Morogoro: Auawa akiamulia ugomvi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,047
Reaction score
6,958
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Mwendapole (22), maarufu kwa jina la Juja wa Ubalozini amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu katika tukio lililotokea kwenye nyumba moja ya starehe (bar) Manispaa ya Morogoro.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manyuki, Rashid Ally amesema Michael aliondoka akiwa na rafiki zake wawili kwenda katika eneo hilo la starehe, ambapo baadaye usiku kulitokea ugomvi uliosababisha Kijana huyo kuchomwa kisu.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa Watu waliozungumza na AyoTV, Michael anadaiwa kuingilia kati ugomvi huo kwa lengo la kumzuia rafiki yake asipigwe, ndipo akachomwa kisu, huku mazingira kamili ya tukio hilo bado yanahitaji uthibitisho kutoka Jeshi la Polisi.

Soma Pia: Morogoro: Jovita adaiwa kumuua mumewe kisa kanyimwa unyumba


 
Pombe, Starehe, wanawake vinatumaliza wanaume
 
Nimeshuhudia na kusikia cases nyingi za mtu kuuawa kwa kwenda kuamulia ugomvi.

Wadau inabidi mambo ya kuamulia ugomvi muyaache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…