Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,627
Vilio, simanzi na majonzi vilitawala vimetawala wakati mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akiongoza maziko ya aliyekuwa ofisa habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Hamza Temba yaliyofanyika Isawerwa kata ya Masama wilayani Hai.
Hamza alifariki juzi katika ajali ya gari iliyotokea Magugu mkoani Manyara ikiwahusisha watu wengine watano, akiwamo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyepata majeraha mbalimbali mwilini.
Pia, maziko hayo yalihudhuriwa na naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Aloyce Nzuki. Akitoa salamu za rambirambi, Dk Nzuki alisema Hamza alikuwa akitegemewa na wizara kwa kuwa alikuwa akifanya kazi zake kwa weledi na kujituma.
Naye Mghwira alisema Hamza alikuwa kijana mcheshi mpambanaji, akijitambua na mwenye mtazamo wa mbali.
“Vijana igeni mfano wa Hamza, alikuwa ni kijana mdogo lakini kimtazamo alionyesha wazi kuwa angefika mbali,” alisema. Aliahidi kuwa karibu na familia ya marehemu kwa jambo lolote litakalojitokeza kwa kuwa Hamza ameacha mke na mtoto mdogo.
Katibu wa Baraza la Wanazuoni la Mudio Islamic, Othman Mtavangu aliwataka vijana kujituma na kuenzi mazuri yaliyofanywa na Hamza.
“Igeni mfano wake maana amefia kazini wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi ya kuwatumikia Watanzania, ila vijana wa leo wanaishia katika kamari,” alisema.
Watu wa kada mbalimbali walizungumzia mema yaliyofanywa na Hamzahuku mkewe, Zainab Ally akipoteza fahamu kwa majonzi. Hamza ameacha mke na mtoto mmoja mwenye miaka mitatu.