Morogoro: Mabadiliko ya tabia nchi

Morogoro: Mabadiliko ya tabia nchi

Real Deal

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
280
Reaction score
114
Niko Morogoro kwa zaidi ya wiki moja sasa, hali ya hewa ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka kumi na tano nyuma. Nakumbuka wakati ule muda kama huu hakukuwa na joto kiasi hiki, Hali ya hewa ilikuwa ni ya u baridi na mawingu mengi, Jua na humidity havikuwa kama ilivyo sasa. Kama ni mabadiliko ya tabia nchi basi Morogoro yajidhihirisha kabisa. Wadau/wenyeji wa Morogoro hii hali imeanza lini.
 
nadhani ni sehemu ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
 
Kama sehemu haijakaliwa na watu kama Amazon sidhani kama kuna cha tabia nchi wala nini
Ila tatizo kubwa ni idadi ya watu kuongezeka na kuharibu vyanzo vya maji na ukataji wa miti
Ukirudi tena baada ya miaka 20 hivi utakuta jangwa kabisa kama hatutaangalia na kutunza ardhi yetu hii nzuri

Nafikiri hata wanyama na ndege uliokuwa unawaona wengi hawapo pia.
 
Wataalam wanasema Global Warming. Na huu ni mwanzo tu na watu wengi sana watakufa kwa hili joto hatarishi. Mvua pia zitakuwa ni kubwa sana kuliko ilivyo kawaida hivyo kuleta maafa makubwa sana sehemu mbali mbali
Duniani.

Niko Morogoro kwa zaidi ya wiki moja sasa, hali ya hewa ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka kumi na tano nyuma. Nakumbuka wakati ule muda kama huu hakukuwa na joto kiasi hiki, Hali ya hewa ilikuwa ni ya u baridi na mawingu mengi, Jua na humidity havikuwa kama ilivyo sasa. Kama ni mabadiliko ya tabia nchi basi Morogoro yajidhihirisha kabisa. Wadau/wenyeji wa Morogoro hii hali imeanza lini.
 
Niko Morogoro kwa zaidi ya wiki moja sasa, hali ya hewa ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka kumi na tano nyuma. Nakumbuka wakati ule muda kama huu hakukuwa na joto kiasi hiki, Hali ya hewa ilikuwa ni ya u baridi na mawingu mengi, Jua na humidity havikuwa kama ilivyo sasa. Kama ni mabadiliko ya tabia nchi basi Morogoro yajidhihirisha kabisa. Wadau/wenyeji wa Morogoro hii hali imeanza lini.

Kuna kiasi kikubwa cha uharibifu wa mazingira hapo, kuna RC mmoja simkumbuki, alisimamia sana zoezi la upandaji miti japo wenyeji wakawa wanalaani kazi hiyo kwa kisingizio kuwa miti inaleta kunguru
 
Hii hali inatisha kwa kweli, Global Warming/Climate change kwa Morogoro effects zake zinaonekana kwa wazi kabisa. Ajabu ni kwamba viongozi wenye kufanya maamuzi na wananchi wa Morogoro wanachukulia poa tuu.

Nilipanda mlima uluguru hadi Morning site, mlima mzima watu wamejenga na kulima mashamba, yale maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka juu yamepungua sana na sehemu nyingine yamekauka kabisa.

Nimeambiwa kuwa mvua ikinyesha Morogoro mjini ni mafuriko, mitaro yote inajaa matope (sababu ya mmomonyoko wa udongo) na kusababisha madhara kwa wakazi na biashara.

Viongozi na wananchi wa Morogoro hamuoni kuwa hili ni tatizo? kwa nini kampeni za kupanda miti na kuzuia watu kujenga na kulima milimani hazipo tena?
 
Kuna kiasi kikubwa cha uharibifu wa mazingira hapo, kuna RC mmoja simkumbuki, alisimamia sana zoezi la upandaji miti japo wenyeji wakawa wanalaani kazi hiyo kwa kisingizio kuwa miti inaleta kunguru
Sasa kunguru na mafuriko, ukosefu wa maji na joto kipi bora? Kunguru wanadhibitika mfano Dar es salaam kunguru wamepungua sana.
 
Wataalam wanasema Global Warming. Na huu ni mwanzo tu na watu wengi sana watakufa kwa hili joto hatarishi. Mvua pia zitakuwa ni kubwa sana kuliko ilivyo kawaida hivyo kuleta maafa makubwa sana sehemu mbali mbali
Duniani.
Nadhani Morogoro hali sio nzuri kabisa, impact yake ni kubwa sana na hasa ukizingatia kuwa iko karibu na jiji la Dar effect ya high population Dar inaonekana Morogoro.
 
Nadhani ndio Mkoa unaoongoza kwa uuzaji wa mikaa! Wanakata sana miti kwa ajili ya kutengenezea mikaa.
 
Sasa kunguru na mafuriko, ukosefu wa maji na joto kipi bora? Kunguru wanadhibitika mfano Dar es salaam kunguru wamepungua sana.

Mentality yao haiyaoni hayo, wanachokiona ni kunguru wakiwa vibarazani
 
Nadhani ndio Mkoa unaoongoza kwa uuzaji wa mikaa! Wanakata sana miti kwa ajili ya kutengenezea mikaa.
Hii nakubaliana nayo. Hivi ile kampeni ya kuzuia utengenezaji, uuzwaji na matumizi ya mkaa imefikia wapi? Au ndo imekufa kama zinavyokufa kampeni zingine zenye manufaa? Na uhamasishaji wa matumizi ya gesi umefikia wapi maana a gesi ndo zinazidi kupanda tuu.
 
Nilikua Lushoto - Tanga last week, kuna joto na mbu balaaa. Sikuamini kabisa, eneo lililokua na Baridi Kali eti nimelala bila blanket?
 
Lushoto iliyokuwa inajulikama kama Geneva of Africa kuna mbu sasa hivi?? mi nimefika huko kabla ya 2000 kwa kweli kulikuwa kunapendeza sana.
 
Back
Top Bottom