Kwa hili nasema kwa sauti kuu kwamba wengi wa mapadre ni watu wanaoendesha maisha kiintelejensia kuliko kiimani. Wanafanya mambo kwa kifichi sana kwa hofu ya wanadamu kuliko wanavyomwogopa Mungu. Ndio maana visa vingi vilivyowekwa wazi vya mahusiano ya kingono ya mapadre ni mwingiliano wa kinyume na maumbile tena baya zaidi ni kwa wanaume wenzao. Haya hayakutokea kwa bahati mbaya bali yanalenga mkakati wao wa kukwepa matokeo kama ya ujauzito ili wasiwe wazi kwa jamii wanayoidanganya kwamba wao ni ma-cluny. Hakuna mahali hata pamoja katika biblia yao panapodai kutokuoa au kuolewa kama sharti la kumtumikia Mungu. Ila wao sasa kwa sababu wameamua kumtii mtu zaidi ya Mungu, wanalazimika kutokuoa kama sharti kuu la kusimikwa kuwa padre. Sasa hili ni kinyume na asili na ni kinyume na sharti la mtu kuwa askofu ama shemasi katika biblia kwani inamtaka awe ni mume wa mke mmoja. Mwenye kuweza kuitunza nyumba yake mwenyewe kabla ya kukabithiwa kanisa. Sasa padre hana nyumba hana mtoto uchungu wa mwana ataupata wapi? No wander fahamu zao zimekufa na hawawezi kutofautisha matumizi ya mke na mme na wala watoto hawana dhamani yeyote kwao. Huu ni wakati muafaka wa kanisa katilic kurejelea misingi ya asili ya binadamu na kuyafurahia maisha ya ndoa na watoto wao wenyewe kama Mungu alivyoagiza katika kitabu kitakatifu, Mwanzo 2:18-25.