more discussions on contrversial Ngorongoro road | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

more discussions on contrversial Ngorongoro road

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jackbauer, Jun 2, 2012.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  source:Tanzania: More discussions on the controversial Ngorongoro road : NL-Aid
   
 2. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Wild life is Tanzania's, the road is for Tanzanian, and decision is by Tanzanians. Why opposition is foreign? I thing they have to fight Carbon emissions rather than concetrating on making the poor, poorer!
   
 3. p

  petrol JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Tatizo letu ni dogo sana, kutegemea wafadhili kutoka mataifa ya magharibi kugharamia ujenzi wa barabara hiyo. haya yanatukumbusha wakati wa ujenzi wa reli ya tazara. wakubwa wote wa magaharibi na benki ya dunia pamoja na IMF waligoma na kusema ilikuwa white elephant. Mwalimu Nyerere na Mzee Keneth Kaunda wakasema itajengwa kwa vyovyote vile. ndivyo ilivyotokea. Kwa barabara hii tuachane na mataifa ya magharibi, tutafute fedha zetu au marafiki wanaotuelewa na tuijenge. aibu ioje kama ilivyotokea hivi karibuni eti serikali ya Tanzania kubwagwa chini na NGO ya kenya kwenye mahakama ya africa mashariki. dharau za namna hii ni kudhalilisha utaifa wa taifa kubwa katika afrika mashariki. tusikubali. tusikubali kuwekewa ngumu na hata majirani zetu kwa sababu zao kama ilivyotokea kenya na rwanda kuwa vinara katika kushinikiza cites itupilie mbali ombi la Tanzania la kuuza vipusa vya ndovu. wakati umefika tufanye yote yenye kuleta maslahi kwa taifa. kuendekeza majirani na wengineo ni kuendelea kudumaza maendeleo ya taifa letu wakati ndio walioko mstari wa mbele kutucheka kwa umasikini wetu.
   
 4. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Mawazo ya kumtegemea mtu mwingine hiyo ni tabu,hivi wanaecology wetu,wahandisi,wanakazi gani maana tunachuo kikuu cha sokoine,mweka hakuna maprofesa wanaoweza kutoa ushauri wao kuhusu hio barabara ila sishangai kwani bunge lililopita tuliambiwa mkulo ameenda marekani kuandaa bajeti. Watanzania tupunguze kuwa tegemezi
   
 5. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wana JF, hivi reli ya TAZARA imepita SELOUS kumekuwa na shida gani? Barabara ya DAR to MBEYA imepita kati ya mbuga ya MIKUMI kuna tatizo lolote? Au sababu inawasaidia kupitisha mali zao? Mbona ninapita kila mara nakuta tembo, swala, twiga nk wapo kama kawa tena na askari wa pori wapo kibao? Mie naomba watanzania tusifuate mawazo ya hawa wanaopinga huo ujenzi wa hiyo barabara, kumbukeni kwenda mwanza tulikuwa ni lazima kupitia kenya, siku hizi hatupiti kwao, mkoa wa mara ni kati ya mikoa yenye ukaribu na kenya kwa kila kitu, kwa nini tusiwarahisishie usafiri? Wanasema wanyama wana-migrate kwani wanadhani katika Enviromental Impact assessment haijazingatiwa kwamba sisi ni ma-bogus ki namna hiyo, ile barabara itafungua biashara ukanda wa Mara. Tuangalie faida zaidi kwa upana wake!
   
 6. R

  RC. JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja barabara hii ijengwe kwani itatuletea heshima kubwa na kutupunguzia umaskini watu wa ngorongoro,mara, na pia itatunganisha watu wa mara na TANZANIA Kwani mpaka sasa hatuko TANZANIA Kama wengi wanavyo dhani.hoja nzuri TATA.
   
 7. m

  massai JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tajeni faida ya hiyo barabara,,kuna mazao gani yatapita huko?mnaijua hiyo njia au mnakurupuka tu?ni zao gani linatoka msoma au malighafi gani inatoka huko musoma kuja miji ya arusha au kwenda dar sokoni?ni hivi,hiyo lami jahkaya anaipigia kifua ili iwe rahisi kufika kwenye hoteli yake inaitwa bilila,hakuna kingine,mnaoisapoti poleni ukweli ndio huo
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  unataka kusema bilila lodge haifikiki kwa sasa?
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kama kuna mtu amewahi kufika ngorongoro atajua umuhimu wa barabara hii......
   
 10. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  tunapozungumzia ngorongor haina maana inapita kwenye caldera ila inapita njia panda ya natron mpaka inakuja kuingilia kleins gate via loliondo
   
 11. m

  massai JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kwani mwanza ilikua hufiki kabla yakuwekwa lami?au hujui umuhimu wa lami katika kuokoa muda na gharama?tunachopinga wana mazingira ni ile kuharibu ecology,uhalisia kama tunavyoiita mbuga za asili,sasa kwenye uasili lami ya nini?angalia jiografia ya tanzania,angalia musoma na uhusiano wa uwepo wa hiyo barabara na uwekwaji lami wake.huwezi ilinganisha barabara iliyopita mikumi na hii tunayoisema,angalia umuhimu kiuchumi na vilevile kama uboreshaji wa huduma za kijamii
   
 12. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama huwezi kusoma picha kubwa behind ''hao wanamazingira'' ni vyema ukakaa kimya.labda nikuulize tunalinda huo uhalisia kwa faida ya nani,kwa gharama ya nani na kwa ujira upi?hao wazungu wanamazingira wanashindwa kuzuia carbondioxide emmission huko USA halafu sisi ndio tunakomalia kulinda mazingira.
  tafakari kabla ya kujiita mwanamazingira halafu ukajiingiza kwenye kampeni usizofahamu chanzo na mwisho wake.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  najua, njia hiyo ushapita? Unajua ilivyo? Unajua adha wanayopata wakazi wa loliondo? Njia inahitajika si tu kurahisisha maisha ya wakazi wako bali hata kwenye kupeleka vyakula pia, haiwezekani wakategemea gulio, wachuuzi toka kenya wawaletee vyakula....
  Mahali gani huko unatumia masaa 6-8 kufika ukitokea arusha? Nyanyachungu 1 shilingi 100?
   
 14. S

  Skype JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena, yaani juzi tu nimetoka huko Ngorongoro aisee bei za vitu ziko juu mno.
   
 15. N

  Never Ever Give Up New Member

  #15
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi ni kwamba wananchi wana haki ya kupata huduma nzuri ya barabara bila kujali ni wapi wanakaa katika nchi hii.Lakini pia hoja ya wanamazingira imepatiwa uvumbuzi kwamba kipande cha barabara hiyo chenye urefu wa kilometa 53 kuanzia Kleins gate(loliondo) had Tabora B(Mugum) hakitawekwa LAMI ili kufanya uhalisi wa hifadhi Serengeti uendelee kuwepo lakin pia kusaidia magari yasiende kwa speed kubwa ili kuzuia wanyama wasigongwe ovyo na magari.Kwa upande wa faida za barabara hiyo Kiuchumi,ni kwamba,barabara hiyo itasaidia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zimedumaa katima maeneo ya ukanda huo mzima,kwa maana ya ukanda wa Ziwa mzima na Arusha na Moshi kwa mfano kusafirisha samaki kutoka Ziwa Victoria kuleta Arusha na Moshi.Pia itasaidia kukuza Utalii katika eneo zima la Loliondo Game Controlled Area na Serengeti kwa ujumla.Kwa wananchi wa wilaya ya Ngorongoro itasaidia kupatikana kwa usafiri wa uhakika na wa haraka na hivyo kufungua masoko ya mifugo yao kwa miji mikubwa ya Arusha na moshi.Vilelvile itasidia kupunguza gharama kubwa za usafirishaji kutoka Arusha-Loliondo au Mwanza-Loliondo na hivyo bei ya bidhaa kupungua na kusaidia wananchi maskini.Kwa taarifa tu ni kwamba sasa hivi mifugo yote kutoka wilayani ngorongoro inauzwa nchini Kenya kwa kukosa usafirishaji mzuri kutoka Loliondo hadi Arusha,kwaiyo sio ajabu wakenya wanaipinga hiyo barabara maana wanajua watakuwa wamepoteza cheap supply of raw material kwa nyama na viwanda vyao vita ngozi.Pia Wakenya wanaipinga barabara hiyo kwa sababu wanajua utalii utaboreka katika ene zima la Serengeti na hivyo kuwakozesha biashara kwa upande wao maana wanajua serengeti is by far beautiful kuliko Masai mara yao!!.Tunaomba watanzania wenzetu waache kufuta mkumbo na kupinga barabara ambayo inamaslahi kwa Taifa na kushabikia watu ambao wanatetea maslahi yao(wanamazingira na wakenya) binafsi.Kwa wale walobahatika kwenda kwa Babu wa Samunge naamini watajua hali ya barabara katika eneo hilo na kwa hakika wataunga mkono kwa ujenzi wa barabara nzuri kwa wananchi wa ngorongoro na mkoa wa Mara.
   
Loading...