Umesema umri kuanzia 33 nakuendelea, mimi nina umri 69 years vp?:bange: utanikubali?
Midhali uko tayari kukusolewa, kushauriwa uwe tayari zaidi. Mi si mkristo sitarajii kuku PM. Imenenwa "mpendelee nduguyako lile ambalo unalipenda wewe nafsini mwako". Tafuta contacts za Dr W Slaa (mgombea urais Tz 2010). Huyu anakidhi karibu vigezo vyako vingi na ana shida, Inasemekana amefikia hadi kuazima au kupora wake za watu jinsi alivyo na shida ya mke.
1 Anapenda na ana uwezo wa kukosoa, katika ndoa yenu uta enjoy na hilo, 2 umri wake ni zaidi ya miaka 33. 3 ni Mkristo, ni padri mpenda bwana hata katika Uchaguzi mkuu wakristo wengi waliridhika nae. 4 ana elimu ya kujitosheleza naamini hakusoma shule za Memkwa wala UPE, 5 kajiajiri kisiasa zaidi, posho yake siijui kwa siku ni kiasi gani lakini matanuzi anayo, usishangae posa za awali na pete vinaweza kuletwa kwa helikopta kama kwenu hakuna barabara, wakati wa ndoa yenu mnaweza mkajinunulia gari la kwendea msalani na lingine sokoni n k.
Sikufatilia kabila lake halisi kama ni mtusi au mmasai ila dalili za ubantu na uhutu hana. any way midhali kigezo kwako si tatizo naamini utamtafuta.
Hii isije ikafikirika namfagilia Slaa peke yake ila na wewe pia nataka ukipate unachotafuta
PretA naona unawapigia chapuo wakaka wa humu JF. mtieni moyo mdada huyu na pia kuweni makini na kumlinda ktk mjadala huu hapa JF kuna watu humu mwezi mchanga hawakawii kuharibu nia safi ya mgeni wetu aliyetujia na shida yake tena anahitaji kuanzisha familia na mwanaJF mwezetu, tumsupport hadi atakapofanikiwa. Pia jena baada ya mafanikio usisite kutupa taarifa ili HARUSI hiyo ifanikishwe na wana JF pia.karibu sana jukwaani dada Jena......nakuhakikishia hapa JF utapata mume mwema.....ila ujiandae kwa masihara lakini usikate tamaa....wapo walio single na wana heshima zao....nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki katika jambo hili
What a coincedence! Wana Jf heshima kwenu, ni mara yangu ya kwanza kuchangia humu jamvini lakini nakutana na habari njema za mchumba, ki ukweli niko single na ninahitaji mchumba umri miaka 34, nafanya kazi serikalini lakini nina hofu kweli na namna hii ya kupata mchumba ni kweli naweza kupata mtu anayefaa kweli kimaisha? Jamani.. "we are talking about life here! Let's be more than serious!
Umesema umri kuanzia 33 nakuendelea, mimi nina umri 69 years vp?:bange: utanikubali?
Kila la heri Dada Jena. Endelea kusali na kuomba, na Mungu Atakujalia. Umefanya vizuri kuamini kuwa mume anatoka kwa Mungu. Ukiwa na imani hiyo, ninakushauri pia katika maombi yako uzingatie mume aliye na heri na wewe zaidi kuliko sifa ulizotaja tu.
just a question...kwa nini unataka kuolewa kiasi hicho?
Mimi Niko tayari!umri wangu miaka 35,elimu yangu chuo kikuu,nimeajiriwa
wana jf, mimi ni mwanadada na leo nimeona nijitoe muhanga kabisa maana ninahitaji mume/mchumba. Niko tayari kupokea kukosolewa ila kwa yule aliyeko kwenye shinda kama yangu tafadhali ni pm.
Mimi ni mkristo ninayempenda mungu na ninahofu ya mungu ndani yangu, tayari niko kwenye umri wa kati ya 30-33 na ninahitaji mume wa kati ya 33 na kuendelea. Awe na elimu ya kujitosheleza, mfanyakazi au aliyejiajiri. Kabila lolote tanzania na pia awe mkristo. Hili swala naomba tu mchukulie kwangu ni kitu halisi hapa sina utani na wala siko kwa ajili ya kumpotezea mtu muda. Na katika hili pia namshikirisha mungu nikiamini mume/mke mwema anatoka kwa bwana. Na pia kwa wale watakao nishauri na kunitia moyo kwenye hili nawashukuru. Kaka zangu popote pale ulipo na unajiona kweli unahitaji mke naomba uni pm lakini kama ni swala la mzaha au kujaribisha naomba usipoteze muda.
Wana JF, mimi ni mwanadada na leo nimeona nijitoe muhanga kabisa maana ninahitaji mume/mchumba. Niko tayari kupokea kukosolewa ila kwa yule aliyeko kwenye shinda kama yangu tafadhali ni PM.
Mimi ni Mkristo ninayempenda Mungu na ninahofu ya Mungu ndani yangu, tayari niko kwenye umri wa kati ya 30-33 na ninahitaji mume wa kati ya 33 na kuendelea. Awe na elimu ya kujitosheleza, mfanyakazi au aliyejiajiri. Kabila lolote Tanzania na pia awe Mkristo. Hili swala naomba tu mchukulie kwangu ni kitu halisi hapa sina utani na wala siko kwa ajili ya kumpotezea mtu muda. Na katika hili pia namshikirisha Mungu nikiamini mume/mke mwema anatoka kwa Bwana. Na pia kwa wale watakao nishauri na kunitia moyo kwenye hili nawashukuru. Kaka zangu popote pale ulipo na unajiona kweli unahitaji mke naomba uni PM lakini kama ni swala la mzaha au kujaribisha naomba usipoteze muda.