Moshi: Wahukumiwa kifungo miaka 90 jela

Moshi: Wahukumiwa kifungo miaka 90 jela

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Raia wa Poland, Damian Krzystztof na mkewe Eliwaza Pyuza walikuwa wakijihusisha na kilimo cha bangi wamehukumiwa jela miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kulima na kusafirisha bangi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 9,2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Moshi, Bernazitha Maziku huku mke wa raia huyo wa Poland na Watanzania wengine wawili wakipigwa faini ya Sh4 milioni kila mmoja kwa kuvuta bangi.

Katika hukumu hiyo, Hakimu amesema ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi 11 wa upande wa mashitaka, umejitosheleza na kwamba raia huyo wa Poland na mkewe watatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kila kosa kwa makosa matatu waliyoyatenda ya kulima na kusafirisha bangi.

Hata hivyo, Hakimu alisema kwa kuwa adhabu hizo zitatumikiwa kwa pamoja hivyo watatumikia kifungo cha miaka 30 jela badala ya miaka 90.

Hakimu huyo amesema ushahidi wa mashahidi 11 wa upande wa mashitaka waliongozwa na waendesha mashitaka wa Serikali, Ignas Mwinuka, Verdiana Mlenza na Lilian Kowero ulijitosheleza na ulikuwa madhubuti.

Amesema Eliwaza na mfanyabiashara wa malori, Hanif Kanan na fundi pikipiki Boniface Kessy wamepatikana na hatia kosa la kuvuta bangi hivyo watatakiwa kulipa faini ya Sh4 milioni kila mmoja au kifungo cha miaka mitatu jela.

Hakimu huyo aliwaachia Hanif na Boniface katika makosa ya kulima na kusafirisha bangi akisema upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.

Hata hivyo, hata kama mshitakiwa, Hanif atafanikiwa kulipa faini hiyo, bado ataendelea kushikiliwa mahabusu na mshitakiwa Damian na mkewe kwa kuwa wanakabiliwa na kesi nyingine inayoangukia makosa ya uhujumu uchumi.

Awali wakili Mwinuka kutoka ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS), aliiomba mahakama itaifishe mali za mshitakiwa wa kwanza na wa pili ambao ni mume na mke, ombi ambalo Hakimu Mkazi, Bernazitha alilikubali na kutoa amri hiyo.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 8 mwaka jana.
 
Nadhani sasa Mama wamshauri aturudishe vijana shamba, Bangi iruhusiwe kulimwa kibiashara. Hata uvutaji mitaani utapungua kwa kiasi kikubwa mnooo!

Kwa mfano wakikubali Mmea ulimwe, Watawaachia wote waliohukumiwa kwa kosa hilo!? Nawaza.
 
Hukumu kwa watumiaji bangi mbona hazina usawa,chid benzi alikuwa mtumia cocaine ila hakufungwa,hao jamaa wametumia bangi wamehukumiwa miaka 3 au kulipa faini.mbona sielewi sheria zetu zikoje
 
Kwanini Bangi isilimwe kibiashara?japokuwa fursa zinafunguka huko duniani bado viongozi wetu wanajitia upofu, tumbaku inalimwa ila bangi NO
 
Hawa walikamatwa lini?
Mbona mnamsema mama yetu.
Embu tuacheni. Hawa hawahusiki na maneno ya mama
 
Back
Top Bottom