kuanzia mchuzi mpaka vitafunio vya chai. Alikua unapika kuku ataleta bakuli. Huwa hapendi wale wapangaji wa kula mboga za majani. Ukiwa wa bamia na matembele kamwe hutaona bakuli lake.

Vituko vimehamia kwenye manukato na pochi. Anakuja kukutembelea chumbani akiona perfume nzuri hiyo imetoa. Siku hizi ameanza kuazima pochi akienda shughulini. Kama ni pochi ya jina kubwa isahau tena.

Mama tumekuchoka wapangaji wako.
Nilikwambia mlishe kitimoto siku moja ukabisha. Akila kitimoto pepo/jini la kupiga vibomu litamtoka...
 
mama wa namna hiyo hapa sidhan kua yupo, tafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe
 
Dah! Mkalisheni chini, mpeni kero zenu kama ni mtu muelewa ataacha hiyo tabia. Lakini wakati mnamweleza mjiandae kuulizia vyumba sehemu zingine, ili akiwatimua iwe msiumize kichwa
 
Nawe si ndio anakurahisishia siku hujapata kodi yake unamwambia "shoga mambo bado kidogo"
 
MAZA HOUSE ACHA KUKERA WAPANGAJI WAKO

message sent n delivered!!
 
Hahaha besti unanikumbusha mbali sana kwenye nyumba za kupanga Chuga na zilivyodizainiwa U au L. Umbea uliokithiri, kupigana juju, mashindano ya kijingajinga yani ukioga mchana unaulizwa unakwenda wapi?

Ukiwa na kauwezo mwenye nyumba anakupapatikia na kukushobokea

Ila ukiwa na nyumba yako una amani. Sisi waswahili tukichanganyikana ni hatariii
Kumbe hayo mambo yapo hadi mikoani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom