MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,114
- 3,768
Sarafu ya Urus ya Ruble imeporomoka kwa asilimia 90% dhidi ya Dola ya Marekani huku nakisi ya bajeti ya nchi hiyo ikifikia zaidi ya asilimia 30 ndani ya kipindi cha miezi 3. Hii inatokana na kudolola kwa mauzo ya nje ya nchi hiyo kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi.
Kabla ya Urusi kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi, thamani ya Dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Ruble 60 za Urusi, lakini mpaka sasa masoko ya Hisa yanaonesha Thamani ya Dola moja ya Marekani imefikia zaidi ya Ruble 100 za Urusi.
Haya yanajiri ikiwa ni baada ya Wizara ya fedha ya Urusi kupanga kutumia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 100 ($ 100B) kwenye Ulinzi ambayo ni sawa na asilimia 30% ya matumizi yote ya serikali. Sekta za Afya, Elimu na Miundombinu ndizo zitakazo athirika zaidi kwani fedha nyingi zitachotwa kutoka wizara hizo kuelekezwa kwenye wizara ya Ulinzi.
Source : Aljazeera.