Hakika.Huo ndiyo ukweli.
Katika Africa, uongozi umefanywa kuwa ni mahali pa wenye akili ndogo, maadili duni au mahali pa watu waliokosa mbinu nyingine za maisha. Na ndiyo maana watu hao hawapo tayari kuukosa uongozi iwe kwa shari au amani, maana wakikosa uongozi, wakale wapi?
Lakini ukweli ni kwamba, kama mbele ya safari mmemweka kipofu aongoze njia, yeye na ninyi mlio nyuma yake, hamwezi kufika mlikotaka kufika. Hii ndiyo sababu ya Afrika, na hasa Tanzania, hata ipite miaka mingapi, kwa aina za viongozi tunaokuwa nao, tutaendelea kuwa kama tulivyo.