'Morogoro-Dar' aikampenia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Morogoro-Dar' aikampenia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Oct 15, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  chizi maarufu mjini dodoma almaarufu 'morogoro-dar' au 'usalama wa taifa' amekuwa akionekana katika mitaa ya mji huu; huku akiwa katika mbio kwenye mitaa ya jiji hili, akipuliza kipenga chake maarufu na kutamka maneno, chagua ccm chagua kikwete.


  huyu chizi kutoka katika kijiji cha mdachi, nje kidogo ya jiji hili amekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa mji huu tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu.


  akivaa t-shirt, kofia na suruali mahsusi za kampeni za ccm, chizi huyo amefanikiwa kuwa kiburudisho kwa wakazi wa dodoma na hapohapo kupiga kampeni.


  'morogoro-dar' ni maarufu hapa mjini dodoma kwa haya;

  • kipenga chake analolipiga kila mara kuonesha uwepo wake mtaa huo
  • zeze lake analolipiga kila mara kwa mahadhi ya cigogo
  • 'kujifanya?' chizi inayopelekea watu kumbatiza 'usalama wa taifa'
  • maneno yake anayotamka kila baada ya takribani sekunde tatu kila awapo hadharani; yaani madereva morogoro dar wanawake laki nane akimaanisha madereva wa barabara tajwa aghalabu huwa na nyumba ndogo kila kituo kwa mtazamo wake.

  nawasilisha!!!
   
Loading...