Morogoro: Wafanyakazi tisa wa LTSP[Wizara ya ardhi], wafariki kwenye ajali Kilombero

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Vijana Tisa Wa mradi Wa LTSP wamefariki dunia jioni hii mjini Ifakara baada ya Gari iliyowabeba kipinduka na kuingia mtoni na wanne wamejeruhiwa,miili na majeruhi wapo hospitali ya rufaa ya Mt.Francis

Walikuwa wakitokea Kiberege kuelekea Ifakara

Wapumzike kwa amani. Amen


=====

Watu tisa ambao ni wataalam wa idara ya Ardhi wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kumshinda nguvu dereva na kutumbukia mtoni wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo amethibitisha na kusema gari hiyo ilikuwa na watu 13 ambapo 9 ndio wamefariki huku waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali ya St.Francis kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Habari zaidi...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki
wa Familia za Watumishi Wanane wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Mfanyakazi Mmoja wa Chama Kijamii waliofariki katika ajali ya
barabarani iliyotokea tarehe 23 Februari, 2019, katika Mto Kikwawila, Wilaya ya
Kilombero, Mkoani Morogoro.

Gari ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili STK 994, waliopanda Watumishi hao ambao walikuwa Wanatekeleza Mradi wa Wizara hiyo, kwenye Halmashauri hiyo, ilikuwa inaenda Ifakara ilipofika daraja la Mto Kikwawila liliingia kwenye daraja na kutumbukia Mtoni upande wa kushoto na kusababisha vifo vya Watumishi tisa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, MB,
kwa masikitiko makubwa anatoa pole kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi, pamoja na ndugu wa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.

“Natoa pole nyingi kwa Mheshimiwa Waziri Lukuvi, ndugu, jamaa na marafiki waliowapoteza wapendwa wao katika ajali hii, Mwenyezi Mungu aziweke roho za Marehemu mahali pema peponi, Amina,”.

Imetolewa na:
Meja Jenerali Jacob G. Kingu, ndc
KATIBU MKUU
23 Februari, 2019.
 
#BRAKINGNEWS;Watu tisa ambao ni wataalam wa idara ya Ardhi wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kumshinda nguvu dereva na kutumbukia mtoni wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo amethibitisha na kusema gari hiyo ilikuwa na watu 13 ambapo 9 ndio wamefariki huku waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali ya St.Francis kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 
AJALI MBAYA WILAYANI KILOMBERO, TISA WAFARIKI

Ni wataalam wa idara ya ardhi, chanzo cha ajali ni gari walilokuwa wakisafiria kumshinda nguvu dereva na kutumbukia mtoni wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Majeruhi wamepelekwa hospitali ya St.Francis kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 
Back
Top Bottom