Monduli kielelezo cha kushindwa mbinu za Lowassa

Monduli kielelezo cha kushindwa mbinu za Lowassa

Jacaranda

Member
Joined
Oct 23, 2011
Posts
45
Reaction score
20
Nilifika monduli usiku moja wa mwezi wa nne nikiwa na lengo la kulala siku moja na kesho kufanya kazi iliyonipeleka na kisha kurudi Arusha mjini.Usiku hua unaadaa,nikiwa bado njiani taa zilizokua zinang`aa upande wa sehemu makao ya mji wa monduli yalipojengwa yalinivutia sana na kunifanya nitamani kufika mapema ili nijimwagie maji ya moto kuondoa uchovu wa safari.Mungu si Athumani baada ya dakika chache nilifika salama na kupokelewa na mwenyeji wangu lakini bahati mbaya wakati naingia kwenye malango ya mji wa monduli umeme ulikatika na kuufanya mji mzima ugubikwe na giza tororo,kwa usiku huo umeme haukurudi na hivyo kunifanya nilale gizani tena bila kuoga kwani nilishindwa kuchemsha maji na nisingeweza kuoga maji ya baridi kwan hali ya hewa ilikua ni baridi sana

Kesho yake nilipoamka umeme ulikua bado haujarudi na hivyo ikanilazimu nivae nguo nilizosafiria ambazo zilikua zimejaa jasho na vumbi ila hizo zilikua ni afadhali kwan nilizokua nazo kwenye bag zilikua zimejikunja sana,nilipoelekea kwenye shughuli iliyonipeleka iliniawia vigumu kuitekeleza kwan presentation niliyokua naifanya illitaji presentation

Nilipomaliza kazi iliyonipeleka nikautembelea mji wa monduli na hii ndiyo analysis yangu,monduli ni mji mdogo ambao wakazi wake ukiwatazama utajua bila shaka wamekata tamaa,stand ya basi ni mbovu isiyo na hadhi ya kua ya wilaya,hospital ya wilaya inaongezewa majengo mengine ambayo inasemekana yametumia pesa nyingi toka kwa mbuge wao ila ukiyatazama majengo ayo ayaendani na thaman za pesa iliyotajwa,kwa kifupi mji wa monduli unaelezea kufeli kwa mbuge wake,mkuu wa wilaya yake na mkurugenzi wake,NB mpaka nilipoondoka jioni umeme ulikua bado haujarudi na nilijulishwa hali ndo iko hivi mara nyingi
 
muongo kabisa wala huyui unachokisema Lini watu wataacha uongo jamani hakuna jimbo lenye huduma kama monduli ingawa ni umasaini
 
Na kukipendeza utasikia huyu atashindwa kugawa vizuri rasilimali za nchi na kuwa na upendeleo, kuzipeleka kwao! Kwa nini asipimwe mtu kwa vipimo halisi???
 
Pointless....Monduli kwetu hapako hvyo licha ya kwamba ni porini....Mbona Dar umeme huwa unakatika siku au hata cku 2??Monduli kwetu tunaogea maji ya baridi ili kujiweka fiti zaidi.Siku ingine omba unyooshewe nguo
 
yan porojo nyingi nkajua ni wa maana kumbe hana lolote, next tym try to come with vivid argument other wise you failed..
 
Pointless....Monduli kwetu hapako hvyo licha ya kwamba ni porini....Mbona Dar umeme huwa unakatika siku au hata cku 2??Monduli kwetu tunaogea maji ya baridi ili kujiweka fiti zaidi.Siku ingine omba unyooshewe nguo

Halaf mondulini miongoni mwa wilaya zinaongoza kwa ukeketaji na ndoa za lazima watoto chini ya umri wa niaka 18.
 
Back
Top Bottom