Mosi, Naomba tunapokuwa Tunaendelea kuchangia kuwa Tundu Lisu anachokifanya huko nje ni sawa au si Sawa tupate nafasi ya kujua kafika vipi huko

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,249
2,000
*Tundu Lisu Kupigwa Risasi Sio Swala La Uchama*

Baada ya kuona post

Maana pasipo kujua chanzo cha tatizo Huwezi Kutatua Tatizo,

Ni lazima tujue, Ukiwa Na Kiongozi wa Ngazi Yeyote Awe Rais, Mbunge au Diwani Katika Eneo lake La Nchi , Jimbo au Kata kukawa Na vifo vingi vya malaria au typhoid lakini Kiongozi huyo badala ya kushughulikia kuondoa/ kupambana Na Mbu ili kuondoa maralia au kuhakikisha analeta maji safi ili kupambana Na typhoid yeye akawa analeta vidonge vingi watu wanywe Mtu huyo hafai kuwa Kiongozi, Maana kila siku watu watazidi kuugua Na vifo havitakoma.

#Pili, Hoja ya msingi ni Tundu Lisu kupigwa Risasi, je Ni Sawa Mtu kupigwa Risasi ??
Naomba Nikumbushe Kwetu Sisi Tanzania Sheria Yetu Mama ni Katiba Kwa Ufupi sisi kama Nchi Tunaunganishwa Na tunaongozwa Na Katika
kwa mjibu wa katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania 🇹🇿 ya mwaka 1977 hakuna ibara ,wala ibara ndogo ya Katiba inayoonyesha Mtu Aliyekosea kosa lolote Apigwe Risasi Ibara Hiyo Haipo. Kwa Hiyo Lisu Hata Kama Angekuwa Ana kosa la aina yeyote (kama lipo) Hakutakiwa Kupigwa Risasi hiyo ndo hoja ya msingi.

#Tatu, Kwa mjibu wa sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 imesema kuwa ni kosa kupanga njama za kumsababishia mtu maumivu au kuua , Hivyo haijalishi mpango huo muovu umepangwa Na nani hoja ni kuwa hairuhusiwi kupanga njama za kuua, maana pia katiba yetu ibara ya 13 imesema watu wote sisi ni sawa vile vile hakuna atakae kuwa juu ya sheria,

#Nne, Sisi kama watanzani bila kujali Vyama vyetu wala kujali kabila au dini ni lazima tujue mtu au watu kupanga njama za kumuua mtu ni kosa kisheria, tukishaelewana hapo ndo tuchangie mjadara maana tukiruhusu Na kuona mtu kuuwawa ni sawa kisa ni mtu wa chama ambacho wewe hukipendi #TUTAANGAMIA

#Mwisho, Kwa Mjibu Wa Sheria zetu polisi wanawajibu wa kuchunguza Na kuwabaini watu wote waliohusika Na tukio lile Na wafikishwe mahakamani Na mahakama wakijiridhisha bila kuacha Shaka kuwa watu hao waliopelekwa Ndio waliohusika Na tukio hilo watapewa adhabu yao kwa mjibu wa sheria,
Ukiona mambo haya hayajafanyika weka akirini tafakari je nchi yetu bado inaongozwa kwa mjibu wa Katiba Na sheria?????????
#Nitarudi

Mwanahabari Huru
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,022
2,000
Mkuu alishasema Katiba inatuchelewesha!! Kwenda wapi? Kufanya nini? Anajua yeye! Pia alishasema Tupo vitani!!! Na kama tuko vitani na mmoja wetu akaanza kuhoji hivi au vile basi mtu huyo anatakiwa apigwe risasi maana ni Msaliti! Grasp that!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom