Mosha wa CCM apongeza ushindi wa CHADEMA Moshi

Mosha wa CCM apongeza ushindi wa CHADEMA Moshi

concrete15

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
882
Reaction score
323
Umeonyesha ukomavu wa siasa kiongozi big up tuijenge Moshi pamoja. Unapaswa kuigwa
Mosha wa CCM apongeza ushindi wa CHADEMA Moshi

Kwa ufupi
-Juzi saa 4.26 usiku, Mosha alimtumia Michael ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), akimpongeza kwa ushindi wa kishindo, kitendo ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya jimbo hilo.

Aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha amempongeza mpinzani wake, Jaffar Michael wa Chadema kwa kupata ushindi wa kishindo.

Michael aliibuka na ushindi wa kura 51,646 dhidi ya kura 26,920 alizopata Mosha, na hivyo kumfanya Michael aliyekuwa Meya wa Mji wa Moshi kutangazwa mshindi.


Juzi saa 4.26 usiku, Mosha alimtumia Michael ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), akimpongeza kwa ushindi wa kishindo, kitendo ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya jimbo hilo.


"Japhary Michael nachukua nafasi hii kukupongeza kwa ushindi wa kishindo katika nafasi ya ubunge wa Jimbo la Moshi," alisema Mosha ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara matajiri nchini.


"Najua kuna sehemu tulikwaruzana ama kuhitilafiana kwa maneno. Hiyo ilikuwa siasa si ugomvi, binafsi nisamehe na Mungu akubariki. Kama utahitaji msaada wowote tafadhali tuwasiliane," alisema.


Akizungumza na gazeti hili jana, Michael alimpongeza Mosha kwa kile alichosema ni ukomavu wa kisiasa aliouonyesha kwa kukubali matokeo.


Mbunge huyo mteule alisema alichokifanya Mosha ni nadra kwenye siasa za CCM katika Jimbo la Moshi Mjini.


Alitoa rai kwa wakazi wa jimbo hilo kufuta tofauti zao za kisisa baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili waanze kazi ya kuijenga Moshi mpya kwa maendeleo yao na ya Taifa.


Mkoa wa Kilimanjaro, umevunja rekodi ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 baada ya upinzani kunyakua majimbo saba kati ya majimbo tisa, huku .


Mwaka 1995, upinzani ulinyakua majimbo sita ya Hai, Siha, Rombo, Moshi Vijijini, Moshi mjini na Vunjo na kuiachia CCM majimbo ya Mwanga, Same Mashariki na Magharibi.


Mwaka 2000 na 2010, CCM ikafanikiwa kukomboa majimbo ya Siha na Moshi Vijijini.
Uchaguzi wa 2015, majimbo hayo yameangukia tena mikononi mwa upinzani.


Mbali na majimbo hayo, katika historia ya vyama vingi, safari hii upinzani umejipenyeza katika jimbo la Same Mashariki ambalo lilikuwa ngome ya CCM na kuwa miongoni mwa majimbo ya upinzani.
Majimbo ambayo sasa yanashikiliwa na upinzani ni Hai, Siha, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Vunjo, Rombo na Same Mashariki huku CCM ikibaki na majimbo mawili ya Mwanga na Same Magharibi.


C
hanzo: Mwananchi
 
Umafia ukishindikana inabidi kunywea. Tofauti ya kura elfu 30 angeponea wapi. Kasababisha hadi vijana kupigwa mabomu
 
Umeonyesha ukomavu wa siasa kiongozi big up tuijenge Moshi pamoja. Unapaswa kuigwa

Ngoja 'VUVUZELA WA CCM' waibuke kama alivyoibuka MZEE MAKAMBA MWAKA 2010 na kuwataka wale wote walioshindwa uchaguzi ndani ya CCM wakate rufaa haraka sana.
 
Umafia ukishindikana inabidi kunywea. Tofauti ya kura elfu 30 angeponea wapi. Kasababisha hadi vijana kupigwa mabomu

wenzenu wakiongoza wameiba nyie mkiongoza halali akil zingine bhana
 
ahamie tu ukawa kama yeye ni wa ukweli
 
Kama kuna uchaguzi ambao utakuwa na mapingamizi mengi mahakamani basi ni wa mwaka huu,
 
Mzee Wasira ana la kujifunza hapa

kwa mujibu wa makongoro nyerere, tangu ameanza shule ya msingi yule Mzee alikuwa anamuona katika serikali ya baba yake na akaendelea kumuona mpaka Siku alipotangaza kugombea urais wa tanzania, lakini amekosa mpaka ubunge.
 
wenzenu wakiongoza wameiba nyie mkiongoza halali akil zingine bhana

Niambie jimbo moja tu ambalo mabomu yalisharindima na akatangazwa mshindi ni ccm. Ubungo hadi vijana wamelazwa selo wakipigania matokeo ya kiongozi waliyemchagua
 
Niambie jimbo moja tu ambalo mabomu yalisharindima na akatangazwa mshindi ni ccm. Ubungo hadi vijana wamelazwa selo wakipigania matokeo ya kiongozi waliyemchagua

usihame hoja umempongeza aliyekubal matokeo ndo nikasema kwenu sawa kwa wenzenu si sawa
 
Jamaa si kapoteza hela nyingi sana

yahaya anadai watu wote aliowapa hela na pikipiki wamrudishie au patachimbika.....pia asisahau za mjinga huwa hazirudishwi mana jamaa kawatesa sana wa2 wakati wa kampeni kuwaweka lockup n mabausa wake kuwapiga wa2 hovyo kisa wanashabikia ukawa
 
ukomavu wa kisiasa big up mosha, business mogul
 
yahaya anadai watu wote aliowapa hela na pikipiki wamrudishie au patachimbika.....pia asisahau za mjinga huwa hazirudishwi mana jamaa kawatesa sana wa2 wakati wa kampeni kuwaweka lockup n mabausa wake kuwapiga wa2 hovyo kisa wanashabikia ukawa

Hahahaha yahaya unaishi wapiii?
 
Mosha ni kama kaingia ghafla uchaguzini.nadhani ni chini ya miezi sita tu.lakini akijijenga vizuri akajulikana vema 2020 atashinda.jimbo la moshi linahitaji mijitu aina ya Ndesamburo au Mosha.ukiondoa kua na halmashauri ilio imara,kiwango cha umasikini na ukosefu wa ajira ni vile vile
 
Back
Top Bottom