Moses Machali: Je, Zitto ni mbadhirifu ktk kile kinachoitwa ubadhirifu wa trilioni 1.5?

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
JE, ZITTO NI MBADHIRIFU KTK KILE KINACHOITWA UBADHIRIFU WA TRILIONI 1.5?
Na Moses Machali
21/04/2018

Ubadhirifu ni nini?
Kwa Mujibu wa Kamusi ya Maana ya Matumizi (Bakhressa Salim K, 1992) katika Ukurasa wa 400 neno Ubadhilifu lina maana ya : “Utumiaji mbaya wa kitu, mali; Ufujaji; Uhulikaji” huku TUKI (2001; Uk. 331)katika Kamusi ya Kiswahili – Kiingereza neno UBADHILIFU lina maana ya “Misappropriation, Embezzlement.” Dhana ya embezzlement katika kamusi ya kiingereza iitwayo RANDOM HOUSE WEBSTER’S COLLEGE DICTIONARY iliyochapishwa mwaka 1997, katika ukurasa wa 426 inaelezwa kwamba Embezzle means “to appropriate fraudulently to one’s own use, as money entrusted to one’s care.” Kwa ujumla neno Ubadhilifu ni wizi au utumiaji wa kitu vibaya.

Baada ya ripoti za CAG kuwekwa hadharani kumeibuka mjadala mkali sana kuhusu SH TRILIONI 1.5. Mjadala huo umesababisha taharuki miongoni mwetu watanzania. Mmoja wa watu walioshikia Bango suala hilo ni Mhe. Kabwe Zuberi Ryagwa Zitto, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ambaye katika Ukurasa wake wa Facebook amekuwa akiutumia kwa kuandika statement mbalimbali kuhusu issue hiyo y sh trilioni 1.5. Kwa mfano Tarehe 18/04/2018 saa 12:23 pm aliandika kwamba:
“Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.

Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.
Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa).
Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie”

Katika aya ya mwisho ya andiko lake anasema kwamba yupo tayari kukamatwa na wala hilo halitafuta ukweli wa Ubadhirifu huo. Hiyo ndiyo kusema kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhilifu na wenye mamlaka ya kuzisimamia kimatumizi, au zimefujwa na wenye mamlaka ya kuzisimamia kimatumizi.

Mhe. Zitto huyohuyo, mnamo tarehe 20/04/2018 akaandika tena facebook kwamba:
“Serikali Inasema Uongo, Ni Muhimu Bunge Lichunguze Ziliko 1.5 Trilioni
-Taarifa Ndogo ya ACT Wazalendo Juu ya Majibu ya Serikali Bungeni Juu ya Ziliko 1.5 Trilioni Zisizoonekana Matumizi yake Kwenye Ripoti ya CAG
Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu.”

Hiyo ina maana kwamba Zitto hajui na au hana uhakika wa mahala fedha zilipo na wala hajui zimefanyiwa kitu gani na hivyo anaomba au anataka Bunge Lichunguze ili kupata uhakika wa matumizi ya fedha hizo.
Mtu Makini anapokutana na statement hizo mbili tofauti lazima atasema kwamba Zitto ana tatizo la UBADHIRIFU wa Kifikra yaani anatumia utashi wake vibaya kwa maslahi yake binafsi na inaweza kuwa ya kisiasa au ya kiuchumi kwa sababu mwanzoni kabisaa tarehe 18 APRIL 2018 alisema kwamba ‘….yuko tayari kukamatwa na kwamba fedha hizo zimefanyiwa Ubadhirifu yaani wizi au matumizi mabaya. Ieleweke kwamba Matumizi mabaya inaweza kuwa zimeibiwa kwa ajili ya mtu binafsi au zimefanya mambo ya hovyo yasiyo na manufaa kwa umma il hali ni fedha za umma. Zitto huyohuyo akasema tarehe 20/04/2018 kwamba Bunge Lichunguze ili kujua ziliko fedha hizo. Hana uhakika na anachokiongea, hali hiyo ni Contradiction.

Kwa kutumia maelezo hayo ni wazi Zitto hana uhakika iwapo fedha zimefanyiwa Ubadhirifu au la, na ndiyo maana msimamo wake unayumba sana ktk suala hilo. Ingependeza sana iwapo Zitto na wengine wenye msimamo na mtazamo huo iwapo tu wangetueleza kwamba fedha hizo SH Trilioni 1.5 zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi gani ya maendeleo nchini na wathibitishe kwamba yeye na wenzake wamefanya uchunguzi au utafiti na kubaini shughuli hizo hazikufanyika. Kwa mfano wengesema kwamba SH BILIONI 500 katika hizo sh trilioni 1.5 zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa barabara X lakini fedha hizo hazikufanya kazi hiyo.

Au Zitto atueleze wazi kwamba Sh Bilioni 600 zilitengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za mikoa kadhaa ya X, Y, Q, K, nk lakini uchunguzi wake unaonesha hospitali hizo hazikujengwa.nk Akiweza kutubainishia kwamba Kiasi hicho cha Shilingi Trilioni 1.5 kilikuwa kwa ajili ya shughuli au Miradi kadha wa kadha ya maendeleo huku akiitaja kwa majina miradi hiyo na kutuonesha mahala ilipopaswa kutekelezwa halafu ikawa haikutekelezwa kweli kweli, basi hapo madai yake ya kwamba SH trilioni 1.5 zimefanyiwa Ubadhirifu yatakuwa halali. Vinginevyo asipofanya hivyo ni wazi anakuwa mtu wa kufanya kile waswahili wanaita bla-blaa.

Pia Zitto arejee Skendo ya ESCROW mwaka 2014 ambapo ktk vita ile tuliyopigana Bungeni miaka ile palikuwa na ushahidi usio na shaka wa Nyaraka za Kesi na hukumu zake, palikuwa na taarifa za kibenki zilizoonesha jinsi miamala ilivyofanyika na hivyo kudhihirisha ubadhirifu, Palikuwa na ushahidi wa nyaraka uliodhihirisha kwamba ktk fedha za ESCROW palikuwa na fedha za umma yaani kodi.

Kwa ujumla palikuwa na ushahidi usiokuwa na shaka yoyote tofauti na hili la trilioni 1.5 ambapo zitto anaongea na kuandika tu pasipo kutoa ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kwamba Serikali ilikusanya sh trilioni 25.3 lakini ilitumia sh trilioni 23.8 na kwamba huo ni ubadhirifu. Hiyo haitoshi kuwa ushahidi usio na shaka. Na zitto anafahamu kwamba Mtu au mlalamikaji anapotoa tuhuma dhidi ya mtu mwingine au mamlaka ni wajibu wake yeye mlalamikaji kuthibitisha madai au msingi wa tuhuma zake. Hivyo Zitto atuthibitishie pasipo shaka yoyote kwamba SH TRILIONI 1.5 zimefanyiwa ubadhirifu.

Kama hawezi kueleza kwamba zilikuwa ni fedha kwa ajili ya shughuli gani specifically na zilifanyiwa ubadhirifu gani ni wazi hajui anachokifanya na hivyo busara pekee ni awe na subira hadi kamati ya Bunge ya PAC na nyinginezo zitakapofanya kazi yake na kutoa ripoti. Kuendelea kusema zimefanyiwa ubadhirifu wakati hawezi kuthibitisha ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi mzoefu kama yeye. Pia anachokifanya ni kinyume cha Principles of Natural Justice kama imevyoandikwa katika kitabu cha HUMAN RIGHTS IN TANZANIA kilichoandikwa na Prof Chris Peter Maina kwamba haikubaliki kumuhukumu mtu pasipo kumsikiliza.

Hivyo kitendo cha Zitto kusema kwamba fedha zimefanyiwa ubadhirifu huku akiwa hatoi ushahidi ni kukiuka msingi huo wa kisheria katika utekelezaji wa haki. Vilevile licha ya serikali kupitia Kauli ya Waziri wa Fedha iliyosomwa Bungeni tarehe 20/04/2018 chini ya kanuni ya 49 ambayo ilieleza kwamba fedha hizo hazijafanyiwa ubadhirifu wowote, Zitto alipaswa kutoipinga taarifa hiyo bila yeye kuonesha jinsi ubadhirifu huo ulivyofanyika na abainishe fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya shughuli zipi. Ninaamini kwamba iwapo zitto atathibitisha hayo ataepuka kadhia ya kuitwa kanjanja wa kisiasa. Na pia zitto ajiulize maswali yafutayo:

What if Serikali ikaja na ushahidi usio na Shaka wa kuthibitisha matumizi ya 1.5 trln? What if pesa hizo zimetumika kununulia ndege zetu mpya za ATCL ambazo hata Mhe Zitto amesikika akisema kwamba anashangaa Kwa nini CAG hajakagua hela za manunuzi ya ndege na kutoa report? Kumbukeni kwamba serikali ilianza mchakato wa kununua ndege tangu mwaka 2016. What if serikali ikija na majibu na nyaraka sahihi kuonesha fedha hizo zimejenga viwanja vya ndege, barabara, zinajenga reli yetu ya SGR, Zinajenga Hospitali na vituo vya afya, sehemu nyingine imepelekwa Zanzibar, nk? mtaficha wapi nyuso zenu ninyi ambao mmesha conclude kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhirifu?

All in all, mimi binafsi sisemi kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhirifu au hazijafanyiwa ubadhirifu kwa sababu hata CAG hajasema lolote kuhusu fedha hizo na ndiyo maana nashangaa wanaosema kwamba zimefanyiwa ubadhirifu pasipo kutuonesha zilikuwa kwa ajili ya shughuli zipi na watuthibitishie madai yao pasipo shaka. Mhe. Zitto Ninaomba utupatie ushahidi usio na shaka kwa kuanisha shughuli ambazo zingepaswa kutekelezwa na hiyo sh trilioni 1.5 maana wewe umeenelea kupinga kauli ya Naibu waziri wa fedha.

Nawasilisha
 
Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.
Salaam.
Jana nilikuangalia na kukusikiliza kwa makini ulipokuwa wanatoa neno baada ya kuwaapisha Majaji uliowateua wiki hii. Niliona pia ulipomsimamisha CAG na kumuuliza kama kuna pesa trillioni 1.5 alizogundua kwamba zimeibiwa na akakujibu hakuna.
Pia nilikusikia ukisema umeisoma taarifa ya CAG mwanzo hadi mwisho.
Haraka nilikimbilia kitabu changu ambacho nami nimekisoma mwanzo mpaka mwisho.
Nilipofungua ukurasa wa 34 niligundua haya:-

1. CAG Anasema, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya mapato yenye dhamani ya Shilingi Trillioni 29.5

2. Mapato halisi yaliyokusanywa ni Shilingi Trillioni 25.3

3. Serikali ilitumia shilingi Trillion 23.8

4. Trillioni 25.3 ukitoa Trillion 23.8 ni Trillion 1.5 ambazo ndizo anazotaka apewe maelezo.

Mtukufu Rais CAG hajasema pesa zimeibiwa. Wala ktk hatua hii hawezi kusema hivyo. Anachosema fedha hizo, matumizi yake hayaonekani na hazipo popote. Inawezekana kweli zimeibiwa, zimetumika kwa uzembe bila kufuata sheria au zipo mahali fulani.

Kwa taratibu za kibunge Maafisa Masuuli(accounting officers) wanatakiwa wampelekee ushahidi wa matumizi yake au ziliko ktk Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali yaani PAC mbele ya CAG ili hoja hii ifungwe. Kama wakishindwa kuifunga PAC na CAG sasa wanaweza kuomba msaada wa Polisi na au Takukuru kutafuta wezi au wabadhirifu.

Mhe Rais bila shaka umesoma pia ktk ripoti kwamba Serikali ktk ujumla wake imepata HATI CHAFU.
Wakati ukipokea taarifa hii Ikulu uliagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kigoma Ujiji na wa Pangani watumbuliwe kutokana na maeneo yao kupata hati chafu.

Mhe unasubiri nini kumtumbua Katibu Mkuu hazina kwa kuisababishia Serikali yako kupata Hati chafu? Mbona kila mara unaapa kuwa mtu wa haki na jana uliwaagiza Majaji wakatende haki kwa Watanzania hasa wanyonge?

Mheshimiwa Serikali yako imepata doa kubwa. Vyombo vya dola haviwezi kulizuia kwa kuwatisha wanaoandika. Hizi ni fedha za maskini wote unaowatetea wauza maandazi, mitumba, mchicha na wengine wakubwa.

Ninakushauri baadala ya kuwatisha wanaohoji, waagize watendaji wa Serikali yako, wapeleke maelezo ya kutosha yenye ushahidi kwa CAG. Vinginevyo hatutaacha kukuuliza kila mara ZIKO WAPI PESA ZETU SHILINGI TRILLION 1.5

Jana Naibu waziri wa fedha alisema uongo Bungeni akidai sehemu ya fedha hizo Billioni 200 Serikali ya Muungano iliisaidia Serikali ya Zanzibar kukusanya mapato yake huku Bara.

Wote tunajiuliza vyanzo vya mapato ya ZNZ huku bara ni vipi? Hebu atutajie tuvijue na je! utaratibu huo ulikuwa wa 2016/17 peke yake tangu uhuru au ulikuwepo Taifa lisijue?
Mheshimiwa naona nakuchosha lakini nataka kusema neno la mwisho.
Inawezekana unadanganywa sana na waliokuzunguka na kwamba hawakuambii mambo mengi kwa faida yao. Wanapenda tu kukuambia yale wanayogundua unapenda kuyasikia na wanaogipa kukukosoa kutokana na ukali wako. Panua wigo wasikilize hata wale ambao hupendi kuwasikia hutakosa jambo lenye faida. Asante.
Joseph RS
 
Kwa vile Machali ni 'mpinzani wa hoja na viroja' vya serikali basi wapinzani wa JF watamkalia kimya na kuupita uzi huu!.
 
Hongera kwa chapisho zuri sana. Na hongera kwa kusoma hicho kitabu. Ubarikiwe sana
 
Zitto alichokuwa anajaribu kufanya ni ku undermine kazi za PAC kwa sababu yeye sio mjumbe.

Kwa kufanya hivyo akasoma ripoti ya CAG kwa haraka haraka ili kuwapiku PAC na chama kikuu cha upinzani CHADEMA.

Ndio maana akajumlisha na kutoa namba bila kujua kuwa kwa mwaka huo wa fedha wakaguzi wamebadilisha taratibu za ukaguzi na kwa sasa wako kwenye taratibu mpya.

Kwa sasa anachofanya ni kutetea reputation yake.

Inanikumbusha ule mwaka alioandika hotuba mbadala ya Wizara ya fedha bila kuwashirikisha CHADEMA na matokeo yake akasahau hata kuweka liabilities. Hotuba yake ikachambuliwa na Mwigulu bungeni kiasi kwamba akaomba msamaha kwa kukosea.
 
Huu mkeka ungekuwa ni wa mbet au meridian bet basi expected win amount ingekuwa 1.5t..
 
Ukisharudi CCM akili yote unakabidhi kwa Polepole wewe unatembea na kopo wazi! Ndicho kinachowakumba akina Machali na Kafulia!!
 
JE, ZITTO NI MBADHIRIFU KTK KILE KINACHOITWA UBADHIRIFU WA TRILIONI 1.5?
Na Moses Machali
21/04/2018

Ubadhirifu ni nini?
Kwa Mujibu wa Kamusi ya Maana ya Matumizi (Bakhressa Salim K, 1992) katika Ukurasa wa 400 neno Ubadhilifu lina maana ya : “Utumiaji mbaya wa kitu, mali; Ufujaji; Uhulikaji” huku TUKI (2001; Uk. 331)katika Kamusi ya Kiswahili – Kiingereza neno UBADHILIFU lina maana ya “Misappropriation, Embezzlement.” Dhana ya embezzlement katika kamusi ya kiingereza iitwayo RANDOM HOUSE WEBSTER’S COLLEGE DICTIONARY iliyochapishwa mwaka 1997, katika ukurasa wa 426 inaelezwa kwamba Embezzle means “to appropriate fraudulently to one’s own use, as money entrusted to one’s care.” Kwa ujumla neno Ubadhilifu ni wizi au utumiaji wa kitu vibaya.

Baada ya ripoti za CAG kuwekwa hadharani kumeibuka mjadala mkali sana kuhusu SH TRILIONI 1.5. Mjadala huo umesababisha taharuki miongoni mwetu watanzania. Mmoja wa watu walioshikia Bango suala hilo ni Mhe. Kabwe Zuberi Ryagwa Zitto, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ambaye katika Ukurasa wake wa Facebook amekuwa akiutumia kwa kuandika statement mbalimbali kuhusu issue hiyo y sh trilioni 1.5. Kwa mfano Tarehe 18/04/2018 saa 12:23 pm aliandika kwamba:
“Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.

Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.
Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa).
Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie”

Katika aya ya mwisho ya andiko lake anasema kwamba yupo tayari kukamatwa na wala hilo halitafuta ukweli wa Ubadhirifu huo. Hiyo ndiyo kusema kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhilifu na wenye mamlaka ya kuzisimamia kimatumizi, au zimefujwa na wenye mamlaka ya kuzisimamia kimatumizi.

Mhe. Zitto huyohuyo, mnamo tarehe 20/04/2018 akaandika tena facebook kwamba:
“Serikali Inasema Uongo, Ni Muhimu Bunge Lichunguze Ziliko 1.5 Trilioni
-Taarifa Ndogo ya ACT Wazalendo Juu ya Majibu ya Serikali Bungeni Juu ya Ziliko 1.5 Trilioni Zisizoonekana Matumizi yake Kwenye Ripoti ya CAG
Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu.”

Hiyo ina maana kwamba Zitto hajui na au hana uhakika wa mahala fedha zilipo na wala hajui zimefanyiwa kitu gani na hivyo anaomba au anataka Bunge Lichunguze ili kupata uhakika wa matumizi ya fedha hizo.
Mtu Makini anapokutana na statement hizo mbili tofauti lazima atasema kwamba Zitto ana tatizo la UBADHIRIFU wa Kifikra yaani anatumia utashi wake vibaya kwa maslahi yake binafsi na inaweza kuwa ya kisiasa au ya kiuchumi kwa sababu mwanzoni kabisaa tarehe 18 APRIL 2018 alisema kwamba ‘….yuko tayari kukamatwa na kwamba fedha hizo zimefanyiwa Ubadhirifu yaani wizi au matumizi mabaya. Ieleweke kwamba Matumizi mabaya inaweza kuwa zimeibiwa kwa ajili ya mtu binafsi au zimefanya mambo ya hovyo yasiyo na manufaa kwa umma il hali ni fedha za umma. Zitto huyohuyo akasema tarehe 20/04/2018 kwamba Bunge Lichunguze ili kujua ziliko fedha hizo. Hana uhakika na anachokiongea, hali hiyo ni Contradiction.

Kwa kutumia maelezo hayo ni wazi Zitto hana uhakika iwapo fedha zimefanyiwa Ubadhirifu au la, na ndiyo maana msimamo wake unayumba sana ktk suala hilo. Ingependeza sana iwapo Zitto na wengine wenye msimamo na mtazamo huo iwapo tu wangetueleza kwamba fedha hizo SH Trilioni 1.5 zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi gani ya maendeleo nchini na wathibitishe kwamba yeye na wenzake wamefanya uchunguzi au utafiti na kubaini shughuli hizo hazikufanyika. Kwa mfano wengesema kwamba SH BILIONI 500 katika hizo sh trilioni 1.5 zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa barabara X lakini fedha hizo hazikufanya kazi hiyo.

Au Zitto atueleze wazi kwamba Sh Bilioni 600 zilitengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za mikoa kadhaa ya X, Y, Q, K, nk lakini uchunguzi wake unaonesha hospitali hizo hazikujengwa.nk Akiweza kutubainishia kwamba Kiasi hicho cha Shilingi Trilioni 1.5 kilikuwa kwa ajili ya shughuli au Miradi kadha wa kadha ya maendeleo huku akiitaja kwa majina miradi hiyo na kutuonesha mahala ilipopaswa kutekelezwa halafu ikawa haikutekelezwa kweli kweli, basi hapo madai yake ya kwamba SH trilioni 1.5 zimefanyiwa Ubadhirifu yatakuwa halali. Vinginevyo asipofanya hivyo ni wazi anakuwa mtu wa kufanya kile waswahili wanaita bla-blaa.

Pia Zitto arejee Skendo ya ESCROW mwaka 2014 ambapo ktk vita ile tuliyopigana Bungeni miaka ile palikuwa na ushahidi usio na shaka wa Nyaraka za Kesi na hukumu zake, palikuwa na taarifa za kibenki zilizoonesha jinsi miamala ilivyofanyika na hivyo kudhihirisha ubadhirifu, Palikuwa na ushahidi wa nyaraka uliodhihirisha kwamba ktk fedha za ESCROW palikuwa na fedha za umma yaani kodi.

Kwa ujumla palikuwa na ushahidi usiokuwa na shaka yoyote tofauti na hili la trilioni 1.5 ambapo zitto anaongea na kuandika tu pasipo kutoa ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kwamba Serikali ilikusanya sh trilioni 25.3 lakini ilitumia sh trilioni 23.8 na kwamba huo ni ubadhirifu. Hiyo haitoshi kuwa ushahidi usio na shaka. Na zitto anafahamu kwamba Mtu au mlalamikaji anapotoa tuhuma dhidi ya mtu mwingine au mamlaka ni wajibu wake yeye mlalamikaji kuthibitisha madai au msingi wa tuhuma zake. Hivyo Zitto atuthibitishie pasipo shaka yoyote kwamba SH TRILIONI 1.5 zimefanyiwa ubadhirifu.

Kama hawezi kueleza kwamba zilikuwa ni fedha kwa ajili ya shughuli gani specifically na zilifanyiwa ubadhirifu gani ni wazi hajui anachokifanya na hivyo busara pekee ni awe na subira hadi kamati ya Bunge ya PAC na nyinginezo zitakapofanya kazi yake na kutoa ripoti. Kuendelea kusema zimefanyiwa ubadhirifu wakati hawezi kuthibitisha ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi mzoefu kama yeye. Pia anachokifanya ni kinyume cha Principles of Natural Justice kama imevyoandikwa katika kitabu cha HUMAN RIGHTS IN TANZANIA kilichoandikwa na Prof Chris Peter Maina kwamba haikubaliki kumuhukumu mtu pasipo kumsikiliza.

Hivyo kitendo cha Zitto kusema kwamba fedha zimefanyiwa ubadhirifu huku akiwa hatoi ushahidi ni kukiuka msingi huo wa kisheria katika utekelezaji wa haki. Vilevile licha ya serikali kupitia Kauli ya Waziri wa Fedha iliyosomwa Bungeni tarehe 20/04/2018 chini ya kanuni ya 49 ambayo ilieleza kwamba fedha hizo hazijafanyiwa ubadhirifu wowote, Zitto alipaswa kutoipinga taarifa hiyo bila yeye kuonesha jinsi ubadhirifu huo ulivyofanyika na abainishe fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya shughuli zipi. Ninaamini kwamba iwapo zitto atathibitisha hayo ataepuka kadhia ya kuitwa kanjanja wa kisiasa. Na pia zitto ajiulize maswali yafutayo:

What if Serikali ikaja na ushahidi usio na Shaka wa kuthibitisha matumizi ya 1.5 trln? What if pesa hizo zimetumika kununulia ndege zetu mpya za ATCL ambazo hata Mhe Zitto amesikika akisema kwamba anashangaa Kwa nini CAG hajakagua hela za manunuzi ya ndege na kutoa report? Kumbukeni kwamba serikali ilianza mchakato wa kununua ndege tangu mwaka 2016. What if serikali ikija na majibu na nyaraka sahihi kuonesha fedha hizo zimejenga viwanja vya ndege, barabara, zinajenga reli yetu ya SGR, Zinajenga Hospitali na vituo vya afya, sehemu nyingine imepelekwa Zanzibar, nk? mtaficha wapi nyuso zenu ninyi ambao mmesha conclude kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhirifu?

All in all, mimi binafsi sisemi kwamba fedha hizo zimefanyiwa ubadhirifu au hazijafanyiwa ubadhirifu kwa sababu hata CAG hajasema lolote kuhusu fedha hizo na ndiyo maana nashangaa wanaosema kwamba zimefanyiwa ubadhirifu pasipo kutuonesha zilikuwa kwa ajili ya shughuli zipi na watuthibitishie madai yao pasipo shaka. Mhe. Zitto Ninaomba utupatie ushahidi usio na shaka kwa kuanisha shughuli ambazo zingepaswa kutekelezwa na hiyo sh trilioni 1.5 maana wewe umeenelea kupinga kauli ya Naibu waziri wa fedha.

Nawasilisha

Hata mzee baba amesema report iende pac kama sheria inavyotaka bila Zito kuliamsha wewe na wenzako mngepata wapi story.

Kupishana na serikali ndio kazi ya upinzani, kuitwa mbadhilifu hivi JK angekuwa na tabia hizi zenu za kushitaki kila mtu mnafikiri MV Dar es Salaam ingeenda jeshini kimya kimya tu.

Ebu mtuache wengine tufikiri tofauti na nyie, Zitto lazima apige mkwara akilegeza akina DAB si watammininia risasi kama walivyofanya kwa wengine.
 
wandamba, watu mnahangaika na mtahangaika sana katika hili. Kwa miezi zaidi ya tisa (Julai 2017 hadi Aprili 2018) serikali ilikuwa na muda wa kutosha kutoa maelezo trilioni 1.5 zilitumikaje. Maelezo yalipokosekana CAG akatoa ripoti yake na baada ya hii ripoti ndio serikali inahangaika kujisafisha. Tatizo ni kwamba harufu ta trilioni 1.5 ni kali na ni vigumu kweli kuisafisha kama ya mnyama aitwaye skunk, huyu mnyama ukimgusa utanuka na mnuko wenyewe hauishi hata kwa pafyumu ya kawaida. Kwa ufahamisho tu serikali ya Magufuli haikumgusa tu skunk, imemkumbatia, si harufu hiyo!
 
Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.
Salaam.
Jana nilikuangalia na kukusikiliza kwa makini ulipokuwa wanatoa neno baada ya kuwaapisha Majaji uliowateua wiki hii. Niliona pia ulipomsimamisha CAG na kumuuliza kama kuna pesa trillioni 1.5 alizogundua kwamba zimeibiwa na akakujibu hakuna.
Pia nilikusikia ukisema umeisoma taarifa ya CAG mwanzo hadi mwisho.
Haraka nilikimbilia kitabu changu ambacho nami nimekisoma mwanzo mpaka mwisho.
Nilipofungua ukurasa wa 34 niligundua haya:-

1. CAG Anasema, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya mapato yenye dhamani ya Shilingi Trillioni 29.5

2. Mapato halisi yaliyokusanywa ni Shilingi Trillioni 25.3

3. Serikali ilitumia shilingi Trillion 23.8

4. Trillioni 25.3 ukitoa Trillion 23.8 ni Trillion 1.5 ambazo ndizo anazotaka apewe maelezo.

Mtukufu Rais CAG hajasema pesa zimeibiwa. Wala ktk hatua hii hawezi kusema hivyo. Anachosema fedha hizo, matumizi yake hayaonekani na hazipo popote. Inawezekana kweli zimeibiwa, zimetumika kwa uzembe bila kufuata sheria au zipo mahali fulani.

Kwa taratibu za kibunge Maafisa Masuuli(accounting officers) wanatakiwa wampelekee ushahidi wa matumizi yake au ziliko ktk Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali yaani PAC mbele ya CAG ili hoja hii ifungwe. Kama wakishindwa kuifunga PAC na CAG sasa wanaweza kuomba msaada wa Polisi na au Takukuru kutafuta wezi au wabadhirifu.

Mhe Rais bila shaka umesoma pia ktk ripoti kwamba Serikali ktk ujumla wake imepata HATI CHAFU.
Wakati ukipokea taarifa hii Ikulu uliagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kigoma Ujiji na wa Pangani watumbuliwe kutokana na maeneo yao kupata hati chafu.

Mhe unasubiri nini kumtumbua Katibu Mkuu hazina kwa kuisababishia Serikali yako kupata Hati chafu? Mbona kila mara unaapa kuwa mtu wa haki na jana uliwaagiza Majaji wakatende haki kwa Watanzania hasa wanyonge?

Mheshimiwa Serikali yako imepata doa kubwa. Vyombo vya dola haviwezi kulizuia kwa kuwatisha wanaoandika. Hizi ni fedha za maskini wote unaowatetea wauza maandazi, mitumba, mchicha na wengine wakubwa.

Ninakushauri baadala ya kuwatisha wanaohoji, waagize watendaji wa Serikali yako, wapeleke maelezo ya kutosha yenye ushahidi kwa CAG. Vinginevyo hatutaacha kukuuliza kila mara ZIKO WAPI PESA ZETU SHILINGI TRILLION 1.5

Jana Naibu waziri wa fedha alisema uongo Bungeni akidai sehemu ya fedha hizo Billioni 200 Serikali ya Muungano iliisaidia Serikali ya Zanzibar kukusanya mapato yake huku Bara.

Wote tunajiuliza vyanzo vya mapato ya ZNZ huku bara ni vipi? Hebu atutajie tuvijue na je! utaratibu huo ulikuwa wa 2016/17 peke yake tangu uhuru au ulikuwepo Taifa lisijue?
Mheshimiwa naona nakuchosha lakini nataka kusema neno la mwisho.
Inawezekana unadanganywa sana na waliokuzunguka na kwamba hawakuambii mambo mengi kwa faida yao. Wanapenda tu kukuambia yale wanayogundua unapenda kuyasikia na wanaogipa kukukosoa kutokana na ukali wako. Panua wigo wasikilize hata wale ambao hupendi kuwasikia hutakosa jambo lenye faida. Asante.
Joseph RS
Machaliiiiii weee unatafuta huruma kwa wakubwaee matumizi ya hela ya serikali yanapangwwa na bunge hiyo hoja yako ya kama zimetumika kununua ndege ni dhaifu ni nje ya bajeti ya serikali ndio maana watu wanauliza wajue zimetumikaje 1.5
 
Inaelekea maelezo ya serikali hayajajitosheleza hivyo watu wanataka kujua zaidi kuhusu trillion 1.5.
Sioni kama ni busara kuzuia watu kuuliza hasa wabunge maana ni sauti ya wananchi wanaowawakilisha.

Hizo pesa sio pesa za mtu binafsi, ni mali ya umma...viongozi mnawajibikaji kwa umma...tumieni busara kujieleza sio kiburi na ubabe.
 
Njaa ni ugonjwa mbaya sana kuwahi kutokea hapa duniani. Bahati nzuri Jiwe huwa haliwakumbatii baadhi ya wanafiki, vigeugeu na vizabizabina. Kwa hilo nampongeza.
 
Back
Top Bottom