More Magufuli, more reforms, tumuongezee muda Magufuli

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MORE MAGUFULI,MORE REFORMS, TUMUONGEZEE MUDA MAGUFULI.

Leo 16:15pm 10/06/2020

Maelezo ama narrative ya viongozi wengi awamu ya tatu na nne zilikuwa zina-reflect namna ya kugawana mapato ya Taifa la Tanzania, kuuza vitalu, kuuza madini, mikataba mibovu.

Kwa ujumla narrative za viongozi katika awamu zilizopita zilionyesha namna ya kugawana keki ya Taifa iliyokuwa inapatikana nchini,namna ya kuvuna vyeo,utajiri na kuzistawisha familia zao,

Awamu tatu zilizopita ukiwa na cheo Serikalini basi ulikuwa unakuwa maarufu hata kama taasisi yako ama Wizara yako haina uimara wala tija yoyote katika Taifa.

Rais Magufuli amebadili gia angani, amewatenga vinara wa ugavi wenye mazoea ya kugawana keki ya Taifa huku watu Milioni 60 wakibaki masikini wakichekwa hata na Kenya!

Yapo ambayo Rais Magufuli hajayasimamia kwa upungufu wa pato la Taifa lakini in the process anaendelea kurekebisha kila mahali ili pato liweze kuongezeka na kuwezesha kufanya mambo makubwa zaidi,

Rais Magufuli licha ya upungufu wa pato la Taifa amechagua miradi mikubwa ya kimkakati ya matrilioni ya hela ambayo kwa kweli japo inakula hela nyingi lakini ni ya manufaa sana kwa Taifa na ni miradi endelevu itayoleta tija kwa kizazi cha Sasa hata vizazi kumi vijavyo,

Tupo Watanzania Milioni 60 lakini nikiri wazi Magufuli ni mmoja tu kati ya watu Milioni 60,Magufuli mmoja anawakilisha takribani nusu ya Watanzania ambao sauti zao zilikuwa zinaminywa na Watanzania wachache matajiri,

Kwa miaka mingi Watanzania waliitaji mtu wa kuyasemea matatizo yao lakini hakupatikana hadi alipokuja Magufuli,ndio maana kila mtu anamuona Magufuli kama katoka sayari nyingine kwa kuwa Watanzania Milioni 60 kwa miaka 30 baada ya Nyerere walikosa Kiongozi anayemaanisha anachoongea na kufanya,

Niungane na kila mmoja kusema,Kama Magufuli atapata muda zaidi ina maana more reforms,mabadiliko zaidi,Viwanda zaidi,Uchumi wa nchi zaidi,Uadilifu zaidi,uchapakazi zaidi na Uzalendo zaidi,

Otherwise tuanze ku support hizi reforms anazofanya ili ziweze kujenga narrative mpya ya taifa na ziweze kujenga vigezo vipya vya aina ya uongozi tunaoutaka kwa nchi yetu, tuviingize kwenye mjadala wa taifa na ndivyo vitumike kupata kiongozi mpya baada ya Magufuli na wasomi wetu wabadilike na waanze kuwaza namna ya kubuni zana za uzalishaji mkubwa utakaotosheleza mahitaji yetu ya nchi na lifestyles zetu. otherwise kama alivyodokeza mbunge Kessy tutarudi kule kule endapo tutakosa mtanzania mmoja wa kuwa Rais mwenye kufanana na Rais Magufuli.

@TumpeMudaZaidiMagufuli.
#MoreReformsMagufuliTena.

Tanzania 🇹🇿 kwanza 🙏🏼

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Tegemea cheo U- DC baada ya uchaguzi mkuu namba ulishasaviwa tayari
 
Mnaemsifia sifia ivyo nae mmemuonamo tu maana Vijana kwa unafiki hamjambo
 
Hivi shule mlienda kusomea ujinga!!?

Bado najiuliza mahusiano kati ya uliyoyaandika na viwango vyako vya elimu bado sijapata jibu... kwamba kuna logic umejaribu kuitoa ama mawazo yako ndio bora zaidi!??

Magufuli sio kila mtu anampenda na wasiompenda sio kama wana sababu binafsi Hapanaa.... bali machafu yake na madhaifu yake aliyoyaonesha 2015-2020 ni mengi na ovyo kuliko hayo mazuri mnayoyashikilia bango. Magufuli hapaswi kupewa hata miaka mitano mingine, atarudi kuiangamiza nchi kabisa...

Hivi Magufuli hajishtukii tuu!?
 
Kuna clip Fulani nyerere alikuwa anasimulia wkt akiwa madarakani mapema ktk awamu yake ya pili alitamani anyatuke aachie kijiti mwingne. Alipata pingamizi na sifa za kinafiki kuwa hakutatokea rais bora mwingne Kama yeye.

Baadae akaja gundua wale waliokuwa wanampigania asitafute kumbe hawakuwa na uhakika wa hatima ya vyeo vyao hapo baadae, hata hizi sarakasi za kumpamba jiwe ni wanasiasa wasio na uhakika wa ajira zao nje utawala wa jiwe
 
MORE MAGUFULI,MORE REFORMS,TUMUONGEZEE MUDA MAGUFULI.

Leo 16:15pm 10/06/2020

Maelezo ama narrative ya viongozi wengi awamu ya tatu na nne zilikuwa zina-reflect namna ya kugawana mapato ya Taifa la Tanzania,kuuza vitalu,kuuza madini,mikataba mibovu,

Kwa ujumla narrative za viongozi katika awamu zilizopita zilionyesha namna ya kugawana keki ya Taifa iliyokuwa inapatikana nchini,namna ya kuvuna vyeo,utajiri na kuzistawisha familia zao,

Awamu tatu zilizopita ukiwa na cheo Serikalini basi ulikuwa unakuwa maarufu hata kama taasisi yako ama Wizara yako haina uimara wala tija yoyote katika Taifa.

Rais Magufuli amebadili gia angani,amewatenga vinara wa ugavi wenye mazoea ya kugawana keki ya Taifa huku watu Milioni 60 wakibaki masikini wakichekwa hata na Kenya!

Yapo ambayo Rais Magufuli hajayasimamia kwa upungufu wa pato la Taifa lakini in the process anaendelea kurekebisha kila mahali ili pato liweze kuongezeka na kuwezesha kufanya mambo makubwa zaidi,

Rais Magufuli licha ya upungufu wa pato la Taifa amechagua miradi mikubwa ya kimkakati ya matrilioni ya hela ambayo kwa kweli japo inakula hela nyingi lakini ni ya manufaa sana kwa Taifa na ni miradi endelevu itayoleta tija kwa kizazi cha Sasa hata vizazi kumi vijavyo,

Tupo Watanzania Milioni 60 lakini nikiri wazi Magufuli ni mmoja tu kati ya watu Milioni 60,Magufuli mmoja anawakilisha takribani nusu ya Watanzania ambao sauti zao zilikuwa zinaminywa na Watanzania wachache matajiri,

Kwa miaka mingi Watanzania waliitaji mtu wa kuyasemea matatizo yao lakini hakupatikana hadi alipokuja Magufuli,ndio maana kila mtu anamuona Magufuli kama katoka sayari nyingine kwa kuwa Watanzania Milioni 60 kwa miaka 30 baada ya Nyerere walikosa Kiongozi anayemaanisha anachoongea na kufanya,

Niungane na kila mmoja kusema,Kama Magufuli atapata muda zaidi ina maana more reforms,mabadiliko zaidi,Viwanda zaidi,Uchumi wa nchi zaidi,Uadilifu zaidi,uchapakazi zaidi na Uzalendo zaidi,

Otherwise tuanze ku support hizi reforms anazofanya ili ziweze kujenga narrative mpya ya taifa na ziweze kujenga vigezo vipya vya aina ya uongozi tunaoutaka kwa nchi yetu, tuviingize kwenye mjadala wa taifa na ndivyo vitumike kupata kiongozi mpya baada ya Magufuli na wasomi wetu wabadilike na waanze kuwaza namna ya kubuni zana za uzalishaji mkubwa utakaotosheleza mahitaji yetu ya nchi na lifestyles zetu. otherwise kama alivyodokeza mbunge Kessy tutarudi kule kule endapo tutakosa mtanzania mmoja wa kuwa Rais mwenye kufanana na Rais Magufuli.

@TumpeMudaZaidiMagufuli.
#MoreReformsMagufuliTena.

Tanzania 🇹🇿 kwanza 🙏🏼

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.

Naunga mkono hoja
P
 
Kuna wakati binadamu tunajidhalilisha sana, ina maana mnaotaka aongezewe mda mnaamini hakuna wa Tz wengine wenye uwezo kama yeye au kuzidi yeye?
 
Back
Top Bottom